Nikki wa II, siasa hazikufai, chunga mdomo wako

Nikki wa II, siasa hazikufai, chunga mdomo wako

Huyu jamaa pamoja na masters yake ya D.S bado hawezi kichambua vitu ku link vitu vizuri si siasa, uchumi hata mambo ya kijamii kulikua na kipindi aliki host TV1 yaani ni mjinga mjinga hivi haeleweki sijui anaongea ongea vitu daaahh aiseee shule zingine hizi...
Hawezi kupanga hoja zikawa na mtiririko mzuri yani akisimamia kimsimamo chake habadiliki. Hana skills za kuongea
 
wana ukawa hebu mjitambue! Yaani hawa jamaa! Ukiwa tofauti na mawazo yao wewe ni tatizo!! Wamejaa Ushabiki tu na matusi!! Hoja hawana ni kuropoka! Tu
Kama dini(iman) za watu zinachambuliwa itakuwaje vyama vyenu,wanachama wenu,viongozi wenu wasichambuliwe! Kila atakayewapinga ni ccm!! ACHENI UTUMWA WA FIKIRA!
 
Kati ya wasanii ninaowaelewa pindi wanapoongea basi ni Niki wa Pili.... Jamaa yuko vizuri sana kichwani, ana uelewa mpana sana sio kwenye mambo ya muziki tu bali hata mengineyo.... Na kama ww unayefanya nae mahojiano mweupe kichwani unaweza kujikuta huna cha kumuuliza na kubaki ukimsikiliza akimwaga madini..... In short jamaa anajielewa sana na elimu yake inamsaidia yy pamoja na jamii kwa ujumla.. Ana ushawishi fulani hiv na kumsikiliza huchoki... Ni mtizamo tu wakuu msijenge chuki.
 
wana ukawa hebu mjitambue! Yaani hawa jamaa! Ukiwa tofauti na mawazo yao wewe ni tatizo!! Wamejaa Ushabiki tu na matusi!! Hoja hawana ni kuropoka! Tu
Kama dini(iman) za watu zinachambuliwa itakuwaje vyama vyenu,wanachama wenu,viongozi wenu wasichambuliwe! Kila atakayewapinga ni ccm!! ACHENI UTUMWA WA FIKIRA!

Exactly!
 
Hata mimi nimeliona hilo mkuu.Ila bado mdogo atabadilika na kuwa bora siku zinavyokwenda.
Ajitahidi mana ni msomi kuna siku alikua na afande sele alikua ana mshinda kwenye mtiririko wa hoja.
Ni msomi lakini hawezi kupanga hoja kwa political context and content ya kibongo.
 
Sasa yeye kutoa hotuba kwa niaba ya wasanii ndo anajiona amefika, pamoja na shule yake mambo ayafanyayo aisee atapotea kabisa, msanii bila support ya wananchi ni useless. Kuna wasanii mbona wamepiga kimya kuepuka kuwagawa mashabiki. Wasanii wawe makini sana uchaguzi huu la sivyo watakua historia

Ni kweli kabisa huyu dogo anajiharibia sana kwasasa katika muziki wake.
 
Nikki yuko smart sana kichwani, pamoja na usanii wake still anawakimbiza wengi tu kiupeo watu mnaowaamini kwenye siasa, tatizo lenu Chadema na UKAWA ni hili mtu akiongea kitu ambacho hamtaki kukisikia mnapanick na anakuwa adui kwenu, yaani nyi kilasiku mnataka msifiwe tuuu mtu akienda kinyume chenu ni tatizo.

Naona saivi kwenye Jukwaa la siasa jamaa anaitwa POLEPOLE anashambuliwa kweli kwenye nyuzi mbalimbali kisa anazungumza msichotaka kukisikia, but siku za nyuma alipokuwa upande wenu mlikuwa mnamsifia sana na kumwita JEMBE. Nikki, we Fanya kazi yako, nakuamini sana, achana na hawa wanaolialia.
 
Hivi mtanaka kila mtu awe anasupport mnachotaka mbona mnakuwa bias sana kila mtu ana uhuru wake anachokiona hebu acheni kulazimisha kila mtu awe upande mnaotaka nyinyi yani watu wanalazimisha kila kitu acheni jamaaa awe uhuru
 
Umewahi hudhuria show zake?.
Umewahi kununua kazi zake?

Mwacheni awe huru

Mkuu kama haufahamu Weusi nawakubali sana tena sana na Nikki wa 2 namkubali pia,na nimeandika hivi si kumponda bali najaribu kuweka wazi ukweli kuwa akijihusisha na siasa atapoteza baadhi ya mashabiki wake,kwani mashabiki/watanzania wapo kimirengo tofauti tofauti. I hope unaelewa nachomaanisha
 
Mkuu kama haufahamu Weusi nawakubali sana tena sana na Nikki wa 2 namkubali pia,na nimeandika hivi si kumponda bali najaribu kuweka wazi ukweli kuwa akijihusisha na siasa atapoteza baadhi ya mashabiki wake,kwani mashabiki/watanzania wapo kimirengo tofauti tofauti. I hope unaelewa nachomaanisha
Watanzania wengi hawapendi ukweli ndo tatizo unafiki ndo sifa kuu yao mada ni nick mtu anaingiza Ukawa sijui madudu gani. Nick ana shule ila mtiririko wako mhhhh anyway maisha ni yake afanye alipendalo si kila akusifiaye anakukubali criticism zimewajenga watu wengi waliokubali mapungufu yao na kuyatendea kazi.
 
Huo ni mtizamo wako brother, sio jambo LA busara kila jambo lifanyike vile unavyotarajia. Hivi kama angeongea sawa na vile unavyodhani ungeongea haya! Kila mtu ana haki na utashi. Haitawezekana wote tufikiri sawa Kaka. Labda kama anatumia nafasi aliyonayo (media) kuwashawishi wasanii Ila kama unakosoa hoja zake yeye kama yeye sidhani kama utakuwa unamtendea haki as naye ana utashi wake na mawazo yake. Ila tuache ushabiki, kama jambo ni zuri basi tukiri kwamba ni zuri na kama baya likewise na sio kuhitimisha jambo kwa ushabiki wa Chama.
 
Nick kama wee ni ccm tusikuone Arusha, uku hatutaki wapuuzi watu tuna makovu kwasababu ya hawa jamaa.
 
ndo tatizo la siasa za tz hasa hawa bavicha yaani ni bure kabisa, wanataka wao ndo wakuendeshe
 
Karume ashasema ukimpenda mtu mpende kiasi na pia ukimchukia mtu mchukie kiasi vilevile ,wote mmechangia kwa usawa yeye mwenyewe apime anocho ona kinafaa alifanyie kazi
 
Msiposikiliza anachukua vyeti anazama kwenye soko la ajira hivyo vtisho vya kususia muziki wake kamtisheni Nuhu Mziwanda
 
Back
Top Bottom