Nikki wa Pili ayape heshima mavazi ya kitaaluma. Achague kuwa PhD holder ama abaki na swagger zake za kisela

Nikki wa Pili ayape heshima mavazi ya kitaaluma. Achague kuwa PhD holder ama abaki na swagger zake za kisela

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Ni kama mtu anayevaa kanzu na barakashia alafu mkononi anachupa ya bia ama msokoto wa bangi. Si sahihi kabisa.

Screenshot_20180422-173658.png


Screenshot_20180422-173644.png

Habari za wakati huu ndugu zangu wa hapa JF.

Leo naomba tujadili hili suala la mtu mmoja kuvaa kofia mbili ambazo kwa mtazamo wangu haziwezi kuvalika kwa wakati mmoja.

Naomba tujadili hili with reference to Nikki wa pili msanii mwanamuziki wa hip hop mbaye yupo mbioni kutunukiwa PhD. Soon Nikki will be having a doctorate.

Hivi katika hali ya kawaida ya maisha inawezekana vipi kwa msanii mwenye kofia mbili (intellectual life pamoja na hip hop life) kama vile Nikki wa pili msanii ambaye tunajua fika yuko mbioni kuwa miongozi mwa watanzania wenye kiwango cha juu cha elimu (Phd Holder) kuweza ku balance maisha ya aina zote mbili yaani kuonekana kwenye video za hip hop zenye wanawake waliovaa nusu uchi, wanaume wenye kuvaa kata K na kuonesha kidole cha kati pamoja na kusuka nywele alafu kesho unamuona yupo na intellectuals wengine kama akina Prof. Kabudi and other high profile intellectual figures, wanajadili mambo mazito ya nchi yahusuyo maendeleo ya taifa letu. How's this possible?

Binafsi, simsemi Nikki vibaya, ila ninadhani anahitaji ku sacrifice kimoja wapo.

Aidha aendelee kuwa wana hip hop ama aachane au apunguze swagger za ki hip hop na avae muonekano wa kisomi zaidi kwa maana yeye ni kioo cha jamii sasa.

Simaanishi kuwa anapaswa kuwatenga wavaa kata K kama kaka yake Joe, hapana, ila kuna ulazima wa yeye kuipa hiyo PhD heshima yake.

I STAND TO BE CORRECTED.
 
Ni wapi imeandikwa mtu mwenye PhD aishi vipi? Nafikiri kupitia Niki vijana wengi watajifunza kua na PhD sio kusubiri ajira na teuzi serikalini. Tafuta PhD kuongeza maarifa kwa shughuli yako yoyote unayofanya.
 
Kwani PHD ina ethics zake? Kama hakuna basi ana Uhuru wa kufanya anachotaka.Kiukweli anatamanisha vijana wengi ambao waliona sio rahisi kwa kijana kutunukiwa PHD.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]wewe unaelimu gan kwan aseee??? Na nan kakuambia kuna mavazi ya standard seven na phd. You have to know that mavazi sio big deal ishu ni kwamba kichwan unanini mekuuu [emoji23][emoji23][emoji23].Afu pia i advice you kupunguza ukoloni manake dah wanaoishii na ww wataja kuchoka mzeee
 
Mavazi ya PhD yapoje, bado una mentality ya kumadress mtu kutokana na muonekano wake? Umezaliwakijiji gani?
 
Ni wapi imeandikwa mtu mwenye PhD aishi vipi? Nafikiri kupitia Niki vijana wengi watajifunza kua na PhD sio kusubiri ajira na teuzi serikalini. Tafuta PhD kuongeza maarifa kwa shughuli yako yoyote unayofanya.

Kuna mahali pameandikwa how a PhD holder should behave, labda kwa bahati mbaya hujawahi kupasoma! Kwa kuanzia tu, ungeanza kufahamu lile gauni linalovaliwa wakati wa mahafali lina maana gani, kofia (na zile pembe zake) au kile ki mkia (tassle). Pia hudhuria mahafali mtu anapokuwa anatunukiwa shahada ya Uzamivu (PhD). Mimi huwa naifananisha na ibada ya mageuzo!

Baada ya kufahamu hayo machache, utarudi hapa jukwaani tujadili!
 
Back
Top Bottom