Nikimaliza chuo nifanye nni?

i do other busines hovewer. kama utahitaji gum boot na vifaa vya usalama huko shamba, tent za kuweka kambi tuwasiliane
 
Wewe uliwaaminisha wazazi wako kuwa ukimaliza tu chuo ajira nje nje, ndo ukomae sasa kuwaaminisha.

Tafuta kazi za kujitolea huku ukitengeneza connection ili upate mchongo.
 
Ni aibu kwa mwanafunzi tena msomi ambaye ametumia zaidi ya miaka 15 akiwa shule na hujui ufanye nini baada ya kumaliza chuo.

Tukiwaita wazembe na wapumbavu mnasema tunawaonea OK ngoja nikushauri, kuanzia leo hii badiri mindset yako na uanze kuishi maisha as if huna mtegemezi unayemtegemea akusaidie na uishi kama wewe ndiye unategemewa yaani kiufupi ifanye akili yako izijue shida mapema na utambuwe kuwa Future yako inadepend na unachokifanya sasa hivi, kwa kulijua hili sidhani kama hutokipata cha kufanya, labda tu uiendekeze akili yako kutoshughulika.

Vya kufanya ni vingi kulingana na uwezo wako /wa familia yako kiuchumi kuweza kukubust mtaji.

Acha kusema unasubiri umalize chuo ndipo uanze kutafuta maisha, hapo utafail pakubwa, anza leo hii, muda huu.

Fikiri kama ungekuwa unadaiwa kiasi fulani cha pesa na umepewa week moja tu kukirudisha je ungefanya nini ili ukipate hicho kiasi?

Hizo njia utakazo tumia basi jaribu kuzitumia sasa ili ujuwe utaishi vipi, kama ni kuomba omba basi una hali mbaya sana, kama ni kuuza baazi ya mali zako basi tumia akili hii hii kuzibadiri mali zako kuwa pesa ichangamshe akili hiyo japo kwa vijibiashara uchwara na hakika utatoboa.
 
Usiweke mategemeo makubwa sana utakua disappointed,
nenda na kasi ya mziki.
Mwisho wa siku kila kitu kitaenda sawia.
 


Kwanza tengeneza CV/Resume. Pili tafuta sentensi ya kujielezea vizuri mmana hapa kwa unacho andika hatujui hata umesomea nini hasa wewe ni engineer, muuguzi au nani. Je ni diploma, degree au ni nini, Chuo gani umesoma, je ulifanya internship au hujafanya....... inabidi uwe na stori fupi ambayo unajielezea. Pili huwezi kuuliza watu wengine ufanye nini? sisi hatujakutuma kusoma course hiyo na huwezi kutuuliza wewe ufanye nini tena baada ya kumaliza chuo sisi tunaweza kukusaidia kwenda mbele lakini wewe ndiye unatakiwa kujua unataka nini kwanza
 

Hili la wazazi kuamini kutoboa baada ya masomo ni zuri lakini madhara yake ni makubwa sana kwa anayeaminiwa kwasababu ikitokea mambo yakaanza kwenda ndivyo sivyo muhusika anadata mapema sana

Kikubwa mkuu ukimaliza chuo take your time
Bado una muda mrefu wa kujipanga na ikitokea ukaona mambo ni magumu usichanganyikiwe sababu ya kufikiria wazazi na matumaini yao juu yako
 
Nakubalian n hoja hii mkuu, wazaz wasiwe kipaumbele. Hapo safar ya kwanza ni kujitegemea kwanza
 
Aaaah serious bro! Upo mwaka wa mwisho, chuo na hujui ufanye nini?kafsnye ulichosomea! Mantiki inataka hivyo!for starters! Ukikosa, ulichosomea, vipo vingi vya kufanya, music production, driving, kupiga picha, kuwa fleet manager kwenye makampuni!
Nilikutana na mwalimu anafunga solar system Zanzibar, anapiga kazi vibarua vya plumbing, kila eneo!
Jamaa yangu, ana degree yw sheria, lakini anafanya kazi ya kupiga picha na video!
Kuna mechanical engineer, anakampuni ya kutengneza video na picha za matukio na sherehe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…