Nikitaka kununua tv flat screen, ni brand ipi bora kwa sasa?

Nna duka la kuuza hivyo vitu
..trust me kwanza Samsung,pili Toshiba.tatu LG,zingine majanga Tu..
LG 32inch ni shilingi ngapi? Je zinatofautiana em nishauri nikichukua LG ya inch 32, ninunue yenye specifications zipi ndo bora kwa sasa?
 
Samsungu ndio kiboko wa matatizo...,kama ukikosa Samsung tafuta Philips...,
 
LG 32inch ni shilingi ngapi? Je zinatofautiana em nishauri nikichukua LG ya inch 32, ninunue yenye specifications zipi ndo bora kwa sasa?
inchi 32 mtumba 400,hadi 450.,mpya 850,000..kuna tofauti kubwa ya picha na picha..Samsung inatoa picha nzuri but gharama,,smartTv hizo zenye YouTube.Netflix,wireless,milioni na laki mbili..hizi ukipata na deck za blue ray..utatisha Sana.uzuri WA Sony kupata miwani HD rahisi..
 
Nna duka la kuuza hivyo vitu
..trust me kwanza Samsung,pili Toshiba.tatu LG,zingine majanga Tu..
Mara ya kwanza kununua LG smart TV, nchi 43, imekaa wiki 2, kioo kikawa kama kimevujia wino, mpaka leo nimeiweka store nimeshindwa kipata spaire ya kioo chake. Mdau mwenye kioo cha hii TV tuwasiliane tafadhali.
 
Bora kabisa ni ipi?
Mkuu kwa technology ya tv hakuna anayewazidi hawa watu wawili samsung na Lg maana kwenye technology ya vioo wao ndio wavumbuzi na wanatengeneza kila kitu wakati wengine wana outsource.
Kama mfuko unaruhusu chukua samsung au Lg
 
waliovumbua wameishakufa
 
Kuna watu kama watatu nimewauliza swali km hili na wamenipa jibu linalofanana.

Wameniambia brand bora kwa sasa ni Samsung, LG na Star X.

Wajuzi wanipe maujuzi nisijenunua kitu feki
Samsung LED.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…