Nikipata shida nasaidiwa sana na wanawake, hii inasababishwa na nini?

Nikipata shida nasaidiwa sana na wanawake, hii inasababishwa na nini?

Bravoozi3

Member
Joined
Dec 12, 2024
Posts
16
Reaction score
40
Mimi ikitokea nimepata tatizo napata msaada na support kubwa sana kutoka kwa wanawake. Hata kipindi nasoma wasichana walipenda kushirikiana na mimi katika discussions na walinisaidia materials ili nifaulu, na endapo nilifeli walijikusanya hata wasichana watano kunipa ushauri.

Sasa ni mtu mzima hali hiyo imeendelea, mfano: juzi nilikuwa nina shida na 500k akatokea binti akanisaidia 300k mwingine akanisaidia 200k, Pia kuna kipindi tulienda watu 12 kuomba kazi katika kiwanda xxx, boss akasema nafasi za kazi zimeisha, tukaondoka ila kuna mdada aliniita akaniomba namba yangu nikampatia, kesho yake kanipigia kanambia "kaka njoo uanze kazi".. Nikashangaa kwanini mimi tu katika watu 12! visa ni vingi mno hivyo ni baadhi tu.

Hii hali inanishangaza sana, nahitaji maoni yenu hii hali inasababishwa na nini?
 
Mwanamke ndiye kaumbwa kuwa msaidizi wa mwanaume.
 
cup-of-tea-teapot.gif
 
Back
Top Bottom