Mimi ni mwanafunzi wa chuo, nipo mwaka wa mwisho. Hapa nilipo ninamawazo mengi kuhusu kipi ntafanya baada ya kumaliza chuo. Nasomea mambo ya Utaalamu wa Vifaa Tiba vya Hospitali. Wazazi wangu na ndugu zangu wana matumaini makubwa sana juu yangu hadi naogopa!!
Mwenye ushauri wwte naomba anisaidie jmn!!!. Kwasababu sahz hadi naogopa kurudi nyumban baada ya kumaliza chuo.
Kwanza toa mentality ya kwamba you have to prove yourself, pambana kwa kadri ya uwezo wako ila si kwa kuonyesha you need to prove yourself.
Kama hukuweza save chochote it’s okay ila kwa huu mwaka wa mwisho pambana upate saving kwa namna yoyote ile kutoka boom kama unalo au hata hela unayo tumiwa home. Hii itakusaidia utakapo hitaji kuanza kujisimamia ukimaliza chuo na si lazima huu ndo uwe mtaji wako wa kuanzisha biashara (si lazima ila unaweza kuwa)
Usirudi home moja kwa moja, tafuta pa kujishikiza mapema ukiwa una maliza mwakani unakua unajua wapi pa kuanzia, whether ni biasharani kwa watu, connections utakazo tengeneza au through industry uliyo somea
Apply kazi mbali mbali si lazima hizo ulizo somea, you never know wapi bahati yako ime lalia
Apply scholarship mbali mbali ukiwa unahangaika na kutafuta kazi, hii inaweza ikawa njia nyingine ya kujiendeleza
Make sure unakua at peace na nyumbani at all times kiasi kwamba pale unapo kwama hawawi wazito kukusaidia. Ile mentality ya kujitaka kuwa mkubwa na kuji isolate itaku cost ukiiweka mbele
Achana na peer pressure, ukiona wenzio wana progress endelea na mwendo wako. Mahusiano muhimu lakini si lazima ukiwa unajitafuta.
TAKE IT SLOW.