Unaongea kwa mantiki ya mawazo yw Mkoani hukoooo Kigoma au Ruvuma Mkuu. Amini usiamini kwa Daaaslam kuna wadosi wakishanunua gari alipendalo lile la awali analiondoa kwa bei rahiiiiisi mno, shida huwa na madalali tu.
Kwa macho yangu nimeshuhudia Mdau mmoja akiuziwa Toyota Corolla pale Ubungo Plazza kwa Mil.3 na gari ikiwa namba B na Injini safi shida ilikuwa matairi. Hadi sasa gari hilo ni Teksi Mkoani jamaa anaingiza hesabu kila wiki.
Kwahiyo tusimkatishe tamaaa mhitaji wa Gari la 2.5 atapata DUET saafi, au Corolla matata ambayo siyo pasua kichwa.