Nihifadhi wapi akiba yangu ya fedha ili nipate faida ya angalau asilimia 10 kwa mwaka?

Nihifadhi wapi akiba yangu ya fedha ili nipate faida ya angalau asilimia 10 kwa mwaka?

Alfredy1993

New Member
Joined
Sep 26, 2017
Posts
3
Reaction score
6
Habari ndugu zangu,

Mimi nataka kuanza kuwekeza pesa zangu za ziada lakini sijui nihifadhi wapi ambako nitajitengezea angalau faida ya asilimia 10 kwa mwaka!

Naomba msaada kwa anayejua
 
Kwa nini mkuu usitafute namna ya kuwekeza iyo pesa. Kuna mtu kashauri UTT ni nzuri. Kuna mtu kashauri stock tatizo market stock ya kampuni nyingi bongo hazikui.

Usijaribu cryptocurrency bila kua knowledgeable
 
Habari ndugu zangu, mimi nataka kuanza kuwekeza pesa zangu za ziada sasa sijui nihifadhi wapi ambako nitajitengezea angalau faida ya asilimia 10 kwa mwaka! Naomba msaada kwa anayejua
Kanunue hati fungani BOT na unaweza ukapata hata zaidi ya asilimia 10 kulingana na muda unaotarajia kuwekeza. Kwa taarifa zaidi ingia kwenye website yao, simply google!
 
Habari ndugu zangu,

Mimi nataka kuanza kuwekeza pesa zangu za ziada lakini sijui nihifadhi wapi ambako nitajitengezea angalau faida ya asilimia 10 kwa mwaka!

Naomba msaada kwa anayejua
Kama inafika 20M ni kopeshe for 3 yrs nitakupa 200%
 
Kanunue hati fungani BOT na unaweza ukapata hata zaidi ya asilimia 10 kulingana na muda unaotarajia kuwekeza. Kwa taarifa zaidi ingia kwenye website yao, simply google!
Kwani hati fungani za BOT unaweza anza kununua za shilingi ngapi(kiwango cha chini cha kununua)?
 
Kwani hati fungani za BOT unaweza anza kununua za shilingi ngapi(kiwango cha chini cha kununua)?
Ingia kwenye website yao BOT kila kitu kipo hadi calculator ya kukuonyesha faida utakayolipwa
 
Habari ndugu zangu,

Mimi nataka kuanza kuwekeza pesa zangu za ziada lakini sijui nihifadhi wapi ambako nitajitengezea angalau faida ya asilimia 10 kwa mwaka!

Naomba msaada kwa anayejua
Tafuta Vijana waaminifu watano (5) esp. Me. ingia nao Mkataba wa Biashara (Biashara ndogo-ndogo less than 300,000/=) na marejesho yawe ni kila mwezi 10%. Chunguza/Jifunze kwa waendesha bodaboda. Kila wiki 40,000/= au kila siku 7,000/= au shughuli inayofanana na hizo. Wengine hutumia fedha yako kufanya biashara na kile kinachopatikana huchukua cha juu na ww wanakupa albaki!🤪
 
Back
Top Bottom