Nikapime DNA au nikubali tu yaishe?

Nikapime DNA au nikubali tu yaishe?

Enyi vijana wa kiume Acheni kudate na wasichana wapumbavu.

Ninyi ndio mna ongeza idadi ya watanzania wapumbavu nchini.
 
Sisi wanaume tunapitia tabu sana, hawa wanawake muda mwingine sijui huwa wanaigiza kuwa vichaa au ni vichaa kweli? Maana visa vyao muda mwngine vinaumiza sana.

Wanawake wengi huwa hawapimi uzito wa meneno yao kabla hajasema, yeye anachojali afanye hivyo ili akukomoe au apime upendo wako kwake.

Hapo yeye kukwambia kuwa huyo mtoto siyo wako ilihali upo nae hakujua ilikua ni hatari kiasi gani , maana hilo ni jambo linaloumiza moyo sana.

Ukishaona mwanamke anakuletea mapichapicha ni bora kukaa Nae mbali tu, ni ngumu kumsahau mtu uliemzoea lakini kwaajili ya kuepusha shari ni bora uvae roho ngumu na kujilazimisha kumsahau
 
Habari za maisha wakuu

Tulitengana akaondoka na mtoto akaenda kukaa kwa dada yake baadae alipata mtu mwingine akamuoa siku ya ndoa yake aliambiwa na dada yake mkubwa pamoja na mume wake huyo kua anipigie simu kwamba anaolewa na kama nikitaka kumsalimia mtoto nimpigie dada yake na sio yeye nikasema sawa hilo limeisha lakini jambo la kusikitisha ni kwamba hiyo ndoa yao ilidumu kwa muda wa miezi mitatu mke akaachwa tena kwa tabia zake hizo za kutoka nje ya ndoa na hata vitu vya ndani alivyoondoka navyo kutoka hapa kwangu kwa ajili akatumie yeye na mtoto kaviacha kwa huyo mwanaume mpaka leo.

Alirudi tena kwa dada yake round hii life lili mgonga sababu alikua hana shughuli yoyote ya kumuingizia kipato zaidi ya sehemu zake za siri kuna siku nilimipigia simu dada yake ili nijue maendeleo ya mtoto dada yake nae asivyo kua na haya mzaramo yule ananiambia eti mrudie mwenzio mlee mtoto nilikataa katakata siwezi rudia matapishi baada ya siku kadhaa dada yake akanipigia simu shemeji njoo umchukue mwanao anaumwa maana mama yake simuelewi hajali kuhusu mwanae.

Bila kinyongo nikaenda kumchukua mtoto lakini siku hiyohoyo mida ya saa tano usiku nasikia mtu ananiita dirishani nauliza nani anajitambulisha anasema amesikia mtoto alikua anaumwa hivyo kaja kumuona nikashangaa ndio uje usiku nikamkatalia asiingie ndani na wala sikufungua mlango alisubiri hatimae akaondoka baada ya wiki moja dada yake anapiga simu anadai sasa hivi mama yake na huyu mtoto katulia hivyo nimrudishie mtoto nikagoma napia nikagundua kumbe lengo la kunipa mtoto lilikua ni mtego ili turudiane.

Huyo mwanamke kapambana kapata bwana mwingine tena kamuoa baada ya kuolewa kaanza kunitumia ujumbe kua nimrudishie mtoto kwa sababu sio damu yangu kwamba nakaaje na mtoto asie wangu na wakati baba yake yupo nikapotezea nikasema hili chizi nini nilipokuja kugundua kua hili jambo liko serious kaenda kawaambia mpaka ndugu zangu kua yule mtoto sio wake ana baba yake mzani sio yeye mwambieni asikae na mali za wenyewe basi bwana bila kinyongo nikamwambia njoo umchukue mwanao bwana nitazaa mwingine kwani mimi bado ni kijana.

Jana ndio kaniacha mdomo wazi kanipigia simu ananiambia eti mtoto kafika umri wa kuanza shule tuma hela nimuandae mapema kabla hajachelewa nimemuuliza baba yake mzazi yuko wapi kaanza kujichekesha kama jinga vile.
Wewe na yeye akili zenu kama za DPW
 
Wanawake wengi huwa hawapimi uzito wa meneno yao kabla hajasema, yeye anachojali afanye hivyo ili akukomoe au apime upendo wako kwake.
Wanwafanyie wanaume mazwazwa wasiojielewa.

Ndio maana mwanamke anaolewa na wewe anapigwa nje na bado anakwambia mrudiane.

Ukiona hivyo ujue kashakuona wewe ni Poyoyo.
 
Mkuu, mi nakushauri kama una uwezo nenda kapime DNA,
Ili kama mtoto ni wako mtunze mpe elimu fresh kama sio wako mkabidhi kwa mama yake jitoe mazima,

Usifanye maamuzi bila vipimo vya DNA, unaweza tupa damu yako kizembe sanaaaa
 
Wanwafanyie wanaume mazwazwa wasiojielewa.

Ndio maana mwanamke anaolewa na wewe anapigwa nje na bado anakwambia mrudiane.

Ukiona hivyo ujue kashakuona wewe ni Poyoyo.
Kabisa mwanamke akishakuonyesha kuwa anahitaji akupunguze kwenye maisha yake na anabwana mwingine hutakiwi kurudi hapo tena maisha yako yote laa sivyo jiandae kudharauliwa
 
Kabisa mwanamke akishakuonyesha kuwa anahitaji akupunguze kwenye maisha yake na anabwana mwingine hutakiwi kurudi hapo tena maisha yako yote laa sivyo jiandae kudharauliwa
Kabisa hadi dada mtu naye anamchezea akili hivyo.
 
Kama utani ila ndio kakuambia ukweli tayari.

Kapimeni DNA Mkuu, sio gharama ni Tsh. 100,000 kwa kila sampuli ambapo itachukuliwa ya kwako, ya mtoto na ya mama wa mtoto jumla 300,000/=

Hapo utaweka gharama za Wakili atakayeshughulikia maombi ya vipimo vya DNA hapa inategemea.na wakili husika ila andaa isiyopungua 500,000/=

Kwa hiyo jumla inaweza ikafika 800,000/= hadi 1,200,000/= unapata majibu yenu mnaishi kwa amani kabisa.
 
Ttzo linakuja kwa uyo mtoto unaweza weka roho ngumu kwa mama je uyo mtoto utafanyaje

Unaweza sema mkapime DNA je kwa wakati huu ambao bado unajishauri uyo mtoto yuko ktk hali gan

Lakin pia chako ni chako tu ata kwa macho unaona sio lazma DNA japo kua DNA itakupa majb sahihi yanakwel ila ata bila dna mtoto wako utamjua tuu

Cha msingi leo mtoto wako wakat ukiendelea kutafta njia sahihi ya nn chakufanya
Mwanamke anaweza kukwambia maneno mabaya akiwa na nia ya kukuumiza kiakili na kifikla na unavyojua wanawake weng akili zao huwa aziwazi sawa pale wanapokua na hasira

Inawezekana kbsa ayo maneno kayasema kwa hasira au akiwa na nia ya kukuumiza moyo ila baada ya kuona ww umetulia bas akili imemrudi na anajutia ndo maana ad kakuomba pesa ya ada ya mtt

Angalia mwanao kwa sasa mengne badae
 
Kama una mashaka kabisa kapime DNA. Ila kama mtoto kafanana na wewe achana naye ni mtoto wako huyo.
 
Kwa tabia ya huyo mwanamke haina haja ya kwenda kupima.
 
Back
Top Bottom