nikiwa na 40mil naweza jenga nyumba ya namna gani....

nikiwa na 40mil naweza jenga nyumba ya namna gani....

Nimemjengea mtu nyumba tegeta ya vyumba vitau na masta moja dining jiko na stoo, varanda mbili tena zote zimemwagwa zege....shiling mil30 imetumika mpaka sasa na imebaki rangi, alluminium, na gypsum tu.....

Kuanzia hapo ndo utakuja jua kwamba ujenzi wa nyumba ni finishing' mkuu sio boma. Nami niliwahi kusimamisha boma moja kwa 45m, nikaanza kujiona nimeukata, aisey ilinichukua zaidi ya hiyo kuwa na 'nyumba' almanusura nigombane na mafundi, gypsum, rangi, aluminium,tiles,toilets,wiring, water system, nk,acha kabsaa!
 
Nimemjengea mtu nyumba tegeta ya vyumba vitau na masta moja dining jiko na stoo, varanda mbili tena zote zimemwagwa zege....shiling mil30 imetumika mpaka sasa na imebaki rangi, alluminium, na gypsum tu.....
We ni fundi wa kawaida, Engineer, Msimamizi, au vyote?!
 
Hiyo pesa inatosha kujenga nyumba rooms 3 , kimoja master ,sebule dinning ,public bathroom pamoja na jiko as long u
na kiwanja tayari
Mchanganuo
Matofali 2000 x 1000 = 2 M
Cement 50 bags = 0.7M
Mawe na mchanga 0.7M
Ufundi mpaka lenta= 1.5M
Nondo za lenta =0.8 M

Kupaua
Bati za south 12000 kwa mita bati 90 =3.3M
Kofia. 0.6 M
Mbao za kupaua 3M
Fundi wa kupaua 0.6M

Piga hesabu hadi kupaua alafu imebaki ngapi ntakuja na finishing calculations

Kwa bei hizo nadhani nahitaji kujenga sasa.
Fundi ameniambia Kujenga msingi tu 2.5-4m
 
Wasikukatishe tamaa bana unaweza kujenga room tatu, sebule, choo, jiko bila hofu kama tu una kiwanja tayari. Mambo ya finishing mapema mapema mbwembwe tu, uwaweza kufanya finishing ndani tu ukahamia, halafu hayo mengine taratibu yatajipa.

Sisi wengine tulifanya hivyo, tukamalizia kwa kutumia pesa ya kodi ya pango ambayo iliokolewa kutokana na kuishi kwangu, leo hii nyumba yangu haina tofauti na mfanyabiashara mkubwa, na geti juu.

Safi sana kaka wewe unafahamu mambo big up ushauri mzuri sana kwa mwenzetu,Ubarikiwe
 
We ni fundi wa kawaida, Engineer, Msimamizi, au vyote?!

vyote mkuu...tena hapo labda sijaeleweka ni hivi kwa hiyo pesa nilotaja ni pamoja na plaster, grill, wiring, na drainage mpaka na mashimo, na blundering, so kilichobaki ni kuweka gypsum, alluminium na rangi tu
 
Taratibu ukianza unamaliza tu,issue kubwa mijini ni kiwanja cha kujengea....
 
Wasikukatishe tamaa bana unaweza kujenga room tatu, sebule, choo, jiko bila hofu kama tu una kiwanja tayari. Mambo ya finishing mapema mapema mbwembwe tu, uwaweza kufanya finishing ndani tu ukahamia, halafu hayo mengine taratibu yatajipa.

Sisi wengine tulifanya hivyo, tukamalizia kwa kutumia pesa ya kodi ya pango ambayo iliokolewa kutokana na kuishi kwangu, leo hii nyumba yangu haina tofauti na mfanyabiashara mkubwa, na geti juu.

Hii staili inatutoa wengi.

Sent from my LT26i using Tapatalk 2
 
Mi nawashangaa sana wanaosema heti millioni 40 ni ndogo,mshikaji hiyo hela hata guest unajenga,cha msingi usimtumie mtu especially mashemeji zako kusimamia mjengo,wewe kusanya material kisha chukua likizo ushinde mwenye site,utagundua ni jinsi gani hiyo hela ilivyo nyingi sana katika ujenzi.
 
Self container!!!!

Hilarious

Hawaii_Single_Container_Housing.jpg
 
Ni kweli pesa ni nyingi sana
Mi nawashangaa sana wanaosema heti millioni 40 ni ndogo,mshikaji hiyo hela hata guest unajenga,cha msingi usimtumie mtu especially mashemeji zako kusimamia mjengo,wewe kusanya material kisha chukua likizo ushinde mwenye site,utagundua ni jinsi gani hiyo hela ilivyo nyingi sana katika ujenzi.
 
Hata mie nawashangaa, mie kuna nyumba arusha imejengwa kwa 5m? Ila fnshng tu ndo bado? Khaa unanikatsha tamaa
 
Wewe anza kujenga nyumba ya kawaida yenye vyumba vitatu vya kulala, sebule, dinning room na jiko. Endelea kujenga kwa kutumia fedha zako kwa uangalifu na kuzingatia bei. Hapo utakapofikia utamalizia baadaye kwani sio mwisho wa kupata fedha. Kama unapanga, hakikisha unajenga nyumba ambayo unaweza kuanza kuishi hata kabla hujamaliza. i. e kujenga na kuweka paa na milango na madirisha halafu uhamie huku ukiendelea kumalizia. usikate tamaa
 
Back
Top Bottom