Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji115]Dada yangu ndo maana huwa tunawaponda wannaume wa Dar wala huwa hatuwaonei!!.....ni waoga sana!!Ndugu zangu kilichonikuta Leo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]!!!!!
Nilikuja Dar ijumaa.(siishi dar huwa nakuja matembezi)
Kumbe mji una wenyewe!!!
Leo si nikatoka nataka kwenda kutembea tembea,[emoji16]
Nikaambiwa nichukue pikipiki nikawa bahili[emoji19][emoji19].
Nikapita mitaani huko. Nikaingia kibanda cha Tigo pesa nikatoa hela.
Ile naondoka ghafla kuna watu wa 3 wananifuata nyuma, halafu kuna uchochoro ,[emoji52]
Moyo ukaanza kudunda, nikiongeza mwendo na hao wanaongeza.
Nikaona wapita njia nikasema bora nimepona[emoji119] .nikaanza kutembea kawaida .
Wale watu walinikuta wakanizuia na wale wapita njia wakawa wameshapita.[emoji17][emoji17]
Kuwaangalia wana kisu na sijui ni misumari ile.!!!
Nikasikia TULIA halafu na tusi juu. Nikasimama, wakaniambia kwa usalama nitoe kila kitu niwape niondoke.[emoji15][emoji15][emoji15](ni saa ,10 jioni) nikawaambia nawaitia mwizi[emoji28].
Wakaniambia nisijisumbue ule mtaa ni wao na wao ni maraisi hamna wa kuwatishia daah!!!
Mara watu wanapita nikaanza kusema "nyie niachieni kwa nini mnaniibia" nikijua wapita njia watanisaidia . khaa wanashangaa wanapita tuu.
Nikifikiria kasimu werevaa kangu hakana hata miezi mi 2.
Nikawa mwekundu ghafla ndani ya dakika 2 nimelia machozi hadi make up imeisha. Nikaanza kuomba msamaha "kaka zangu nisameheni mama yangu anaumwa yupo hospital ndiyo nimekuja kumuuguza"[emoji53][emoji53]
Akaja mmoja nahisi ni mwenzao akawaambia mwacheni huyo akaniambia nifuatee, nikasema Mungu wangu ndiyo nimfuate wapi tena hapo ndipo nilipojikojolea (sio utani)
Hiyo ikawa pona yangu akaniambia nimpe namba zangu atanitafuta na niwe makini.
Nikaondoka nikarudi nyumbani ( nilipofikia) nikaingia ndani nikafunga milango na madirisha yote na nimeshusha mapazia ,
Nikalala nikajifunika hadi usoni nahisi watakuja.
Nilijawa hofu sana.
Khaaaaa pakuche tuu niondoke [emoji17][emoji17][emoji17][emoji17].
MTU UNAVAMIWA NA VISU WATU WANAANGALIA TUU.
Kweli nilizaliwa mwenyew nitakufa mwenyewe.
Nyie KAKA JAMBAZI kama mpo huku nawaambia SIWAOGOPI[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]. Na nimewablock[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]
Ha ha ha[emoji53][emoji53][emoji53]( nacheka kwa kujilazimisha)jaman nimechekaaaaahahaha wewe dogo hujawah ambiwa unakipaji cha kuchekesha ?/hahaha yaan nacheka jaman kha sijui ni ie tu nnakuonaga km katuni aisee hahaha!pole
Ha ha ha[emoji53][emoji53][emoji53]( nacheka kwa kujilazimisha)
Usinicheke bana yaani hapa naogopa hata kwenda uwani
Huku jijini huwa kila mtu anapambana na hali yake usishangae mama wanaume wa dar kukupita ndo tunavyoishi. Pole ndo uwe makini. maana unaweza kuja hata msibani.usiseme hutokaa ujeSirudi tena.[emoji41][emoji41][emoji41]
Asante sana, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]watanijua eti kama kuna member alipita.pole sana kwa yaliyokukuta lkn ungetaja mtaa ili vijana wa siro wautembelee mtaa huo maana ni aibu kubwa
Sent using Jamii Forums mobile app