Hahaha
Kazi ipo
Hivi Unajua kisa cha Baba wa taifa la Tanzania kutofautiana kabisa na Kenyatta jambo moja kubwa ilikuwa ni baada ya Kenyatta kukataa kata katu kuunganisha Kenya na Tanzania na nchi nyingine ziwe nchi moja?
Na inawapasa kati ya mambo ambayo mnatakiwa mumchukie Kenyatta ni kukataa hii offer ya Nyerere na kati ya mambo Watanzania tunapaswa kumkosoa Nyerere ni kufikiria hili suala (sio baya lakini ni kwa wrong people)
Fikiria saivi kungekuwa hakuna tofauti kati ya mkazi wa Turkana jangwani mle na mkazi wa Morogoro peponi, yaani mtu kutoka Wajiir angeweza kwenda Chunya kuanzisha mgodi wake wa madini ya dhahabu kama waunguja wanavyotoka unguja na kumiliki biashara na utajiri Kigoma.
Nyerere dhamira yake ilikuwa safi kabisa tena alimuambia Kenyatta mimi nipo tayari hata kesho wewe uwe Rais kabisa wa hiyo unified political federation lakini Mungu alivyo waajabu na alikua akituwazia watamzania mema aliweka moyo mgumu kwa Kenyatta
Na hivyo hivyo Nyerere alitaka kwa Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia, Zimbabwe mpaka South Africa in fact SADC ya kwanza kabisa iliundwa Tanzania japo ile ilikuwa ni SADC ya kijeshi au ukombozi wa nchi za kusini, target ikiwa kuja kuunda dola moja ndio maana Nyerere alijitoa kwa vyote, then baadae ndio ikawa economic oriented SADC lakini ni wazo la Nyerere kabisa
Sasa kati ya Kenya na Tanzania nani mwenye uhalali wa kumuita mwenzake alikumbatia mipaka ya kikoloni? Na ya heri ukumbatie mipaka ya ukoloni kuliko kukumbatia mipaka ya ukabila sababu hapo unafanya akili ya mkoloni iwe bora yako mara million.
Kuhusu ugunduzi wa gas madini, vyote hivi viligunduliwa na Nyerere miaka ya 60 huko, kitu Nyerere Alisema ni kwamba "hizi rasilimali za ardhini ziachwe hivi hivi mpaka watoto wetu watakapopata maarifa na uwezo wa kuvitumia wenyewe kwa manufaa"
Na kwa kipindi chote Nyerere alivyokuwa hai hakukuwa na company yoyote ya kigeni ya uchimbaji wa kitu chochote Tanzania bali baada ya Nyerere kufa tu ndio huo mwiko ulivunjwa, kwa hiyo kusema tulikuwa tukipanda mihogo tukose kujua kilichomo chini inaonesha ni jinsi gani unavyokurupuka, pale Dodoma ipo maktaba kubwa kuliko zote Africa ya geological arrangements za Tanzania na pale University of Dar es salaam tokea enzi ya mjerumani 18000s mpaka leo kwa hiyo kila kitu kilijulikana kilipo kila eneo.