Nijuzeni: Costantine Kimanda alikuwa ni mchezaji wa aina gani?

Nijuzeni: Costantine Kimanda alikuwa ni mchezaji wa aina gani?

kimdanda..jpg

Constantine Kimanda

Constatine Kimanda alikuwa ni beki wa kati au mkoba wa Yanga na timu ya taifa ya Burundi na sio Congo DRC.

Ilikuwa ni mwaka 1994 alipochezea Yanga ambapo alisajiliwa chini ya uongozi wa katibu mkuu wa wakati ule marehemu George Mpondela.

Alikuwa pamoja na marehemu Method Mogella ambae waliuzwa wote na Mpondela kwenye timu ya uarabuni ya Sharjah FC.

Yanga ya mwaka 1994 ilikuwa ni kali kwelikweli kina Steven Nemes Sekilojo Chambua, Mohamed Hussein au "Mmachinga", Nico Bambaga, Edibily Lunyamila, James Tungaraza "Boli Zozo", na Salvatory Edward.

Wengine akina Said Mwamba Kizota, marehemu Salum Kabunda "Ninja", Issa Athuman, Keneth Mkapa, Selemani Mkati, Rifati Said, Sanifu Lazaro, David Mjanja na Mwanamtwa Kihwelu.

Wachezaji wengine walikuwa ni Allly Yusuf "Tigana", Willy Martin, Ngadu Ramadhan, Joseph Lazaro, Willy Mtendamema.

Mwaka 1994 ndipo kulitokea mgogoro mkubwa kwenye klabu hii na kukazaliwa Yanga Asili na Yanga kampuni.

Hivyo Yanga kampuni chini ya Marehemu Mpondela ikaenda kufungwa goli 4-1 na Simba na baaada ya hapo wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wakatimuliwa.

Kimanda ndiye aliefunga goli pekee la Yanga.

Baada ya mgogoro huo kipa Rifat Said alirudi Zanzibar, Edibily Lunyamila akaenda Malindi ya Zanzibar na Saidi Mwamba pamija na Steven Nemes wakahamia Simba.

Ndipo Kocha wa Yanga Tambwe Leya akaamua kusuka kikosi kipya cha Yanga kilichokuwa na wachezaji kama Anwar Awadh, Mzee Abdallah, Silvatus Ibrahim “Polisi”, Maalim Saleh “Romario”, Nonda Shaaban “Papii”, Bakari Malima na Kally Ongala.

Wengine akina Seki Chambua Salvatory Edward na wengine.

Vijana hawa waloitwa Black Stars ndiyo waloiwezesha Yanga kuja kucheza nane bora mwaka 1998 ya klabu bingwa Afrika na baadae mwaka 1999 wakanyakuwa ubingwa wa Afrika Mashariki.

20130318-181403.jpg

Edibily Lunyamila na Mohamed Hussein.

Kimanda kwa sasa anaishi na kufanya kazi nchini Ubelgiji.
Nimekubali mchango wako!
 
Nimekumbuka kikosi cha kina eustas bajuala beki WA kushoto WA yanga mwaka 99 kiliwafunga nakivubo sports club villa kampala na kuchukua kombe la afrika mashariki na kati.
serikali ikatuma ndege kwenda kuchukua timu Uganda waziri mkuu sumaye akaipokea timu airport.

Unamkumbuka Beki Patrick Ntambwe
 
Mohamed Hussein ndiyo ameweka rekodi ya kufunga goli nyingi kwenye ligi ya Tz
 
Constantine Kimanda na Ngadou Ramadhani hawa walikuwa ni wachezaji wa timu ya taifa ya Burundi baada ya kutoka nchini kwao na kwenda kwenye mashindano kukatokea vurugu wakashindwa kurudi kwao walipotua nchini RIP ABAS GULAMALI akawasaji.

Ilikuwa pacha hatari ya Rip Method Mogella na Constantine Kimanda hawa kwa pamoja waliuzwa Arabuni lkn Rip Method akarudi nchini.

Constantine Kimanda alipendwa mno Arabuni kiasi waligomea offer ya kumuuza Belgium akaamua kutoroka na Timu ya Arabuni ikashtaki FiFa Constantine Kimanda akafungiwa na Fifa miaka 5.

Yupo Belgium anafanya shughuli zake hili ni kwa hisani ya Bita John alinisimulia siku moja kwa kuwa walicheza naye Arabuni.
 
Back
Top Bottom