Nikikubali mtaniona 'dhaifu' ila nikikataa 'nitaumbuka' zaidi lakini 'nikinyamaza' naweza 'Kunyimwa' zaidi. Je, lipi jema?

EU hawataki mchezo safari hii, rudisheni pesa za watu.

Huu upuuzi wenu wa kupokea maburungutu ya hela za mabeberu halafu kumbe mnafahamu 'ugonjwa' haupo kwa miujiza ya Jiwe, unali'cost taifa zima . !
Ni vyema kama 'Uzi' ukiwa umenzishwa 'Kimafumbo' hivi basi nawe pia utiririke na userereke nao 'Kimafumbo' hivyo hivyo ili kutoharibu 'rhythm' nzima. au unadhani ni Wewe tu pekee ndiyo umeweza 'Kukielewa' nilichokikusudia na kukilenga hapa na kwamba hawa 'Members' wengine wote waliokutangulia 'Kukomenti' wao hawajanielewa? Umenikera mno na unaonekana una 'Kiherehere' Waganda wanasema una 'Lugezigezi' sana tu.
 
Nimehongea tena Wake za Watu Arusha, Kisarawe Pwani, Tanga na wengine Mwanza na Kagera huku zilizobaki nimeweka Lami kwetu huko Mara.

Duh! ,kama Matumizi yenyewe ndio hayo una Kazi Mwaka huu.Hautapata Raha hata hao Wake za Watu ulio wahonga hawatokupa Raha utazitapika Kaka,sisi kama Familia tuna kucheki tu utakavyo someshwa namba
 
Ni Aibu sana ,Mkuu kwani ulifikiri hapo ulipo ni mbaaaali sana kiasi ukahisi hawezi stuka kwa ulicho kifanya !?

Mbaya zaidi Familia ndio inapiga kelele baada ya wewe kuitumia vibaya Pesa ya Rafiki yako ,na umejitahidi weeh kuiziba Mdomo umeshindwa.
Ciril Mkuu nipe 'Maujanja' basi ili 'nimpoze' huyu 'Mzungu' kwani Akiba ( Hazina ) Kwangu 'Kumekauka' sasa na 'Familia' yangu 'itateteseka' baadae.
 
Hayo 'mafumbo'unamfumbia nani?

Hizo style za 'kidada' wengine hatuziwezi!
 
Nawewe umekuwa Jiwe unawapangia watu jinsi ya kucoment?
 
Ciril Mkuu nipe 'Maujanja' basi ili 'nimpoze' huyu 'Mzungu' kwani Akiba ( Hazina ) Kwangu 'Kumekauka' sasa na 'Familia' yangu 'itateteseka' baadae.

Mkuu GENTAMYCINE hauna namna labda umuahidi Mikataba mizuri nyuma ya Pazia ,kuhusu lile Shamba lako la kule Kusini au vinginevyo sivyo utaumbuka.Hata hivyo atakupa masharti mengi sana ili akukaushie kwa soo lako Mkuu.
 
Hahaha wanasema tumekula wote na sio peke yao.πŸ˜†πŸ˜†
Ila nadhani Mimi ndiyo 'nimeila' zaidi kwani hapa juzi tu nilikuwa na 'Sherehe' Kubwa ambayo ilinifanya pia niweze 'Kuwanunua' Wageni wa mbali huku wengine 'nikiwaahidi' kuwa wakihudhuria tu basi nitawapa 'Zawadi' na wale niliowapa 'dhamana' ya kuhakikisha 'Sherehe' yangu 'inafana' sana nao pia niwapa sehemu ya huo 'Mgao' ambao Mimi niliuomba nikawatibie Wanafamilia wangu kwa Ugonjwa wa 'KOROMA' sana.
 

Duu,πŸ™„ kwa kweli Soo lako sio la kitoto na sidhani kama yupo wa kukutoa ktk hili sababu Kitanzi umejiweka mwenyewe tena cha Chuma steel kabisa.
 
Nawewe umekuwa Jiwe unawapangia watu jinsi ya kucoment?
Hao wengine waliousoma na Kuuelewa huu 'Uzi' na 'Uwasilishaji' wake wa 'Kimafumbo' na Wao wanachangia 'Kimafumbo' unadhani ni 'Majuha' kama Wewe na huyo 'Mpuuzi' mwenzako hapo juu? Kwahiyo Wewe na huyo 'Mpuuzi' mwenzako ndiyo mnajianya Kuelewa sana hivyo 'mmewashwawashwa' huko 'Kunako' Kwenu na kuja na 'Viherehere' hivi cha 'Kukomenti' kiuwazi zaidi? Mnakera na sijawaiteni katika huu 'Uzi' sawa?
 
Popoma genius,umefunga inbox? najaribu kukucheki
 
Sio kama nna mtetea ile Hukumu ya Max kuhusu Jamiiforums pengine ndio ina pelekea kuletewa tungo tata kuwakwepa hawa walio shika mpini Mkuu.
Mpumbavu huyo hawezi Kukuelewa na wapo wengi tu kama Yeye ambao wanadhani kuja na aina hii ya 'Uwasilishaji' wa 'Mafumbo' nimekurupuka.
 
Hyo mzungu achana nae asikupandishe kisukari kweli hela alikupa ukatibie ugonjwa hospitali,ila kwa bahati nzuri ukatibia mizizi na maombi, sasa shda iko wapi si umetumia kwa matumizi mengine,hata ningekuwa mimi ndo "GENTAMYCINE " nsingeweza kurudisha hyo hela kwa rafiki yangu kama ni uaminifu ufe tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…