Nikinunua umeme kisha nikaingiza Token, inaandika "error 77 na Token haziingii

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
Tatizo ni kwamba, nikinunua umeme kisha nikaingiza Token, inaandika "error 77" na Token haziingii.

Kwa sasa ni zaidi ya wiki tatu naongea na watoa huduma wa ngazi mbalimbali wakiniahidi kuwa mafundi wa karibu watafika kutatua tatizo lakini hakuna kinachoendelea mpaka sasa.

Kila nikiwapigia simu wanachukua Namba ya mita na Namba ya simu lakini utekelezaji hakuna.

Shida ni nini? TANESCO
 
Tatizo ni kwamba, nikinunua umeme kisha nikaingiza Token, inaandika "error 77" na Token haziingii. Kwa sasa ni zaidi ya wiki tatu naongea na watoa huduma wa ngazi mbalimbali wakiniahidi kuwa mafundi wa karibu watafika kutatua tatizo lakini hakuna kinachoendelea mpaka sasa. Kila nikiwapigia simu wanachukua Namba ya mita na Namba ya simu lakini utekelezaji hakuna. Shida ni nini?
Wape elfu 20 uone kama hawakutumii code ya kuifungua meter dakika hiyo hiyo
 
Tatizo ni kwamba, nikinunua umeme kisha nikaingiza Token, inaandika "error 77" na Token haziingii.

Kwa sasa ni zaidi ya wiki tatu naongea na watoa huduma wa ngazi mbalimbali wakiniahidi kuwa mafundi wa karibu watafika kutatua tatizo lakini hakuna kinachoendelea mpaka sasa.

Kila nikiwapigia simu wanachukua Namba ya mita na Namba ya simu lakini utekelezaji hakuna.

Shida ni nini? TANESCO
Huenda kunajambo baya uliifanyia 77, 77 inalindwa na mwenge mnaoudharau, na ni huo mwenge ndio unaotutia ujinga watanzania tuwe tunainamisha vichwa chini kama kondoo, katubu haraka.
 
Wape elfu 20 uone kama hawakutumii code ya kuifungua meter dakika hiyo hiyo
Tatizo ni kwamba, nikinunua umeme kisha nikaingiza Token, inaandika "error 77" na Token haziingii.

Kwa sasa ni zaidi ya wiki tatu naongea na watoa huduma wa ngazi mbalimbali wakiniahidi kuwa mafundi wa karibu watafika kutatua tatizo lakini hakuna kinachoendelea mpaka sasa.

Kila nikiwapigia simu wanachukua Namba ya mita na Namba ya simu lakini utekelezaji hakuna.

Shida ni nini? TANESCO
Ingiza aina ya tatizo, jina na namba ya ya mita kwenye Google, utapata ufumbuzi.
 
Zima sockets zote bakisha moja, hakikisha remote yako ina battery.
Andika sifuri ikifuatiwa na namba ya mita rudia tena sifuri ikifuatiwa tena na namba ya mita halafu weka Ok ikiondoka mita itakuandikia GOOD. Kama kwako haiwaki hata ukiweka battery kwenye rimoti nenda nyumba jirani mnayetumia nguzo moja, fanya kama nilivyoeleza hapo juu. Nakutakia sikukuu njema
 
Tatizo ni kwamba, nikinunua umeme kisha nikaingiza Token, inaandika "error 77" na Token haziingii.

Kwa sasa ni zaidi ya wiki tatu naongea na watoa huduma wa ngazi mbalimbali wakiniahidi kuwa mafundi wa karibu watafika kutatua tatizo lakini hakuna kinachoendelea mpaka sasa.

Kila nikiwapigia simu wanachukua Namba ya mita na Namba ya simu lakini utekelezaji hakuna.

Shida ni nini? TANESCO
mimi sio fundi wala mfanyakazi wa Tanesco ila niandalie 15,000 nikishamaliza kazi yako nitumie kwenye namba yangu...

