safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Mtu akikamata vijisenti utaona anajenga msikiti/kanisa kuuuubwaaa kwao.
Jiji la dar lina nyumba za ibada (kanisa/msikiti)karibia kila kona na watu hawajai, ila jiji la dar hospitali zinajaa sana, foleni za maji zinajaa sana, shule zinajaa sana.
Mtu anajenga nyumba ya ibada kijijini kisha wanakuja kusali watu watano tu,wakati huo kijiji hiko hiko kwenye huduma za afya au shule kuna watu kibao.
Nikipata pesa sitojenga nyumba ya ibada kwanza kwa sababu hiyo iliyokuepo haijai na kama kujaa kwa siku moja moja.
Nitajenga shule kwa sababu zilizokuepo zinajaa wanafunzi hawatoshi.
Nitajenga zahanati kwa sababu zilizokuepo zinajaa wagonjwa hawapati matibabu bora.
Nitanunua vitanda kwa sababu vilivyokuepo havitoshi watu wanalala wawili wawili n.k
Nitanunua madawati kwa sababu wanafunzi wanakaa chini na kuchafuka huku wakiongeza gharama ya sabuni.
Nikijenga msikiti/kanisa nitapata thawabu kwa wanaokuja kuabudu pekee na ni wachache hao wanaoabudu.
lakini nikijenga shule, kununua madawati, kununua vitanda hospitali, kujenga zahanati hapa nitapata thawabu hata kwa wasiokuwa wana ibada kwa sababu zahanai, vitanda, madawati hayachagui dini zote wanatumia.
Nikinunua misahafu watakaosoma ni waislamu wachache lakini nikichimba kisima watatumia wakristo, waislamu na hata wapagani na Mungu atanilipa kwa kila mtu anayetumia huduma hiyo.
Kwa mantiki hiyo kujenga nyumba za ibada na kujenga huduma zajamii zinazotumiwa na dini zote kwangu naona kujenga huduma za jamii ndio bora zaidi kwa sababu huduma hizo zitatumiwa na dini zote.
Sisemi ni vibaya kujenga nyumba a ibada lakini ni vizuri zaidi kuanzisha huduma za jamii ambazo wana jamii wanateseka nazo.
Nenda vijijini hakuna msikiti/kanisa linalojaa kwamba watu wengine wakawa wanasali nje hakuna.
Lakini angalia shule za vijijini na zahanati,na huduma za maji hizo foleni ndio utagundua ni wapi uweke kipaumbele.
Kwa sasa katika dini jambo la muhimu ni kuwahimiza watu washike dini na waijue na sio kujenga nyumba za ibada wakati watu wanakufa njaa na kiu na magonjwa mbali mbali.