Mavurunza
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 230
- 172
Mkuu ushauri wanguHabari ndugu zangu,
Mimi nataka kuanza kuwekeza pesa zangu za ziada lakini sijui nihifadhi wapi ambako nitajitengezea angalau faida ya asilimia 10 kwa mwaka!
Naomba msaada kwa anayejua
1. Wekeza kwenye hati fungani. Hii ni low risk investment ila inataka mtaji mkubwa ili uweze kuona faida ya maana.
2. Wekeza kwenye ardhi hasa kama unaishi maeneo ya Dar. Hakuna sehemu ambayo ardhi ya Dar inashuka thamani. Hapa risk yake ni kuwa makini wakati wa manunuzi usije ukaingia mikononi mwa matapeli.
3. Cryptocurrency. Hii high risk investment lakini ulipaji wake ni mkubwa sana. Kwa mwaka unaweza kupata faida hata mara 100 ya uwekezaji wako. Hii ni nzuri kwa mtu mwenye lengo la kuwekeza kwa muda mrefu kwani kuna kipindi coin zinashuka sana thamani kabla ya kupanda kwa fujo. Uwekezaji huu unakubidi utafute maarifa sahihi kwanza na kujiridhisha kabla ya kuwekeza.