Nikiwaambia msioe muwe mnasikia; kwa miezi 4 mwamba kaishi maisha magumu bila mshahara kumbe mkewe ana laki 8 ndani, na usaliti juu kaambulia

Nikiwaambia msioe muwe mnasikia; kwa miezi 4 mwamba kaishi maisha magumu bila mshahara kumbe mkewe ana laki 8 ndani, na usaliti juu kaambulia

Kuna binti alikuja niomba ushauri kuwa anataka kuingia katika ndoa na jamaaa m'moja ambaye yupo vema kimaisha, anampenda na yupo tayari kumuoa hata kesho.

Me nikamuuliza swali unategemea nini kutoka kwa jamaa ndoa ikishafungwa yaani awe na wajibu gani kwako katika maisha yenu pamoja. Akanitajia vitu vya kawaida tu kuwa anitunze, nipatie mahitaji kama mavazi, urembo, pocket money, ahudumie watoto, alipe kodi na tujenge ya kwetu, anisaidie pia wazazi na ndugu zangu pale wanapohitaji msaada wangu,anifungulie biashara yangu, anipende kwa dhati asinisaliti wala kuwa na mwanamke mwingine nje yangu yaani awe mwaminifu.

Nikamkatisha kwa kumwambia sawa kwakifupi awe vema kifedha ili aweze kukupa yote hayo sababu akiwa hana pesa then 90% ya hayo uliyosema hayatafanyika.

Nikamuuliza sasa wewe jamaa anataka kukuoa , ategemee wewe kutimiza majukumu yapi na kuwa na wajibu gani kwake?!

Akasema, nitamzalia na kulea watoto wetu, nitampikia chakula kizuri, nitampa penzi kitandani,nitamfulia nguo na usafi wa nyumba, nitakuwa namfariji wake. Kamaliza.

Nikamuuliza kwahiyo hayo ndio majukumu na wajibu wako?! Akajibu ndio.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Nikamwambia achana na ndoa nenda kaombe kazi ya uhousegirl tu, sababu nimekusikiliza unanitajia majukumu ya house girl na mdangaji kwa asilimia kubwa, sijaona ukinipa majukumu ya MKE WA MTU.
 
Eeeh bwana ehh ni Mimi Mr. Liverpool Tena.

Weekend hii tumempiga Manure na nyundo Kali sanaa mpaka kapoteana.!!
Sasa jiulize ile ilikua Old Traford, je wakija Anfield..!!!
Wewe hua unapenda kuwaambia wenzako wasioe ila subiri siku yakukute ndo utajua maana ya Mke hlf yakikukuta njoo ulete stori hpa kma unavoleta za wenzako
 
Kila mtu afanye analoona kwake ni sawa, kuna watu wameoa na wanaishi fresh kabisa sio ndoa zote ni mbaya kuna ndoa zingine watu wanafurahia.
 
We jamaa utakua una shida mahali alafu unapretend uko sawa. Mwandiko wako tu unasadifu hayo.
Budah..!!
Mtu yeyote anaye amini tofauti na unachoamini haimaanishi ana tatizo.

Anamaanisha AKILI ZENU HAZIFANANI.

Umekua kinara wa kukatisha tamaa watu wasioe..sijui unafaidika na nini kumtumikia shetani.
Kutokuoa ni ushetani?
Kwahiyo..
Mapadre, Benzos, Dangote, Bill gate, Judge mkuu fulani (certain time) wa Kenya, Kanye west na wengine wengii wenye mafanikio duniani hawajaoa au wamekimbia ndoa.

HAWA WOTE NI MASHETANI
Mungu akusaidie sana maana seems una changamoto tusiyoijua..
Kukataa kuoa hakuusiani na Mungu ni maamuzi yako binafsi.

Ina maana Rajan Ratan mwenye kampuni ya Eicher Tajiri mkubwa India hajaoa.

Ana changamoto yoyote na Mungu?

MUNGU HUBARIKI MAAMUZI YA MTU.

TAFUTA HELA KIJANA ILI ULE MAISHA.

Usisahau nyuzi za malalamiko humu kila siku tunaletewa.

#YNWA
 
Shameless... akili za kivulana hizi. Kwahiyo upuuzi wa mke wa john ndo unahalalisha ndoa ziwe batili? I swallow my words. Unashangaza sana. Yana ndo mnakaaga vijiweni munafarijiana hivi? U need some help

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
The help I need is MONEY and MORE MONEY ili nifaidi maisha.

We subiri mumeo akose pesa watu wazijue rangi zako vizuri.

Nasikia siku hizi mnawaita "mbwa" na sio mume wangu Tena.

Ila pia usome humu ndani watu wanavyofunguka.

Usisahau Comment #40

#YNWA
 
Wewe hua unapenda kuwaambia wenzako wasioe ila subiri siku yakukute ndo utajua maana ya Mke hlf yakikukuta njoo ulete stori hpa kma unavoleta za wenzako
Kuna wenye wake yamewakuta makubwa na yakawaua kwasababu ya mke.

