Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
- Thread starter
-
- #21
kwa matazamo wako nani alikuwa fundi zaidi ya mwenzake?Beki 5 ya Yanga,
Alikua mtu mmoja serious na smart sana,
Ujio wake Yanga ulileta Changamoto kwa Beki 5 ya Simba ya wakati huo, George Magere Masatu (GM).
Changamoto ilikua kwamba nani Beki 5 bora kwa wakati huo.
Mstari wa nyuma toka kushoto: Salum Kabunda "Ninja", Constantine Kimanda, Steven Nemes, Keneth Pius Mkapa, Suleiman MkatiKimanda ndio yupi hapo?
Ingawa Mi ni Mnazi wa Kutupwa wa Simba, nadhani Kimanda alimzidi GM.kwa matazamo wako nani alikuwa fundi zaidi ya mwenzake?
Kimanda alicheza vizuri sana alipoongezewa nguvu na Method Mogella, kwa upande wa Massatu alicheza na tofauti tofauti mabeki wengi sana na alidumu kwenye ubora wake mpaka anastaafu sokakwa matazamo wako nani alikuwa fundi zaidi ya mwenzake?
Mstari wa nyuma toka kushoto: Salum Kabunda "Ninja", Constantine Kimanda, Steven Nemes, Keneth Pius Mkapa, Suleiman MkatiVuta kumbukizi ya hii mechi
Hapana, Damian Mrisho "Kimti" alikua Mkigoma,Damian Kimti ni Mrundi kumbe?
Halafu vuta picha ya mzozo wa Said Maulid "SMG". Yalitafutwa mpaka madaftari yake ya darasa la sita!Hapana, Damian Mrisho "Kimti" alikua Mkigoma,
Urundi wake ulikuja baada ya kua aliifunga kila timu iliyokutana na Simba enzi hizo,
Timu zikafululizana FAT kukata rufaa kua si Mtanzania,
Mwisho wa siku FAT iliztupilia mbali rufaa hizo ila jina la Mrundi ndio likaanzia hapo,
Kabla ya kufululiza kuzifunga hizo timu hakuna aliewaza kua ni Mrundi
uko vzr mzee!Mstari wa nyuma toka kushoto: Salum Kabunda "Ninja", Constantine Kimanda, Steven Nemes, Keneth Pius Mkapa, Suleiman Mkati
Mstari wa mbele toka kushoto: Nico Bambaga (RIP), Sekilojo Chambua, Edibily Jonas Lunyamila, James Tungaraza "Boli Zozo" (RIP) na Said Mwamba "Kizota " (RIP)
Nimekusoma vyema sana!Hapana, Damian Mrisho "Kimti" alikua Mkigoma,
Urundi wake ulikuja baada ya kua aliifunga kila timu iliyokutana na Simba enzi hizo,
Timu zikafululizana FAT kukata rufaa kua si Mtanzania,
Mwisho wa siku FAT iliztupilia mbali rufaa hizo ila jina la Mrundi ndio likaanzia hapo,
Kabla ya kufululiza kuzifunga hizo timu hakuna aliewaza kua ni Mrundi
Mohamed Hussein Machinga. Striker wetu, Dar Es Salaam Young Africans baby
Constantine Kimanda
Constatine Kimanda alikuwa ni beki wa kati au mkoba wa Yanga na timu ya taifa ya Burundi na sio Congo DRC.
Ilikuwa ni mwaka 1994 alipochezea Yanga ambapo alisajiliwa chini ya uongozi wa katibu mkuu wa wakati ule marehemu George Mpondela.
Alikuwa pamoja na marehemu Method Mogella ambae waliuzwa wote na Mpondela kwenye timu ya uarabuni ya Sharjah FC.
Yanga ya mwaka 1994 ilikuwa ni kali kwelikweli kina Steven Nemes Sekilojo Chambua, Mohamed Hussein au "Mmachinga", Nico Bambaga, Edibily Lunyamila, James Tungaraza "Boli Zozo", na Salvatory Edward.
