Nigeria: Watu nane wakamatwa na Polisi kwa kosa la kula mchana mwezi wa Ramadhani

Nigeria: Watu nane wakamatwa na Polisi kwa kosa la kula mchana mwezi wa Ramadhani

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Watu wanane wamekamatwa na polisi wa Kiislamu katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria Kano kwa madai ya kukataa kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

17742938_303.jpeg


Polisi wa Hisbah wanasimamia sheria za Kiislam huko Kano – moja ya majimbo 12 ya Waislamu kaskazini mwa Nigeria wanaotumia mfumo wa sheria wa Sharia pamoja na sheria za kidunia za nchi hiyo.

“Wahusika walikuwa wanawake watano na wanaume watatu, wakila alasiri katika mwezi wa Ramadhan,” Aliyu Kibiya, Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Hisbah Jimbo la Kano alinukuliwa akisema.

Kufunga kwa watu wazima ni suala la wajibu hasa kwa wale wenye uwezo wa kutokula na kunywa.


Walio wagonjwa na wale ambao wanaweza kupata athari za kiafya iwapo watafunga kula na kunywa, wakiwemo watoto, wanawake wajawazito, wasafiri na wanawake wanaonyonyesha.

Kwa mujibu wa BBC wanawake hao waliiambia Hisbah kwamba walikuwa na msamaha kwa kuwa wako kwenye hedhi, lakini polisi waliwaambia pamoja na hali hiyo hawakupaswa kula hadharani.

Ikiwa watashtakiwa mahakamani, wanaweza kulipishwa faini au kupelekwa kwa taasisi ya marekebisho ya tabia.

Taarifa ya Bw Kibiya ilionya kuwa uvamizi zaidi utafanywa katika jimbo lote kuhakikisha watu wanazingatia wajibu wao wa kidini.
 
Kufunga kwa Muislamu mwenye afya ambaye hana tatizo lolote la kiafya ni lazima.
Kwa maana nyingine ni lazima mtu aione pepo?

Naamini kwamba, uislamu na ukristo msingi wake mkuu ni mafundisho ya vitabu vitakatifu pamoja na free will aliyonayo mwanadamu kufuata mafundisho hayo au kuyapotezea.

Sasa inakuwaje mtu ameamua kuikataa pepo alazimishwe wakati huo huo unasema huyo mwanadamu ana free will kuchagua kwenda mbinguni au motoni!
 
Johnny Impact kuwa na adabu, na heshimu imani za watu! Unaposema uislamu ni ugaidi unakosea sana..

Pumzi inakuhadaa, kuwa makini na kauli zako!
 
[emoji16][emoji16]. kwanini mnatuchukia waislam ?.tumewakosea nini?.
Mbona hata wakristo nao wanafanya.
Kuna dada Huku kitaa ana makalio makubwa anasema hapendi waislam.
Sijui waislam walimfanya nini
Na kwa mpalangee[emoji57][emoji57]
 
Back
Top Bottom