Nijuzeni: Costantine Kimanda alikuwa ni mchezaji wa aina gani?

Timu kali kama hii utaifungaje kwa mfano?
Ilichabangwa 4 kwa 1 na Simba, mwaka 1994, Mzee wa Kiminyio Madaraka Selemani alimtesa Kimanda kweli kweli, baada ya hapo Kimanda alikimbilia uarabuni, ni enzi za Yanga kandambili RIP Mpondela
 
Nimekubali mchango wako!
 
Mkuu Konaball kweli wewe mhenga. Boli Zozo wa Stela Club Adjame ya CIV.
Alicheza mechi mbili, mechi ya kwanza Yanga ilishinda goli 2-0 magoli yote yalifungwa na marehemu James Tungaraza aka Boli Zozo .
 

Unamkumbuka Beki Patrick Ntambwe
 
Mohamed Hussein ndiyo ameweka rekodi ya kufunga goli nyingi kwenye ligi ya Tz
 
Constantine Kimanda na Ngadou Ramadhani hawa walikuwa ni wachezaji wa timu ya taifa ya Burundi baada ya kutoka nchini kwao na kwenda kwenye mashindano kukatokea vurugu wakashindwa kurudi kwao walipotua nchini RIP ABAS GULAMALI akawasaji.

Ilikuwa pacha hatari ya Rip Method Mogella na Constantine Kimanda hawa kwa pamoja waliuzwa Arabuni lkn Rip Method akarudi nchini.

Constantine Kimanda alipendwa mno Arabuni kiasi waligomea offer ya kumuuza Belgium akaamua kutoroka na Timu ya Arabuni ikashtaki FiFa Constantine Kimanda akafungiwa na Fifa miaka 5.

Yupo Belgium anafanya shughuli zake hili ni kwa hisani ya Bita John alinisimulia siku moja kwa kuwa walicheza naye Arabuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…