Nikipata utajiri nitakuwa katili sitakuwa na huruma

Kuna clip ya mkuu wa kaya na washikaji zake, anawaambia yeye akiwa mkuu wa kaya watu watalimia meno. Kwa bahati mbaya akawa kweli mkuu wa kaya na sasa watu wanalimia meno kweli kweli.

Kwa bahati mbaya kijana maono yako yatatimia na tutakukoma. Au wewe ndiyo Jiwe mwenyewe unatucheza shere hapa yaani sote wajinga na hatujitahidi.
 
Kwq roho hiyo baki nayo, hutatajirika ng'o!
Kwani pesa haijui kwa kwenda?
 
Mkuu kwa nini usisign contract na shetani maana utajiri mbona jamaa anautoa kwa masharti rahisi tu ya kuonesha upendo wako kwake
 
Mimi nadhani mleta mada kaamua kuwananga matajiri wa sasa namna wanavyobehave kwenye jamii zetu. Kuna watu huko mtaani wananyanyasa wengine mno.

Unakutana na watu huko wakisimulia manyanyaso ya matajiri mpaka inashangaza.

Mhudumu mmoja aliwahi nisimulia namna regular customer wao anavyowatukana anakuambia jamaa akiona wanachelewa kuleta oda yake anaanza kuwaambia wakakague usafiri aliokuja nao na kwamba umaskini wao ndio umewafanya wamhudumie yeye, you can imagine huyo mhudumu atakuwa na mawazo gani.
 
If wishes were Horses......Beggars would ride it,

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu tutakuloga
 
Hizo ndo uliota usiku wa Jana au juzi alafu ukaamka huna ata Mia hizo ndoto zakuokota pasa majumba kwenda ulaya kwa ndege binafsi yako alafu una amka zilikuwa ndoto hahaaaa ndoto raha Sana
 
Utakufa maskini pole sana kijana!
 
Mkuu mufti Simba pole sana, mbona unaitesa nafsi yako? kwani mkuu unataraji kubadilisha nini katika ulimwengu huu zaidi ya wewe kudhalilika na kuishia mavumbini na walobaki wakakusahau na historia yako ilojaa ujivuni kibri na dharau pia kufutika.
Ni lazima tutambue aliyetuumba katuumba na akatuweka madaraja tofauti kwa makusudi yake, basi usiwe na ghadhab jitahidi kuwa msamehevu na fanya jitihada ya kutafuta mali kwa njia za halali huku ukimuomba mola wako akupe mali na akuongoze katika njia bora ya kuitumia mali hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…