Njoo inbox nikufanyie kazi yako

malipo baada ya kazi..

mimi ni Graduate, kazi zangu ni za kubangaiza, usije ukanidhulumu mkuu😭😭
 
Halafu TANESCO, ondoeni basi ule utaratibu wenu wa kututaka kwenda nyumba za jirani kurejesha umeme iwapo tu units zitaisha zote. Mkumbuke kuna kujisahau!!

Sasa inakuwaje umeme umekata ndani ya nyumba yangu, nimenunua units!! Eti ili umeme urudi, natakiwa kwenda kutumia mita ya jirani!! Hivi ni kwa nini msiweke utaratibu wa kurejesha hiyo huduma huku wateja wenu wakiwa majumbani kwao? Kuna ulazima gani wa mimi kwenda kwa jirani? Na kwa nini mliweka utaratibu wa kidwanzi kama huu kupitia hizi mita zenu za LUKU? Kumbukeni zamani hakukuwepo na ujinga kama huu.

TANESCO, wakati fulani mjue mnatudhalilisha! Ondoeni hii kitu bhana.
 
Halafu hiyo ni kweli haimake sense.
Hao wasomi wao walioweka huo utaratibu wajitafakari.
Hivi chukulia kwa mfano mtu anaishi mahali kwenye bangalow lake lililojitenga peke yake mashambani na hakuna jirani karibu au majirani waliopo maeneo hayo nyumba zao hazina umeme atafanyaje?
Au chukulia kwa mfano mtu yuko na majirani lakini hawana story wala hawaelewani kwa hiyo inabidi mtu akalazimishe story na mtu ambaye hawana maelewano yoyote kwa sababu ya umeme
Halafu TANESCO, ondoeni basi ule utaratibu wenu wa kututaka kwenda nyumba za jirani kurejesha umeme iwapo tu units zitaisha zote. Mkumbuke kuna kujisahau!!

Sasa inakuwaje umeme umekata ndani ya nyumba yangu, nimenunua units!! Eti ili umeme urudi, natakiwa kwenda kutumia mita ya jirani!! Hivi ni kwa nini msiweke utaratibu wa kurejesha hiyo huduma huku wateja wenu wakiwa majumbani kwao? Kuna ulazima gani wa mimi kwenda kwa jirani? Na kwa nini mliweka utaratibu wa kidwanzi kama huu kupitia hizi mita zenu za LUKU? Kumbukeni zamani hakukuwepo na ujinga kama huu.

TANESCO, wakati fulani mjue mnatudhalilisha! Ondoeni hii kitu bhana.
 
Habari Tate Mkuu, asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole sana kwa changamoto hiyo, jinsi ya kuondoa ujumbe wa error 77 kwenye mita yako tafadhali nunua betri mpya kisha weka kwenye rimoti ya kujaza token na chomeka kwenye soketi ndani kwako hata kama unit zimeisha kisha bonyeza 0 namba ya mita 0 tena namba ya mita weka OK itakuandikia good/accept na utajaza token zako, Mfano 024213255672024213255672. Na kuhusu maoni uliyotupatia tumepokea kwa utekelezaji zaidi.^LS
 
Huu utaratibu uko nchi gàni? Ni kwa mita zipi? Mbona mimi umeme unit zikiisha naweka tuu bila kuhusisha jirani?
 
Habari Tate Mkuu, asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole sana kwa changamoto hiyo, jinsi ya kuondoa ujumbe wa error 77 kwenye mita yako tafadhali nunua betri mpya kisha weka kwenye rimoti ya kujaza token na chomeka kwenye soketi ndani kwako hata kama unit zimeisha kisha bonyeza 0 namba ya mita 0 tena namba ya mita weka OK itakuandikia good/accept na utajaza token zako, Mfano 024213255672024213255672. Na kuhusu maoni uliyotupatia tumepokea kwa utekelezaji zaidi.^LS
Ahsante. Ngoja nifanye hivyo.
 
Back
Top Bottom