Nina mchepuko wangu ambao ninausimamia kwa 100% katika kila kitu
Huu mchepuko unanipenda kwa ninavyouona,pia nishauchunguza sana hauchepuki labda kama unafanya kwa siri sana
Tatizo lake haridhiki,anaomba helq kila sekunde hata umpe kiasi gani bado kesho atakuja akuombe
Unaweza mpa pesa nyingi tu ila kesho akarudi kutaka nyingine
Mpaka najiuliza hivi huyu hajui kuwa tuko kipindi cha bwana jpm??
Kilichonikera ni lastweek nimetoka kumlipia kodi yake kwenye nyumba anayokaa pesa nyingi vi mil kadhaa
Sasa cha ajabu jana nimeenda kupumzika kwake nikiwa naumw kweli na anaona hilo ila asubuh alipomka bila kujali naumwa na nimetoka kumlipia kodi juzijuzi tu eti akaniambia anaomba nimnunulie Iphone 7!!!!
Nilimwangalia na kukubali kishingo upnde ila nimepanga nikipona naenda kwa mwenye nyumba na kumweleza nafunga ile nyumba maana mimi ndo mpangaji na sio yeye
Na kwa sababu kila kitu kilichopo ndani ya ile nyumba nimenunua mimi nimepanga nimtolee nguo zake zikiwa kwenye begi na kuziweka nje kisha nibadili vitasa na funguo za milango yote
Akija atakuta vitu nje na mimi ntakuwa nishabadili line zangu kwa siku mbili tatu
Baada ya hapo ntatulia kdg kama wiki au mwezi kisha niibuke vyuoni nione kama ntapata mchepuko mpya uliokosa mkopo unitunze
Nb: nakuwa na mchepuko kwa sababu hatuko katik mahusiano mazuri na wife na isitoshe yuko mkoani
Je niko sahihi?