Mipangomingi
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 2,713
- 2,062
Nimemjengea mtu nyumba tegeta ya vyumba vitau na masta moja dining jiko na stoo, varanda mbili tena zote zimemwagwa zege....shiling mil30 imetumika mpaka sasa na imebaki rangi, alluminium, na gypsum tu.....
We ni fundi wa kawaida, Engineer, Msimamizi, au vyote?!Nimemjengea mtu nyumba tegeta ya vyumba vitau na masta moja dining jiko na stoo, varanda mbili tena zote zimemwagwa zege....shiling mil30 imetumika mpaka sasa na imebaki rangi, alluminium, na gypsum tu.....
Hiyo pesa inatosha kujenga nyumba rooms 3 , kimoja master ,sebule dinning ,public bathroom pamoja na jiko as long u
na kiwanja tayari
Mchanganuo
Matofali 2000 x 1000 = 2 M
Cement 50 bags = 0.7M
Mawe na mchanga 0.7M
Ufundi mpaka lenta= 1.5M
Nondo za lenta =0.8 M
Kupaua
Bati za south 12000 kwa mita bati 90 =3.3M
Kofia. 0.6 M
Mbao za kupaua 3M
Fundi wa kupaua 0.6M
Piga hesabu hadi kupaua alafu imebaki ngapi ntakuja na finishing calculations
Kwa bei hizo nadhani nahitaji kujenga sasa.
Fundi ameniambia Kujenga msingi tu 2.5-4m
wadau nisaisieni nikiwa na kama 40mil naweza jenga nyumba ya namna gani kwa hapa dar
Wasikukatishe tamaa bana unaweza kujenga room tatu, sebule, choo, jiko bila hofu kama tu una kiwanja tayari. Mambo ya finishing mapema mapema mbwembwe tu, uwaweza kufanya finishing ndani tu ukahamia, halafu hayo mengine taratibu yatajipa.
Sisi wengine tulifanya hivyo, tukamalizia kwa kutumia pesa ya kodi ya pango ambayo iliokolewa kutokana na kuishi kwangu, leo hii nyumba yangu haina tofauti na mfanyabiashara mkubwa, na geti juu.
We ni fundi wa kawaida, Engineer, Msimamizi, au vyote?!
Wasikukatishe tamaa bana unaweza kujenga room tatu, sebule, choo, jiko bila hofu kama tu una kiwanja tayari. Mambo ya finishing mapema mapema mbwembwe tu, uwaweza kufanya finishing ndani tu ukahamia, halafu hayo mengine taratibu yatajipa.
Sisi wengine tulifanya hivyo, tukamalizia kwa kutumia pesa ya kodi ya pango ambayo iliokolewa kutokana na kuishi kwangu, leo hii nyumba yangu haina tofauti na mfanyabiashara mkubwa, na geti juu.
Mi nawashangaa sana wanaosema heti millioni 40 ni ndogo,mshikaji hiyo hela hata guest unajenga,cha msingi usimtumie mtu especially mashemeji zako kusimamia mjengo,wewe kusanya material kisha chukua likizo ushinde mwenye site,utagundua ni jinsi gani hiyo hela ilivyo nyingi sana katika ujenzi.