Nikisafiri kwenda sehemu sipendi kufikia kwa Mtu

Tatizo wengi wenu mmepanga,hivyo mnaogopa ndugu yako au rafiki akifikia kwako itakuwaje!.

Ukiwa na nyumba kubwa mbona fresh tu,mgeni anakuja kwako inabidi na wewe ubadirike,kinachofanya wengi muwachukie wageni ni UCHOYO & UBINAFSI!
Huo ni ukweli mkubwa sana.

Enzi zangu wakati nimepanga Room Moja na Mke wangu hatukuwahi kuruhusu hata Rafiki wa kututembelea sababu tunaona aibu.

Ila wakituone maofsini na kwenye majukwaa ya kisiasa tulikuwa watu wa maana sana.

Kumbe hamna kitu
😂😂😂

Kwa sasa nakaribisha ndugu yeyote hata awe Mtoto wa Mjomba wa Sahangazi na Bibi yake.
 
Nilikuwa na tabia ya kukaribisha wageni, nilikuja kugundua ni jambo lisilokuwa na faida yoyote. Sasa hivi ninapokea ndugu wa karibu tu.
 
Mwenyewe automatically nimejikuta hivyo.
Hasa mjini labda nikienda village.

Sababu ni ratiba. Sipendi kibadili ratiba zangu kisa mtu mwingine. Muda wa kuongea na watu wangu wa karibu, napenda kusoma sana na sipendi kelele. Siangalii TV, aina ya vyakula ninavyotaka vitawapa shida, napenda kuandika, Napenda maombi ya Muda mrefu, napenda kusikiliza Hymnals.
Yote hayo mara nyingi kila ninapoenda naonekana wa ajabu
 
Niliwahi kwenda mkoa fulani nikamtaarifu ndugu yangu kuwa nitakuwa huo.....akanisihi sana nifikie kwake....nikaona haina shida......aisee nilijuta ule uamuzi........

Nilikuwa najiweza hata kukaa hotel lakini nikasema nisimkwaze ndugu yangu.....

Nafika pale mapema kidogo tunapiga Stori za hapa na pale muda wa kulala napelekwa chumba cha watoto na humo kuna watoto kama wanne na wawili natakiwa kulala nao......

Vyakula sasa ndio adhabu......nilikuwa kila asubuhi nikienda kwenye mambo yangu namuachia jamaa kiasi cha pesa ili aongezee kwenye bajeti yao ili tufurahie maisha..... lakini matokeo yake mkewe anatulisha vitu vya ajabu......

Kila siku ugomvi na mkewe mimi ndio muamuzi....muda mwingine ugomvi ukizidi hakupikwi......

Nilikaa pale kama wiki hivi niliona kama nimekaa mwezi........

Kwa sifikirii tena kufikia kwa mtu nikisafiri.......
 
Kiukweli Mimi sipendi kufikia Kwa mtu yaani inafika muda unataka wenzako washafunga milango mapema sana

Jambo lingine kuharibiane bajeti ya msosi Tu weru unaamka asubuhi unaona machalii wanakula andazi 2 we mtu mzima umeletewa chapati na maziwa

Weraa Mimi nafikia gest Tu
 
Kufikia kwa watu keroooooo
Nikafikia kwa ndugu yangu, picha linaanza siku ya kwanza nyumba nzima wamefunga(fasting)namimi wanataka nifunge nikawakubalia kishingo upande.

Alfajiri ya saa kumi na moja naamshwa kwenye maombi, hamna kitu sipendi kama kuamshwa alfajiri, kulivopambazuka nikafua kashati kangu, mida ya tea tukagonga tea, ikaja kusoma bibilia tulivomaliza kusoma nikoga nikavaa shati langu nikabeba rasket yangu huyooo nikayeya.

Nilipanga kukaa siku tatu lakini ilinilazimu kuondoka, yaani nishindwe kuvuta embassy kisa ulokole wenu.
 
Hii ni bonge ya FACT mkuu, naunga mkono hoja!
 
🤣🤣🤣 Aisee nimecheka sana!
 
Sema pia inategemea na mazingira mbona kunawatu wananyumba kubwa na vyumba mpaka vya kufikia wageni na huduma zote unazozisema kwahiyo wewe mgeni ndio unapaswa kuangalia unapofikia pakoje.

Sema mimi wageni nawapenda sababu ni huleta baraka kiimani zaidi pia wageni ndio hukupa moyo wa kukufanya uzidi kuiboresha nyumba au makazi yako yawe yenye kuvutia.

Ila sio wageni wote wanapaswa kufikia nyumbani kwako pia lazima uwe na eligibility test Kwa nature ya mgeni.

 
Kwa upande wangu mikoa mingine yote nipo tayari kufikia kwa ndugu na ndugu wanafurahia uwepo wako unakua kwenye mazingira ya kupewa support kukamilisha ulichoenda kufanya, mahusiano na undugu unahimarika kwa kuonana

Ila kwa Dar kwakweli sipendi kufikia kwa mtu yeyote kuna kipindi nilifikia kwa watu kama watatu mara tofauti nikaona kabisa hawa nimekuja kuwaongezea mzigo hali siyo nzuri sana japo wanakua wakarim lakin mambo siyo sawa na ukitaka kuchangia chochote wanakataa maana wanaona inakua siyo uungwana kupokea mchango wako wa fedha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…