Night Clubs kufa sio kwa Tanzania tu, Dunia nzima night club culture inakufa kwa sababu kizazi Z hakipendi Clubs

Watu wengi wamekua wakijiuliza kwa nini siku hizi night clubs zinakufa sana, mfano Maison na nyinginezo hapa Tanzania.

Ukweli ni kwamba night Clubs Dunia nzima zinakufa kwa sababu kizazi Z ambao ndio walipaswa kua wanaruka majoka usiku kucha hakipendi kwenda night Clubs.

Sababu nyingine ni kwamba kipindi hiki bar ama migahawa mingi ya mtaani inatoa burudani ya muziki usiku kucha huku bei ya vinywaji ikiwa ni ile ile, so mtu anaburudika hadi asubuhi kwa bei ndogo tofauti na kwenda clubs. Migahawa na bars nyingi za mtaani wameajiri professional DJs wale waliokua wanapiga ngoma clubs na kununua vifaa vya kisasa vya muziki ambavyo havikua vinapatikana huko nyuma.

Watu wengi wanasema waliacha kwenda clubs kwa sababu ya clubs kuingiza utamaduni wa meza, kununua meza na pia bei ghali ya vinjwaji kuliko uhalisia.

Zaidi ni kwamba ujio wa mitandao ya kijamii imevuruga zaidi hasa kwa kizazi Z wakitumia muda mwingi zaidi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kukutana clubs.

Kizazi 'Z' ndiyo aina gani ya binadamu?
 
Mimi wa kazulamimba nielewesheni tofauti ya Lounge na Club wakuu
Naweza nisiwe sahihi pia mkuu;

Lounge - zipo kwa ajili ya casual gatherings, meetings za kibiashara, mazungumzo ya karibu, yaani mnalewa kistaarabu, mziki laini n.k japo wabongo lounge tuna maana yetu tofauti zinapigwa amapiano mtapoteana na hizo business meetings zenu.

Club - ni kwa ajili ya loud music, kucheza, let loose, kujiachia, unajisahau for a day kesho wakusimulie ulivoleta mabalaa

Haya ni mawazo yangu mkuu sina uelewa sana naweza kuwa siko sahihi pia
 
Ulivyoandika nimecheka mkuu dah 🤣🤣
 
Hewaaaa na miziki yetu ya zilipendwa
Taratibu na konyagi Pembeni
Open bar ndio mpango mzima, kwanza clubs hewa yenyewe nzito hata AC zikiwashwa hasa kama watu ni wengi.
Hata kiusalama clubs sio, yaani mnafungiwa sehemu moja halafu exit ndogo, ikitokea ajali ya moto n.k its too dangerous.

Ndio maana sisi wazee tunaenda zetu live band
 
Hewaaaa na miziki yetu ya zilipendwa
Taratibu na konyagi Pembeni
Hivi konyagi OG zinapatikana wapi, nilikuta watu wana sample Hennessy.

Kuna ulazima viwanda vya pombe kali kufungua authorized dealers au maduka yao maalumu, sticker za TRA hazitoshi.
 
kizazi antisocial sana.......muda mwingi kwenye screen
 
Kila Zama na Kitabu Chake....

To each their Own....
 
Hivi konyagi OG zinapatikana wapi, nilikuta watu wana sample Hennessy.

Kuna ulazima viwanda vya pombe kali kufungua authorized dealers au maduka yao maalumu, sticker za TRA hazitoshi.
Mkuu fake zimekuwa nyingi sana na ukiwa mzee wa kufakamia kila chimbo utakunywa konyagi za kina
Massawe walizotengeneza uchochoroni
 
Watu wengi wamekua wakijiuliza kwa nini siku hizi night clubs zinakufa sana, mfano Maison na nyinginezo hapa Tanzania.

Ukweli ni kwamba night Clubs Dunia nzima zinakufa kwa sababu kizazi Z ambao ndio walipaswa kua wanaruka majoka usiku kucha hakipendi kwenda night Clubs.

Sababu nyingine ni kwamba kipindi hiki bar ama migahawa mingi ya mtaani inatoa burudani ya muziki usiku kucha huku bei ya vinywaji ikiwa ni ile ile, so mtu anaburudika hadi asubuhi kwa bei ndogo tofauti na kwenda clubs. Migahawa na bars nyingi za mtaani wameajiri professional DJs wale waliokua wanapiga ngoma clubs na kununua vifaa vya kisasa vya muziki ambavyo havikua vinapatikana huko nyuma.

Watu wengi wanasema waliacha kwenda clubs kwa sababu ya clubs kuingiza utamaduni wa meza, kununua meza na pia bei ghali ya vinjwaji kuliko uhalisia.

Zaidi ni kwamba ujio wa mitandao ya kijamii imevuruga zaidi hasa kwa kizazi Z wakitumia muda mwingi zaidi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kukutana clubs.

Duuh
 
Back
Top Bottom