Nikiwa kama Rais wa Mashabiki 'lia lia' wa Bendi ya Wenge BCBG yake JB Mpiana hapa JamiiForums naomba kuwajua Wenzangu tafadhali

My favorite, sema majina ya nyimbo ndio sijuagi
 
Hapa nilipo nassikiliza kitu laiiiiiini NO COMMENT SHENGEN hakika WENGE ilikuwa moto wa Gesi.
Sjui watu Wabad kama akina Kitshindja walienda wapi khaaaa?
Wenge Chali
Extra Music Chali
G 7 chali
Kwakweli music wa hizo bendi ulikuwa unasuuza moyo.
 
Huyo Burkina Faso ni mtu hatari mnooooo.
Je anamuweza logaloga?
Roga Roga Mwenyewe ambaye Jina lake halisi ni Ibambi Ikombi ameanza kujifunza Kupiga Gitaa la Solo wakati Burkinafaso Mbokaliya akiwa 'on Fire' na huyu ni Mwalimu wake katika Fani.

Roga Roga unaweza Kumshindanisha tu Wapiga Gitaa la Solo kama akina Flam Kapaya wa Wenge Maison Mere ya Werrason, Ramazani Fulutuni wa Quarter Latin yake Koffi Olomide, Pitchou Concorde wa Bendi ya Felix Wazekwa na Schevchenko Patou wa Bendi yake JB Mpiana ya Wenge BCBG.

Watu sahihi tu wa Kuwafananisha au Kuwashindanisha na Burkinafaso Mbokaliya katika Upigaji mahiri wa Gitaa la Solo ni Diblo Dibala, Dally Kimoko, Beniko, Cain Madoka, Alain Makaba, Mitre Ficarre Mwamba, Dilu Dilumona na Nene Tchacou.
 
Hapa nilipo nassikiliza kitu laiiiiiini NO COMMENT SHENGEN hakika WENGE ilikuwa moto wa Gesi.
Sjui watu Wabad kama akina Kitshindja walienda wapi khaaaa?
Wenge Chali
Extra Music Chali
G 7 chali
Kwakweli music wa hizo bendi ulikuwa unasuuza moyo.
Haya mliokuwa mnataka kumjua Alain Makaba alivyo balaa kwa Kupiga Solo Gitaa pamoja na Burkinafaso Mbokaliya hebu usikilizeni huu Wimbo wa No Comment Shengen kwa Makaba alipiga Solo namba Moja na Mbokaliya alipiga Solo namba Mbili.
 
Tuko sambamba mkuu ila nasikitika tu kusema moja ya nyimbo zangu pendwa "Pentagon" siioni HAPA
Wimbo huu ( huo ) wa Pentagone ndiyo ulimtambulisha rasmi Bingwa wa Kurapu ( Atalaku ) na Mwalimu wa Marepa ( Atalakus ) Wengi Congo DR aitwae Tutu Calugi ( Yombo Lumbu ) na ukitaka umsikie Calugi alivyo hatari kwa Kughani ( Kurapu ) msikilize katika Nyimbo za Etepe Buengo, Filandu na Coco Madimba zilizopo katika Album ya Pentagone ambayo ndiyo iliuza sana na mno mpaka ikawa ndiyo Chanzo Kikuu hasa cha Kusambaratika Kwao.
 
Ule wimbo wa Djojo Ngonda huwa naupenda sana!
 
Ule wimbo wa Djojo Ngonda huwa naupenda sana!
Na ni Wimbo mtamu zaidi ukipigwa Live ( Mubashara ) huku ukimuona Rapa ( Atalaku ) Kiongozi wa sasa Wenge BCBG Pitshou Lisimo ( GENTAMYCINE ) pamoja na Wasaidizi wake akina Fusee De Gaire, Pajo na Bin Laden Wakighani ( Wakirapu ) kwa kubadilishana na 'Wakiserebuka' kwa Ufundi zaidi.
 
Mimi werrasoni dam dam ,ngoja niwaone mnavyotililika wazee wa jb mzee wa kupotea,
Yaan yeye abadiliki bado anapiga melody zilezile za zamani
Ndo hapo palipo mpoteza kama blaze bula
 
Dah mkuu umemsahau kimbangu solo umemsahau wapi?yan waweza kusikiza tu ile gitaa peke yake na ukalizika mtafute youtube,alikuwa kwa werrah
 
Mimi werrasoni dam dam ,ngoja niwaone mnavyotililika wazee wa jb mzee wa kupotea,
Yaan yeye abadiliki bado anapiga melody zilezile za zamani
Ndo hapo palipo mpoteza kama blaze bula
Congo DR nzima Bingwa wa Live Shows ni JB Mpiana na Bendi yake Wenge BCBG ambayo huko Congo DR kwa Umahiri wake imepachikwa Jina la Utani la Le Equipe Nationale ( yaani Timu ya Taifa )

Mwamba wa Muziki Congo DR Koffi Olomide kila akihojiwa na Media mbalimbali ndani na nje ya Kwao huko kuwa ni Mwanamuziki gani 'Tishio' Kwake na amemfanya aumize Kichwa huwa hachelewi kumtaja 'Fundi' Jean Bedele Tshituka Mpiana.

Umeshajiuliza ni kwanini Wakongo wamembatiza JB Mpiana jina la 'Leadere Charismatique' na mpaka Wanamuziki Wengi wakubwa nao humwita hivyo hivyo? Ukiona GENTAMYCINE nampenda Mtu sana au Kitu mno jua kwa 100% ni Kizuri, Kimebarikiwa na hata Mwenyezi Mungu nae anapenda.
 
Hivi Tutu Caludgi yupo wapi kwa sasa? Jamaa alikua na kipaji halisi kabisa ambacho kwa sasa wengi hawana hata Fabrigas hajafika

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Hivi Tutu Caludgi yupo wapi kwa sasa? Jamaa alikua na kipaji halisi kabisa ambacho kwa sasa wengi hawana hata Fabrigas hajafika

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
Tutu Calugi ( kwa Utani huitwa Kalundjiste ) kutokana na kwamba alianzisha Shule yake ya Kuwafundisha Watu Kughani ( Kurapu ) huko Congo DR sasa yuko nchini Ufaransa akiwa amejikita zaidi katika Ulokole na Dini kama alivyofanya aliyekuwa Mpiga Gitaa la Solo wa Wenge BCBG Schevchenko Patou Solo ( aliyepiga vyema kabisa katika Album ya Kipe Ya Yo ) ambaye nae kwa sasa amekuwa Mlokole na anaimba na Kupiga Makanisani huko Ufaransa akishirikiana na Mkewe.

Moja ya Marapa ( Atalakus ) ambao walipitia katika Shule binafsi ya Tutu Calugi ( Kalundjiste ) ni Mukeba Kalondji ( Bill Clinton ), Eyale Kalondji ( KEROZENE ), Theo Mbala, Celeo Mozami Muviu, Fusee De Gaire na Zaparo ambaye kwa sasa ndiyo Rapa ( Atalaku ) mahiri wa Bendi ya Extra Musica Zangul yake Roga Roga ( Ibambi Ikombi )
 
Daaa ile shughuli si ya kitoto ndio Mana hadi makoo huwa yanaleta shida. Mungu amtendee vema!
 
Niliwahi kugoogle lakini sikuona taarifa zake za kutosha,

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…