Nilizoe kusoma mikasa ya mapenzi,kwenye simulizi za magazetini,vijarida na vitabu.siku moja nikiwa mkoa fulani ,niliamua kumtafuta rafiki yangu ambaye tulipotezana kwa muda kidogo baada ya kumaliza chuo.Nilipompigia simu alifurahi sana na akanihimiza nifike haraka sana nyumbani kwake.siku hiyo nilikua niko na jamaa yangu mwingine.Basi tulipofika nyumbani kwake nikamkuta yuko na jamaa mwingine, wote walikua wanyuka suti maridhawa.Lakini hali ilibadilika ghafla, siyo kama vile tulivyoongea kwenye simu,kwani yule jamaa mwingine alikua mnyonge sana.Ndipo ikabidi niulize kulikoni?
Mwenyeji wangu akafunguka kuwa muda ule walikua wametoka kanisani, na yeye akiwa Bestman lakini Bibi harusi alikua Kala kona.walijitahidi kumtafuta bila mafanikio."Nilipigwa butwaa kwani nilizoea hadithi kumbe huwa inakua kweli"Basi kama kawaida ikabidi tuanze na kufarijiana na busara za uongo na ukweli zilitawala.Yule jamaa alikuwa ni mwl na mwezi huo ilikua aende UDSM kujiongezea shule,lakini kutokana na pilikapilika za ndoa, na maisha mapya aliamua kuahirisha shule yake hiyo.Kitu nachokumbuka kumshauri,ni kwamba 1:Ajikubali kwamba imemtokea kwani ndio hatua moja wapo ya kuanza upya maisha.2:Ilikuwa imebaki wiki moja chuo kufunguliwa-hivyo nilimshauri ajaribu kuwasiliana na uongozi wa chuo kama wangemruhusu aendelee na chuo,kuliko kuendelea kukaa pale mkoani.
Nilipiga zangu castle zangu, na baadae nikaaga.Kwa jinsi tulivyoongea na yule Bwana,akapenda tuondoke wote kwani na yeye alitaka kurudi nyumbani.basi tuliondoka wote,kufika sehemu tukaona kijiwe, ikabidi niombe tupige mbili tatu,na ikawa hivyo.nilifanya hivyo ili kuwa na uhakika kuwa yule bwana akitoka pale,asiende kujitundika,kwani ningehuzunika sana kwa kutomsaidia.Tuliendelea na maongezi mpaka nilipoona ile hali yake ya huzuni iliyopitiliza imemtoka.
Ndipo tuliagana na huku akitushukuru sana,kwani alisema alikua kachanganyikiwa sana,lakini kwa wakati ule atleast alipata mwanga wa wapi pa kuanzia maisha yake mapya.
Baada ya siku mbili tatu tukapata taarifa yule Bibi harusi alitoroshwa na mpenzi wake wa siku nyingi ambaye aliokuwa amewasili toka SA.Hakuonekana pale mkoani kwa muda wa miezi yapata mitatu.Then kuna siku,nikiwa na jamaa yangu mmoja, tulipishana na binti mmoja mtaani.jamaa yangu akaniuliza kama namfahamu nikamwambia hapa.Ndipo aliponifahamisha kuwa huyu ndio yule binti,aliyeingia mitini wakati wa harusi,nilimuangalia huku tukipishana,nikijaribu kumkariri ili siku nyingine asije akamkimbia mtu mwingine mbele ya macho yangu.
Baada ya miezi kadhaa ,aliyekuwa anapaswa kuwa Mpambe wa bibi harusi nikapata taarifa kuwa kapata ajali na kufariki.Nilisikitika sana kwani nilikua nikimfahamu yule biti,huku wakati tukio hili likiendelea sikua nimejua kuwa yeye ndie aliukua mpambe wa BIBI HRUSI wetu.
Na simulizi yangu ndio inaishia hapo.
Dingi swayo,nakuomba tu ufuatilie hizi simulizi na kujifunza kutoka kwa yaliyowatokea wengine.Ila usiombe ikakukuta wewe,siku hiyo naamini utavaa kaptula kichwani.Kwani inaweza kukukuta kwa stahili tofauti.Na pia ujue haya matukio hutokea pasipo kujarajia.