Nikki Mbishi aichoma moto album ya Kimbunga, kisa rapper huyo kufanya wimbo wa ‘Kwaito’

Nikki Mbishi aichoma moto album ya Kimbunga, kisa rapper huyo kufanya wimbo wa ‘Kwaito’

Mtamile

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
2,838
Reaction score
1,274
Nikki-Mbishi-pic-620x400.jpg
Kitendo cha rapper Kimbunga kuachia wimbo wenye mahadhi ya Kwaito,uitwao ‘Usitukane’ aliomshirikisha Chege, kimemfanya Nikki Mbishi aichome moto album ya rapper huyo aliyokuwa nayo ndani mwake kwa kile anachosema ni ‘uchafu uliokuwa mahala isiyo sehemu yake.

Nikki Mbishi anaamini kuwa Kimbunga ameuasi muziki wa hip hop kwa kile anachodai ni kutokana kuendekeza njaa.
“Mimi siafikiani na hicho alichokifanya huyo jamaa ambaye mimi niliona bora nifanye usafi hususan kwa wimbo wake alioutoa sasa hivi na taswira aliyojivika kutoka mwanzo, kaniongopea yaani,” amesema Mbishi.
“Na afadhali angekuwa amefanya Kwaito basi tunazoziona kama za Mafikizolo, kwasababu wale wanaimba kwaito mbona tunapenda, sio hizi, hizi zimekaa kinjaanjaa.
Nikki Mbishi amesema wasanii wanaojiita wanafanya hip hop wanatakiwa kuwa na msimamo sio kufanya muziki wasiouweza ili kupata shows na kwamba yeye ataendelea kuwa na utambulisho ule ule.
“Mimi ntabakia kuwa vilevile unavyonifahamu na identity yangu ndio hii hii na character yangu ndio hii niko nayo mimi. Kwahiyo watu wasitegemee chochote cha tofauti kutoka kwangu na hii ni nadhiri naweka,” ameongeza.

Nyimbo yenyewe hii hapa Kimbunga ft Chege - Usitukane by ChaliiMusic - HulkShare
source: Kikwetu Kwetu Blog - Kikwetu Kwetu Blog
 
Kimbunga ni fake mcee aliepata attention kupitia mabingwa wa promo wale suckers.
 
eti anajiita mfusi wa ruuge!! kimbng cho ko yule..

Ilikua ipo wazi asingeweza kuudanganya umma kwa muda mrefu ilikua lazima arudi kwenye asili yake na ashatumika kama wenzie kumtumikia bepari acha apotee.
 
Ilikua ipo wazi asingeweza kuudanganya umma kwa muda mrefu ilikua lazima arudi kwenye asili yake na ashatumika kama wenzie kumtumikia bepari acha apotee.
wack sana yule jamaa.. napale wafu fm kuna staff atakuw anampasua kama c kupasuliwa..
 
Kimbunga naona anajaribu kufata upepo wa Nay, anatamani kuwa kama Nay kitu ambacho hakiwezi
 
inasemekana madee, nay, wametoka kwa hiphop wamehamia bongo fleva na wamepata mafanikio makubwa na ya ghafla tofaut na mwanzo...
so kimbunga anahisi atapata cloud ya kutosha kupitia style hizo..
 
kimbunga nilimkubali sana baada ya kutoa ngoma yake ya ''non movement alignment,,,,2009 kama sikosei,,,he was real,,,lakin baada ya kujiingiza kwenye crew ya hao watu wa clouda jamaa kabadilika,yaan anafanya mziki sijui niuweke kundi gan,,,in short to me jamaa is no longer a hip hop music artist,,,,,Sana tu Nikk,,safisha uchafu getto,,,tamadun music fo rever.
 
Kuchoma album ya mtu mwingine ni ujinga na kutafuta attention ya watu.

Bora kama angesema amechoma copy ya hiyo single kama alikuwa nayo ndani kwake...na kwanini uichome moto?
 
Mnampa promo tu huyo kimbunga,sijawah kumkubali toka nilipoanza kumsikia
 
Huu ni ugonjwa na kutafuta umaarufu. Yani ana mpangia mwanaume mwenzia jinsi ya kutafuta pesa?
 
kwa sababu niki mbishi ana degree yake so anafikiri kila mtu ana uhakika
 
Back
Top Bottom