Husikii Wala husomi kila fulani kaua na yeye kajiua kwasababu ya mke?

Unadhani yule mwamba wa Kigamboni bila kuoa angekua kachoma mtu na gunia la mkaa na muda huu anasubiri kunyongwa tu mahabusu..!!!

Hawa wameao, mbona sasa matatizo yanawakuta?

Ila hizi comment humu unazisoma.

Anza na #40.

#YNWA
 
Hawa watu inataka moyo sana kuishi nao! Yani kimsingi hamna haja ya kushangaa huyo mke jamaa alifosi yeye
Wenye moyo endeleeni kuishi nao kwa moyo mimi huwa naishi nao kwa akili na ukauzu..

Pili huwa najitahidi kuwe na uwajibikaji wa wote,siwezi toa mtaji mimi afu pesa mtu aseme ni zake,aisee ataenda kwa baba yake ampe mtaji Ili atafute pesa zake.
 
Kila mtu afanye analoona kwake ni sawa, kuna watu wameoa na wanaishi fresh kabisa sio ndoa zote ni mbaya kuna ndoa zingine watu wanafurahia.
Nyingi ni Vimeo hata hao unaosema wanaishi vizuri inategemea uelewa wa mwanamke na mwanaume..
 
Hapo ndipo huwa nachoka na hutu tu story twa wanaojiita wazee wa system

Kwahiyo mnatushauri tutafute hera mpaka tuzeheke na watoto tutawapataje ili kutimiza andiko la Mungu nendeni mkaijaze Dunia.
 
Wengi wanaoa wasindikizaji, ndio maana hizi changamoto wanakutana nazo
 
Eeeh bwana ehh ni Mimi Mr. Liverpool Tena.

Weekend hii tumempiga Manure na nyundo Kali sanaa mpaka kapoteana.!!
Sasa jiulize ile ilikua Old Traford, je wakija Anfield..!!!

Turudi kwenye mada ....

HIVI KWANINI HAMSIKII NIKIWAAMBIA MSIOE ??[emoji15][emoji15][emoji15]

Sasa Kuna mwenzenu yamemkuta huku ......

Nimemsikitikia sanaaa "Hiii BAGOSHAAAA" (in jiwe's voice)

Mr. Liverpool ni mfanyakazi na mkuu wa idara fulani katika moja ya Halmashauri nchini.

Ana rafiki yake nae ni mkuu wa Idara (kaimu) nyengine (tumuite John).

John kuna jambo alizingua mwezi wa 2 akapigwa SP (Due to Absentees - alisepa kazini wiki bila ruhusa Wala taarifa na aliondoka kiboya hasaa).

John aliishia miezi 4 bila mshahara (akipambana na nisamehe na kumbembeleza HR mpaka wakafungua mshahara, waliufungua mwezi wa 6).

Jana nikaona nipige na John story; "Alitoboa vipi maisha miezi 4 bila MSHAHARA" Tuliongea mambo mengii ila Kuna jambo kanisikitisha sanaaa.

Anasema ........

Kipindi hana mshahara ndio aliijua rangi halisi ya mkewe..!!
Kaishi na mkewe miaka 5 ila hakujua huyu mkewe yuko hivi..!!

Mwezi wa 4 ndio ulikua mwezi mgumu. Hali ilikua ngumu japo kwa nje hakuonyesha.

Alivyoona mambo magumu hasa ilibidi amshirikishe mkewe. Alimueleza kila kitu mkewe japo mkewe ana duka la mahitaji ya nyumbani ambalo alifunguliwa na John ila alimjibu hana kitu.

(John alioa mama wa nyumbani ila aliamua kumfungulia duka ili asiwe wa nyumbani kabisa..!!!)

Ikabidi John anyamaze tu "mtu gani kwenye biashara miaka miwili apati faidi ye kila siku anatangaza hasara?"
John alijiuliza mengi akaona anyamaze alale.

Maisha yalikua taiti, John alikosa hela ya bia na ya manhood (kulinda wallet).
Ye alikua ana hakikisha tu mwanae mmoja wa ndoa anakula na kufurahi.

Kumbe bana John alikua anapitia mengi kwa siri sanaa na hata kula alikua anakula mgahawa wa mbali ili tusimuone yule mzoea makuku ana kula maharage..!!!

Aliogopa aibu na maneno ya walimwengu.

Kuna siku hali ya ugumu ndio ilizidi alirudi home empty (kazini hakupata dili wala kaposho cha kikao).
Kukopa hataki (atalipa nini na hana mshahara?).

Kufika home akamshirikisha mkewe, mkewe akatoa jibu lile lile SINA HELA..!!!

Asubuhi ya siku ifuatayo ilifika aliwazaa akaona leo haendi kazini. Alimwacha mkewe aende dukani, John aliamua kufanya searching nyumba nzima.

