Iwapo nikibahatika kupewa nafasi ya kuonana na mh. Rais jk nitamshauri hv, mosi, avunje uongozi mzima wa helsb kwa sababu hauna tija nzuri kwa maendeleo ya elimu ya juu na unafanya kazi ya kubahatisha tena afadhari ya waganga wa kienyeji. Mf. Bodi hiyo inawapa kipaumbele watoto yatima lakini mbona wapo ambao ni yatima na wamekosa na wasiyo yatima wamepata mia? Wanasema wenye dip wanaweza kujisomesha kwa mshahara gani mfano waalim kila siku wanalia mshahara mdogo na tena wanawajua wategemezi wao? Na kwann hayo yote wasingeyaweka wazi ili sisi wenye dip tusiombe kabisa? Huu siyo ubabaishaji!? Pili, ningemuomba asimike uongozi mpya na tena aliye mwadirifu na ambae alisomea tanzania na kuishi tanzania na tena aliyesoma shule za akina kayumba ili ajue anaowahudumia ni watu wa aina gani? Tatu, ningemuomba atoe agizo kwa uongozi mpya kwamba uhakikishe kila aliyekosa mkopo analipiwa asilimia isiyopungua hamsini kwa kila mmoja ili wote twende chuo. Nnne, kwa ajili ya maboresho ya mwakani fomu za kuomba mkopo ziboreshwe kuwepo na maswali mengine ya ziada badala ya hz form za sasa zinalenga kujua uhai wa wazazi na ulemavu wa wazazi kwani siyo kila yatima hana uwezo wa kujisomesha hiyo siyo kweli kwani wapo wazazi wao walikuwa ni mawaziri wakurugenzi n .k hao huwezi ukasema et kwa sababu wamefariki basi kwa kutumia kigezo cha uyatima et uwape mkopo.au mzazi akiwa na ulemavu et iwe hoja ya kupewa mkopo ilihali wapo hadi wabunge waremavu.au kwa kuwa mimi ninadiploma et ninyimwe mkopo bila kujua mshahara niupokeao ni kiasi gani na ninawategemezi wangapi? Tano, pia ningeshauri aangarie uwezekano wa kustandalaizi huo mkopo yaani kila atakayeomba atalipiwa asilimia hamsinii ili kila mmoja awe anajipanga kuongezea hamsini kuliko kumrundikia mtu mmoja asilimia mia moja ili hali wengine wakikosa hata asilimia moja. Mwisho ningemwambia kwamba huku nyuma yako upo umati mkubwa sana ukikupigia magoti na kukulilia wewe na we neno lako moja waweza ukawaponya au ukawaangamiza na kuwazika ardhini milele hadi kiyama. Je ww ungemwambiaje?