Wengine akina Said Mwamba Kizota, marehemu Salum Kabunda "Ninja", Issa Athuman, Keneth Mkapa, Selemani Mkati, Rifati Said, Sanifu Lazaro, David Mjanja na Mwanamtwa Kihwelu.
Wachezaji wengine walikuwa ni Allly Yusuf "Tigana", Willy Martin, Ngadu Ramadhan, Joseph Lazaro, Willy Mtendamema.
Mwaka 1994 ndipo kulitokea mgogoro mkubwa kwenye klabu hii na kukazaliwa Yanga Asili na Yanga kampuni.
Hivyo Yanga kampuni chini ya Marehemu Mpondela ikaenda kufungwa goli 4-1 na Simba na baaada ya hapo wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wakatimuliwa.
Kimanda ndiye aliefunga goli pekee la Yanga.
Baada ya mgogoro huo kipa Rifat Said alirudi Zanzibar, Edibily Lunyamila akaenda Malindi ya Zanzibar na Saidi Mwamba pamija na Steven Nemes wakahamia Simba.
Ndipo Kocha wa Yanga Tambwe Leya akaamua kusuka kikosi kipya cha Yanga kilichokuwa na wachezaji kama Anwar Awadh, Mzee Abdallah, Silvatus Ibrahim “Polisi”, Maalim Saleh “Romario”, Nonda Shaaban “Papii”, Bakari Malima na Kally Ongala.
Wengine akina Seki Chambua Salvatory Edward na wengine.
Vijana hawa waloitwa Black Stars ndiyo waloiwezesha Yanga kuja kucheza nane bora mwaka 1998 ya klabu bingwa Afrika na baadae mwaka 1999 wakanyakuwa ubingwa wa Afrika Mashariki.
Edibily Lunyamila na Mohamed Hussein.
Kimanda kwa sasa anaishi na kufanya kazi nchini Ubelgiji.
Mohamed Hussein Machinga. Striker wetu, Dar Es Salaam Young Africans baby
NDIO WEWE NINI KIONGOZI ?
Nakumbuka enzi aileeee akiwa pale kwetu Ntwala pembeni yake alikuwa Amlima, nami nilikuwa .....NDIO WEWE NINI KIONGOZI ?
Nico Bambaga hajafa banaMstari wa nyuma toka kushoto: Salum Kabunda "Ninja", Constantine Kimanda, Steven Nemes, Keneth Pius Mkapa, Suleiman Mkati
Mstari wa mbele toka kushoto: Nico Bambaga (RIP), Sekilojo Chambua, Edibily Jonas Lunyamila, James Tungaraza "Boli Zozo" (RIP) na Said Mwamba "Kizota " (RIP)
Pitia hapaNico Bambaga hajafa bana
Timu kali kama hii utaifungaje kwa mfano?Mstari wa nyuma toka kushoto: Salum Kabunda "Ninja", Constantine Kimanda, Steven Nemes, Keneth Pius Mkapa, Suleiman Mkati
Mstari wa mbele toka kushoto: Nico Bambaga (RIP), Sekilojo Chambua, Edibily Jonas Lunyamila, James Tungaraza "Boli Zozo" (RIP) na Said Mwamba "Kizota " (RIP)
Duh R.I.PPitia hapa
Nico bambaga hatunaye
Huyu Jamaa alinifurahisha kitu kimoja tu,
Akiwa Bandari Mtwara alijenga kombinesheni safi sana na Idifonse Amlima.Huyu Jamaa alinifurahisha kitu kimoja tu,
Pamoja na kua Kibonge ana kitambi lakini alikua fundi sana wa kubinuka Samasoti pale atupiapo kambani, kama vile Julius Aghahowa wa Nigeria
We jamaa unazinguaYupo mtaani kwetu anaendesha boda boda