Nigeria leo ni Sikukuu ya Eid El Fitr?

Nigeria leo ni Sikukuu ya Eid El Fitr?

Binafsi huwa nashindwa kuelewa kwa sababu Saudi Arabia mwezi ukiandama sehemu nyingine yoyote Duniani huwa hawafungui mpaka uonekane kwao, ila kwa hapa Tanzania Waislam wa Answar Sunnah wanasema ukionekana popote watu wanafungua, lakini Saudia wasipofungua na wao hawafungui hata kama nchi nyingine apart from Saudia utakuwa umeonekana, sasa hapa ndipo nnaposhindwa kuelewa hii concept ya mwezi muandamo.
Hizi zinazoitwa Imani za kiDini ni kwa manufaa ya watu fulani. Hakuna Nabii wala Mtume aliyekuwa muumini wa dini au dhehebu fulani...
 
Mungu anatajwa kama fiction tu ili utiwe hofu uwe mtii wa sheria za nchi bila shuriti. Mungu unaye wewe ndani ya ufahamu wako asilia. Unapaswa uamini habari za Mungu huko unakohubiriwa kwenye dini ili akili yako iwekwe sawa usiwe kaidi
Ina maana hakuna MUNGU wala Sheria zinazotokana na yeye kiongozi...?
 
Wewe unaishi "outer space"?

Huwezi kuwa na mwezi "outer space" ambapo hakuna sayari. Mwezi au Miezi (satellite moons) hukaa karibu na sayari.

kafanye homework yako.
Dada kama dada...! 😅
 
Sasa hawa wanaofunga ikitokea mwezi ukaandama kabla ya siku 30 hawatavusha siku ili itimie 30? Mbona hapo itakuwa ni abrakadabra za binadamu kujiamulia siku za kufunga na Mungu hahusiki hapo
Hapana mwezi hata ukiandama siku ya 29 watakuwa wamefunga siku 29 which is right kwa sababu kuna miezi mirefu na miezi mifupi mkuu.
 
Back
Top Bottom