Nijuzeni kiini cha maarifa ya kichanga kuanza kulishwa chakula baada ya miezi SITA toka azaliwe

Nijuzeni kiini cha maarifa ya kichanga kuanza kulishwa chakula baada ya miezi SITA toka azaliwe

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Kuna mwenye kujua history ilianzaje mpaka wahenga wakagundua mtoto akizaliwa akae miezi SITA bila kula chochote hata maji..

Na je mwanzo pengine walikuwa hawana hio akili wakawa wanalishwa ndani ya miezi miwili au mitatu tumbo halijakomaa je ilikuaje wali survive kweli hao watoto?

Kuna madhara makubwa kiasi Gani kwa mtoto aliyekomaa na kuanza kukaa kaa ila mdogo wa chini ya miezi mitano ukampa maji?
 
Sijui chochote, nachojua wanaanza na maziwa ya mama, kisha uji mlaini mwisho wanamalizia na dona ngumu kama ile ya uwele.
 
Hii sio ishu ya wahenga, hii ni sayansi.

Mtoto anakuwa hajakomaa mpaka kulishwa vyakula vigumu tofauti na maziwa ya mama.

Mambo ya wahenga, ambayo pia ni imani potofu ni ishu ya kubemenda.
 
Jiandae kuna virutubisho kwenye unga, mafuta ya kula na chumvi vitaongezwa kwaajili ya kukupa akili ili uweze kuvumbua ndege kama wazungu. Hili halina ubishi
 
Uji ni chakula kwani?
Kwani we unahisije...?!
Mmeng'enyo wa uji na ule wa maziwa unahisi ni sawa?

Uji una some sold particles. Obviously end product yake huwezi linganisha na ile ya maziwa.
Kimba la uji lazima litakuwa na ugumu kiasi kulinganisha na lile litokanalo na maziwa{lojolojo}.

Hivyo uji ni msosi tena heavy kabisa!
Mtoto chini ya miezi mitano anatakiwa agide maziwa ya mama coz yana virutubisho vingi ktk ukuaji wake na kujenga mfumo wa mwili kiujumla.
Toto chini ya umri huo, ukilizoesha mamisosi magumumagumu hata ukuaji wake utadumaa na litakuwa lakulaku na mtumbo utafutuka kama wa "churamagamba" kuliko uhalisia wa mwili wake.
Hii kitu ni mambo ya kisayansi sio wahenga.
 
Nimependa hiyo sayansi yako ya mchongo.
Uji ukitoa sijui wa lishe ni 98% carbohydrates.Kutia nguvu, mtoto nguvu za nini?

Mtoto ili akuwe anahitaji Protein kwa wingi kujenga mwili. Kama maziwa ya mama ni kidogo au mambo mengine ya ubize na kazi basi kisayansi kikombe Cha supu ya utumbo au kongoro ni bora kwa afya.

No wonder kisukari na nguvu za kiume ni janga coz tunaanza sugar(carb) addiction kwa watoto mapema sana.
 
Tumbo la mtoto wa umri huo halina uwezo wa kumengenya na kunyonya madini muhimu nje na maziwa ya mama,kwahio hatapata faida kutoka kwenye vyakula unavyompa,zaidi utamletea matatizo ya tumbo kama infections na kudumaa ukuaji
Pia kwakua maziwa ya mama asilimia kubwa ni maji,haitaji maji ya ziada pia.
 
Amen. Uzi ufungwe

Cc Smart911
 
Back
Top Bottom