Alikuta vifuatavyo:-

1. Kwenye begi la nguo lilikua limechanwa chini.
Alijiuliza begi jipya kuchanika..!! akakuta mule kwenye mchano Kuna vidonge vya uzazi na laki 3 kamili..!!!

2. Akainua godoro, kwa mwisho kwenye kono ya godoro akakuta kuna laki 5.

Akafanya searching kubwaa sanaa kwenye chumba chao cha kulala. Anakwambia alivyovigundua vilimfanya apate hasira hasaa.

Alitoka kwa hasira mpaka dukani kwa mkewe. Akamkuta mkewe anahudumia mteja, kuangalia simu akakuta haijajifunga (mkewe alikua akiangalia kitu YouTube)

John alizuga pale dukani akaiba ile simu akaenda kujificha ili aifanyie upekuzi.

Alivyoviona ........

1. Kumbe mkewe ana bwana ambae alikuaga mwanafunzi mwenzake chuo.

2. Na kwa kusoma sms, inaonyesha huyo jamaa ni X wa mke, na jamaa kapata Kazi mkoa huu huu tuliopo.

3. Mke wa John alimlipia jamaa kodi ya kuanzia maisha kazini na godoro alimnunulia.

3. Mke wa John anavyosemaga anaenda mjini kujumua vitu vya dukani huwa anashukia kwa mwamba ambacho ni chumba cha mke wa John na X..!!

4. Kwenye chatting ya WhatsApp inaonyesha X alimshauri mke wa John waache kutumia P2 ila mke awe anakula vidonge vya majira..!!!

Yaani John Ali screenshot kila chatting akajitumia WhatsApp.
Kwa kuonyesha ukatili hakufuta zile picha ili mkewe ajue kwamba John amejua.

Sasa haya yametokea Kati ya mwezi wa 4 mpaka wa 6.
John anasema anahitaji kuvunja ndoa.

Mke kuona John haitaki tena ndoa kakimbilia kanisani.
Mchungaji alimuita John, John alijibu "Mumewe huyo ni Michael (X)"

Mke akakimbilia kwa wazazi aombewe msamaha.
Wazazi wa mume na mke wamekaa, ila John anasema aliomba ili aelewe cha mtu basi yafanyike mazungumzo mengine na kwenye hayo mazungumzo Michael (X) awepo.

Ila Michael aligoma kabisaa kutimba kwenye usuluhishi na kwa taarifa ya mke pale alipokua anaishi Michael kahama na hajui kahamia wapi na namba za simu hazipatikani tena...!!!

John aligoma kumsikiliza yoyotee kwahiyo wazazi walisepa bila maelewano.

Nilichoshangaa sasa, anasema... Hajawahi kuongea na mtu juu ya hili ila Mimi kumuuliza mambo ya ku survive bila mshahara ndio kumemfanya animwagie yotee kama kushusha mzigo wa fikra..!!!

John haitaki tena ndoa na mpaka tunavyoongea hapa kasha file kesi ya talaka.

Kwake hajafika tokea mwezi wa 6 na nyumba haitaki tena.

John huenda kumchukua mwanae shule akitoka siku za Ijumaa huenda nae gheto lake jipya huku akimtaarifu mkewe "mtoto yupo kwangu".

Mshahara ulivyofunguliwa John kumbe kapanga chumba karibu kabisa na kwangu..!!

Kanunua vitu vichache vya kuanzia maisha.
Kaamua kumuachia mkewe nyumba tu aishi na mwanae.

Ye kaondoka na Shamba la Eka 10 na kiwanja chenye pagala..!! Hati ya nyumba kaacha kwa mkewe ye kaondoka na documents za kiwanja cha pagala na Shamba.

Kabla mahakama haijaamua John kashagawa mali na maisha yanasonga...!!!

Nilichofanya nilienda kupajua kwake alikopanga maana sasa Mimi ndio nimekua jirani yake..!!

Kwenye pagala lake anataka ajitahidi amalizie hata vyumba viwili ahamie maana maisha ya kupanga alishayasahau kabisaa.

TURUDI KWENU WANAUME WABISHI ......!!!!

Na hizi ndio ndoa zenu mnazokimbilia.

Mwamba alijifanya kupenda akamfungulia mpaka biashara kumbe POLE YAKE.

NIKIWAAMBIA MSIOE MUWE MNASIKIA.

Nani kakwambia kuwa wanakupenda?

Braza They love your wallet..!!

Huyu alimpenda John au alipenda pesa za John za kufungulia biashara??

Just hook with them halafu pita hivi kabla wallet haijaisha.

Ila man usisahau kuwezekeza kwenye Mali na akili (financial knowledge).

SECURE YOUR FINANCIAL FUTURE.

When You have ASSETS and FINANCIAL KNOWLEDGE, Then it's ENOUGH..!!!

PESA NDIO KILA KITU, Huoni ZILIVYOMUOKOA RAFIKI YANGU JOHN.

#YNWA
Usije ukaingia kwenye 18 za HR .hakuna rangi utayoacha kuiona vizuri
 
Back
Top Bottom