Nikiondoka sirudi tena Dar

Nikiondoka sirudi tena Dar

Ndugu zangu kilichonikuta Leo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]!!!!!
Nilikuja Dar ijumaa.(siishi dar huwa nakuja matembezi)
Kumbe mji una wenyewe!!!
Leo si nikatoka nataka kwenda kutembea tembea,[emoji16]
Nikaambiwa nichukue pikipiki nikawa bahili[emoji19][emoji19].
Nikapita mitaani huko. Nikaingia kibanda cha Tigo pesa nikatoa hela.
Ile naondoka ghafla kuna watu wa 3 wananifuata nyuma, halafu kuna uchochoro ,[emoji52]
Moyo ukaanza kudunda, nikiongeza mwendo na hao wanaongeza.
Nikaona wapita njia nikasema bora nimepona[emoji119] .nikaanza kutembea kawaida .
Wale watu walinikuta wakanizuia na wale wapita njia wakawa wameshapita.[emoji17][emoji17]
Kuwaangalia wana kisu na sijui ni misumari ile.!!!
Nikasikia TULIA halafu na tusi juu. Nikasimama, wakaniambia kwa usalama nitoe kila kitu niwape niondoke.[emoji15][emoji15][emoji15](ni saa ,10 jioni) nikawaambia nawaitia mwizi[emoji28].
Wakaniambia nisijisumbue ule mtaa ni wao na wao ni maraisi hamna wa kuwatishia daah!!!
Mara watu wanapita nikaanza kusema "nyie niachieni kwa nini mnaniibia" nikijua wapita njia watanisaidia . khaa wanashangaa wanapita tuu.
Nikifikiria kasimu werevaa kangu hakana hata miezi mi 2.
Nikawa mwekundu ghafla ndani ya dakika 2 nimelia machozi hadi make up imeisha. Nikaanza kuomba msamaha "kaka zangu nisameheni mama yangu anaumwa yupo hospital ndiyo nimekuja kumuuguza"[emoji53][emoji53]
Akaja mmoja nahisi ni mwenzao akawaambia mwacheni huyo akaniambia nifuatee, nikasema Mungu wangu ndiyo nimfuate wapi tena hapo ndipo nilipojikojolea (sio utani)
Hiyo ikawa pona yangu akaniambia nimpe namba zangu atanitafuta na niwe makini.
Nikaondoka nikarudi nyumbani ( nilipofikia) nikaingia ndani nikafunga milango na madirisha yote na nimeshusha mapazia ,
Nikalala nikajifunika hadi usoni nahisi watakuja.
Nilijawa hofu sana.
Khaaaaa pakuche tuu niondoke [emoji17][emoji17][emoji17][emoji17].
MTU UNAVAMIWA NA VISU WATU WANAANGALIA TUU.
Kweli nilizaliwa mwenyew nitakufa mwenyewe.
Nyie KAKA JAMBAZI kama mpo huku nawaambia SIWAOGOPI[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]. Na nimewablock[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]
[emoji115]Dada yangu ndo maana huwa tunawaponda wannaume wa Dar wala huwa hatuwaonei!!.....ni waoga sana!!
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
jaman nimechekaaaaahahaha wewe dogo hujawah ambiwa unakipaji cha kuchekesha ?/hahaha yaan nacheka jaman kha sijui ni ie tu nnakuonaga km katuni aisee hahaha!pole
Ha ha ha[emoji53][emoji53][emoji53]( nacheka kwa kujilazimisha)
Usinicheke bana yaani hapa naogopa hata kwenda uwani
 
Hopefully Hukujiunga Jf On The 9Th Of August To Post This.

Sent using Jamii Forums mobile app
d911bf30a5faa555ee3331cd61547642.jpg
 
Back
Top Bottom