Nikianza kumtongoza mwanamke kabla hajakubali nakuwa na shauku naye akikubali tu napoteza hamu naye

Nikianza kumtongoza mwanamke kabla hajakubali nakuwa na shauku naye akikubali tu napoteza hamu naye

Kaluluma

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
468
Reaction score
619
Habari zenu wakuu,kijana wenu naomba ushauri katika hili
iko hivi;

Mwanzoni wakati naanza mambo ya mahusiano nilikuwa vizuri tu na watu niliokuwa nao katika mahusiano nikimaanisha upande wa kuwasiliana na mambo mengine madogomadogo hali iliyofanya nifurahie sana kuwa kwenye mahusiano.

Shida imekuja kuanza miezi kama kumi iliyopita
,yaani nikimtongoza mwanamke kabla hajanikubalia nakuwa namsumbua sana calls za mara kwa mara kumjulia hali,kuonana mara kadhaa ila anaponikubalia tu yaani napoteza kabisa mzuka nae hata kama bado sijasex nae.
Yaani naweza maliza hata wiki sijamuona wala kumjulia hali wala kuwasiliana nae halafu naona sawa tu,

jambo linalopelekea kuachwa na wanawake ambao nakuwa nimeanzisha nao mahusiano,maana wengi wanalalamika siwafai maana sina muda nao kabisa.Japokuwa huduma zao nawazingatia. kiasi kwamba kuna mmoja aliwahi kuniambia haya
nanukuu
"wewe kaluluma hunifai kabisa yaani mwanaume unapitisha siku mbili hujanijulia hata hali kama naumwa au nimekufa je?,bora uendelee tu na mambo yako"
tukawa tumeachana kihivyo
nimejitahidi sana kubadilika lakini nimeshindwa.

Baada ya kuwa na wanawake kadhaa na mambo kuwa vilevile nikaona kabisa labda huenda mahusiano sio fungu langu nikatafuta kitu kingine ili niwe addictive nacho

Nikaangukia kwenye playstation games lakini upweke bado ukawa tatizo kubwa kwangu nikaikosa ile faraja niliyoihitaji.

Nikaona isiwe kesi nikatafuta njia ya kupunguza masaa ya kuwa active kwenye real world ,
hapo ndio nikadumbukia kwenye ulevi wa pombe kali (hasa konyagi,k vant na spirit nyinginezo)

Ikawa kila nikiamka naamkia mizinga ya konyagi nakunywa mpaka nazima ila nikishtuka bado nahisi kuna kitu nakosa maishani.

Kwenye ulevi huu nilifika pabaya mpaka nikaanza kuvuta bandadu(wale wanaotumia vilevi mbalimbali wanaijua hii kitu).

Nikiri wazi tu kwamba,huu ulevi ulipelekea kuzorota mpaka shughuli zangu za utafutaji mkate.

Maana ilikuwa naamka na pombe kali mpaka nazima halafu nikiamka najiongezea dozi tu ili nisiwe active.

Marafiki zangu wamenishauri sana mpaka kufikia hatua ya kunitafutia mwanamke huenda nikawa sawa lakini sioni hata umuhimu wa huyo mwanamke.

Naomba yeyote mwenye ushauri au aliyewahi kupitia hali kama hii aninasue katika hili,

Maana naona dalili mbaya mbele yangu nisije kushindwa anzisha familia huko mbeleni maana naanza kuhisi kama sihitaji kuwa na familia ilihali mimi bado kijana mdogo tu.

Nisaidieni jamani,natanguliza shukrani.
 
Hiyo hali inasababishwa na kuumizwa sana na mtu uliyekuwa unampenda kwa hyo kila mwanamke kwako ww unaona atakuumiza pia hali inayopelekea kuwa hvyo
Mliachanaje na ex wako kabla ya kupata hawa ulionao sasa hivi.
 
Tuliachana vizuri tu,maana mi nilihama mkoa nikamuacha yeye mkoa mwingine.
 
Hiyo hali inasababishwa na kuumizwa sana na mtu uliyekuwa unampenda kwa hyo kila mwanamke kwako ww unaona atakuumiza pia hali inayopelekea kuwa hvyo
Mliachanaje na ex wako kabla ya kupata hawa ulionao sasa hivi.
Point....mimi nipo kama huyo mselaa....yaan nikishapiga napita iv...hata hapa kuna manzi niko nae naona kaninunia kumbe hajasoma mchezo kwamba akiondoka ndo imeisha ivo....anaona kama ananikomoa kumbe anapiga chura teke
 
vp mkuu hujafikiria kujikomboa kwenye hiyo ishu,maana mi naona ninakoelekea hali inaweza kuwa si shwari.
 
Back
Top Bottom