Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,558
- 64,966
Mwezi Oktoba huu ndio unaishia, tunaingia mwezi Novemba kwenda mwezi Disemba na baadaye mwezi Januari.
Kwa lugha za mtaani, tunaweza kusema ndio mwaka unaisha hivi.
Miezi niliyoitaja hapo juu, ndio miezi yenye matumizi makubwa kwa watu walio wengi; kwa sababu ni miezi yenye sikukuu za mwisho wa mwaka na kukaribisha mwaka, pamoja na visherehe vidogo vidogo vya kifamilia na kidini.
Ikifuatiwa na matumizi ya kuumiza ya kuandaa vijana kurudi mashuleni pamoja na kulipa ada kwa mwezi Januari, hasa kwa wale wenye familia na watoto. Kwenye kipengele hiki, wengi hujuta kuwa na watoto wengi, na kwa nini watoto wao hawakuwasajili kwenye shule za vidumu na mifagio.
Nikitafakari hii miezi naishiwa nguvu kabisa.
Nipo hapa kwa mangi, nimekuja kukopa balimi na safari.