Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu hajafa bado anaishi ndio maana matunda ya kazi zake yanajidhihirisha hadi leo
Nikola Tesla the Genius of all days; big sana kwa mleta uzi huu nlikuwa nafahamu vichache juu ya mwanafizikia huyu ila kwa thread hii nimegain vingine vingi.
Sikuwahi msikia huyu mtu, asante mtoa mada!!
Kweli mkuu hati miliki ilimcost huyu jamaa, Tunajifunza hapa kama umefanya hadimu jitahidi kuweka hati miliki. Mfano Leo Jamaa wa LG wanaproject ya kudesign a smartphone from camera yenye uwezo wa kupiga selfie eneo kubwa au watu wengi bila ya selfie stick, kwa mfumo huuhuu wa hati miliki nadhani watapata wateja wa technology hiyo karibu makampuni yote ya simu kwa mabilioni ya pesa.
Ila jamaa alikuwa anatamani kutumia muda mwingi sana kufanya ugunduzi na kutaka kazi yake isaidie watu wengi. Unajua kabla ya project ya niagara falls ya kuzalisha umeme, kulikuwa na vita vikali sana kati ya dc na ac ipi itumike kwa umeme wa majumbani.
Upande wa thomas edison ambao ni dc voltage, walikuwa na mkono wa J.P Morgan ambaye alikuwa mwanahisa. Upande wa ac tesla alikuwa na george westinghouse. Hela nyingi sana zilitumika na kila upande mpaka ikataka kupelekea westinghouse kutaka kufilisika. Ndo hapo Tesla ikabidi aseme yeye ataachia hati miliki zake na hata taka malipo(royalt) ya patents zake.
Westinghouse ndo walipoponea na kutengeneza pesa nyingi.
uko vizuri. Kama maabara yake liyokuwa na pepars zaidi ya mamia ya ugunduzi kuungua na vitu vyote vilivyokuwemo kubaki majivu ambayo ikapelekea aanze moja tena, KAribu kila kitu duniani huyu jamaa angekuwa na mkono wake.Tesla alikuwa ni mvumbuzi si mfanya biashara.
Wametengeneza gari sasa hivi za umeme kwa kutumia teknolojia yake ya betri na super charger aliyoivumbuwa miaka mingi sana iliyopita , zinafanya kazi vizuri na zinauzika sana kuliko gari yoyote ya umeme na imepewa jina hilo hilo Tesla:
![]()
Source na soma zaidi: Tesla Motors | Premium Electric Vehicles
uko vizuri. Kama maabara yake liyokuwa na pepars zaidi ya mamia ya ugunduzi kuungua na vitu vyote vilivyokuwemo kubaki majivu ambayo ikapelekea aanze moja tena, KAribu kila kitu duniani huyu jamaa angekuwa na mkono wake.
Nadhani A-level ulikuwa HGL au HGK (Sanaa). Waliosoma Physics A-Level wanamjua,nikiwamo mimi.
Nilisoma EGM mkuu, ila nipo interested sana na hayo mambo najitahidi kujifunza!!
Vizuri havimudu kwakweli, je kuhusu technolojia ya kupaa kwa ndege aeroplane vp kuna mkono wake?
uko vizuri. Kama maabara yake liyokuwa na pepars zaidi ya mamia ya ugunduzi kuungua na vitu vyote vilivyokuwemo kubaki majivu ambayo ikapelekea aanze moja tena, KAribu kila kitu duniani huyu jamaa angekuwa na mkono wake.
Tesla alikuwa kikwazo kwa wafanya biashara wakubwa na wanasayansi wenzake,hivyo walifanya kila mbinu kumtuliza.Hayo mabaya karibu yote yaliyomtokea yalipangwa na wafanyabiashara akiwemo JP.Morgan.
-Tesla alipingana na mwalimu wake kuhusu sayansi ya AC motor,Tesla alikuwa sahihi.
-Tesla alipingana na Edison kuhusu sayansi na faida za AC current,Tesla alishinda.
-Mantiki za Tesla zilipingana na hoja za Albert Eistein kuhusu relativity theory,Tesla alikuwa sahihi.
Tesla alijenga mnara mkubwa sana kwa lengo la kulisha umeme dunia nzima bure,watu wangepata umeme huo kwa njia ya kuukinga na antenna kwenye nyumba zao.JP.Morgan alipomuuliza "unajenga mnara huo kwa lengo gani?",Tesla akasema "nataka kulisha umeme dunia nzima bure bila kutumia wire".JP.Morgan aliposikia hivyo akasimamisha ufadhili wake kwa Tesla na kuachana naye,Tesla akashindwa kuendelea na project hiyo kwa kukosa mfadhili.
Tesla alikuwa mwanasayansi mwenye ethics halisi za sayansi halisi,alikuwa na lengo hasa la kuona watu wanafaidika na kichwa chake.Lakini lengo lake lilitofautiana na mabeberu wa kipindi kile ambao ndio offsprings zao zinashikilia serikali ya Marekani kwa sasa.Na ndio maana project yoyote yenye lengo la kusaidia watu walio wengi bure au kwa gharama nafuu kwa sasa haiwezi kufadhiliwa au kuachwa iendelee.Ukitaka kuamini hili anza kufuatilia taratibu masuala makubwa kwenye AFYA,KILIMO na ELIMU,utaona kuna watu kazi yao ni kuzuia maendeleo katika nyanja hizo.
Kwangu mimi Tesla ndio mwanasayansi bora wa karne yake.Sasa hivi kuna mwanasayansi mmoja muhimu sana na amefanya mambo mazito sana kwenye dunia hii lakini wengi hawamfahamu,huyu jamaa project yake ikikamilika dunia itaandika historia nyingine kabisa na kuweka mambo ya sasa kwenye makabrasha yatakayowekwa kwenye makumbusho kwa ajili ya kufundishia watoto wetu.Huyu anaitwa Jacque Fresco,project yake inaitwa The Venus.
Fuatilia 'The Venus Project' kwenye mitandao/youtube ili ujionee huyu ni mtu wa aina gani.Hapa ndio utaona kwamba sisi tumewekewa vifungo vya akili na mambo fulani katika dunia hii,especially MONEY.
"You should not be at all surprised if someday you see me fly from New York to Colorado Springs in a contrivance which will resemble a gas stove and weigh almost as much." Nikola Tesla, 1913 ALIKUWA ANAZUNGUMZIA HERIKOPTER UNAYOIJUA KWA SASA....
In January 1928, the U.S. Patent Office granted Tesla what would be his final patent, for a novel method of transporting bodies through the air. He described and sketched an open box-type craft with a tilting propeller and wing that theoretically would enable the vehicle to rise vertically and fly horizontally, though he also suggested a design in which two propellers coaxially or otherwise disposed would revolve in opposite directions, powered by his turbine engine....