Pole sana ila ni simpo tuu.. Mara nyingi soda huwa haikati kiu kabisa.. Ndio maana umesema huwa unaanza na soda halafu baadaye unakunywa maji, that means maji yanayokukata kiu.
Wengi tuliweza kwa kugeuza unaweza kununua soda kama unavyotaka, lakini hakikisha umenunua na maji tena makubwa.
Kisha hata kama unaitamani soda kiasi gani.. Anza na maji.. Kunywa maji ya kutosha, gugumia chupa yako halafu ukiiangalia soda utaona huna hamu nayo kwa wakati huo utaamua kuiweka pembeni kwanza..
Hata ukiinywa utakunywa kidogo sana na la muhimu ni kuwa maj yashatangulia ya kutosha.
Hata uwe na hamu ya soda kiasi gani ukianza tu kunywa maji ile kiu na hamu ya soda huwa inakata kabisa, lakini ukianza na soda unaweza ukanywa hata chupa mbili na bado kiu ipo na lazima utalazimika kunywa maji ndio utakuwa okay.. So just do vice versa utakuwa umetibu tatizo kirahisi sana.
Nyongeza ni vema uwe unanunua vile vichupa vidogo vya soda usisithubutu kununua chupa kubwa.. Kuna kaushamba fulani tunako waswahili eti mtu anadhani zile size ndogo ni kwaajili ya watoto no no no.. Au eti utaonekana huna hela hiiiii learn to mind your business.
Kile ni kipimo kizuri kwa mtu mzima mls 250 hadi 300 usizidishe hapo utakufa na utagundua hao uliokuwa unawaogopa au kuwaonea aibu ulikuwa tuu ni ujinga wako tuu maana hakuna aliyekuwa na time na wewe.. Ni kunishtukia tuu.
Mimi ukiona ninavyokula hotelin au mgahawani utanishangaa nipo very very selective.. Ni afadhali nishinde njaa kuliko kula kitu ambacho najua kitaniletea shida.. Huwa sili kabisa.
Mimi nakula mchemsho tuu usitiwa tiwa sijui nini au macuta mafuta, asubuhi, jimbi, mihogo, viazi mtori plain, vitafunwa vya mafuta nadra na nakula kwa hamu tu au kama hakuna alternative basi nitakula kidogo sana.
Juice za viwandani ndio mauaji ya halaiki yaani baada ya miaka michache hili taifa sijui litabaki na kina nani???? [emoji848]
Unakuta eti mtu hanywi pombe jambo jema kabisa halafu anakunywa kopo zima la Azam juice peke yake kwenye masherehe na mwingine anapewa makopo 2 na anajisifu eti alichangia fedha kubwa halafu asinywe wee.. Yaani mchango wako mwenyewe unakuuaa???
Ana unafuu mlevi kuliko mnywa juice 🧃 ilijazwa masukari ya viwandani na masweetener hatari kabisa.
Vifo vya kujiua Tanzania ni vingi mno mno sijui huko kwa Mungu Tutajibu nini??