Mtamile
JF-Expert Member
- Aug 2, 2011
- 2,838
- 1,274

Kitendo cha rapper Kimbunga kuachia wimbo wenye mahadhi ya Kwaito,uitwao Usitukane aliomshirikisha Chege, kimemfanya Nikki Mbishi aichome moto album ya rapper huyo aliyokuwa nayo ndani mwake kwa kile anachosema ni uchafu uliokuwa mahala isiyo sehemu yake.
Nikki Mbishi anaamini kuwa Kimbunga ameuasi muziki wa hip hop kwa kile anachodai ni kutokana kuendekeza njaa.
Mimi siafikiani na hicho alichokifanya huyo jamaa ambaye mimi niliona bora nifanye usafi hususan kwa wimbo wake alioutoa sasa hivi na taswira aliyojivika kutoka mwanzo, kaniongopea yaani, amesema Mbishi.
Na afadhali angekuwa amefanya Kwaito basi tunazoziona kama za Mafikizolo, kwasababu wale wanaimba kwaito mbona tunapenda, sio hizi, hizi zimekaa kinjaanjaa.
Nikki Mbishi amesema wasanii wanaojiita wanafanya hip hop wanatakiwa kuwa na msimamo sio kufanya muziki wasiouweza ili kupata shows na kwamba yeye ataendelea kuwa na utambulisho ule ule.
Mimi ntabakia kuwa vilevile unavyonifahamu na identity yangu ndio hii hii na character yangu ndio hii niko nayo mimi. Kwahiyo watu wasitegemee chochote cha tofauti kutoka kwangu na hii ni nadhiri naweka, ameongeza.
Nyimbo yenyewe hii hapa Kimbunga ft Chege - Usitukane by ChaliiMusic - HulkShare
source: Kikwetu Kwetu Blog - Kikwetu Kwetu Blog