Nikinunua umeme kisha nikaingiza Token, inaandika "error 77 na Token haziingii

Huu utaratibu uko nchi gΓ ni? Ni kwa mita zipi? Mbona mimi umeme unit zikiisha naweka tuu bila kuhusisha jirani?
Kwenye zile mita za kutumia rimoti umeme ukiisha ukataka kuweka umeme kwenye mita kuna option mbili za kuweka umeme.
1. Kuchomeka rimoti kwenye socket ya umeme na kuingiza token(njia hii ni kama umeme haujaisha kabisa kwenye nyumba yako)
2. Kuweka betri kwenye rimoti ya mita na kuweka umeme. (Njia hii unatumia iwe umeme umeisha kabisa au bado upo)
Sasa watu wengi hii njia ya kutumia betri hawaizingatii sana maana TANESCO wanashauri betri zitumike pindi tu unapoweka umeme zisikae kwenye rimote zinaweza kuvuja na kuharibu rimoti. Kwa hiyo kuondoa huo usumbufu mtu anaona bora tu atumie njia ya kuweka rimoti kwenye socket ili kuingiza token.
Sasa tatizo linakuja umeme ukiisha kabisa huwezi kuingiza hadi uende kwa jirani umuombe uchomeke rimoti kwenye socket yake ili uingize token.
Ushauri wangu; kama umeme ukiisha kabisa tumia betri hata za rimoti ya TV unazitoa unaziweka kwenye rimoti ya umeme halafu ukishaingiza token unazirudisha zilipotoka kuliko kwenda kumsumbua jirani.
 
Mkuu hizo mita za rimoti si zina option za kutumia betri? Kwanini usitumie hiyo option kuliko kwenda kwa jirani. Tena kwa vile ni tendo la mara moja unatoa betri kwenye rimoti ya TV unaziweka kwenye rimoti ya mita ya LUKU unaweka Token zikiingia unazirudisha kwenye rimoti ya TV. Au option nyingine usisubiri umeme uishe kabisa. Huo ndio ushauri wangu .
 
Solution ni powerbank tu hapo sijawahi kupata shida kuingiza umeme
 
Tanesco wanasemaje?
 
Bonyeza zero then namba za Mita tena bonyeza zero ukifuatia namba za Mita afu malizia ok.itakubali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…