NIKOLA TESLA: Kwa nini watu kama hawa dunia ni nadra kuwapata?

NIKOLA TESLA: Kwa nini watu kama hawa dunia ni nadra kuwapata?

hivi kuna chanzo chochote kinaweka wazi kuwa mentor wa einstein alikua tesla

Mimi simjui vzuri tesla lakini einstein namjuajua na nimemsoma pia,huyu jamaa alikua noma..kuna wakati ashapewa fursa ya kua rais wa taifa la marekani kipindi hicho lakini akakataa...ni mtu ambaye theory zake mpaka leo wanasayansi bado zinawatatiza

haijalishi nani alikua mentor wa nani
hakuna ukweli katika hili 100% hizi ni story za mitaan
 
hivi kuna chanzo chochote kinaweka wazi kuwa mentor wa einstein alikua tesla

Mimi simjui vzuri tesla lakini einstein namjuajua na nimemsoma pia,huyu jamaa alikua noma..kuna wakati ashapewa fursa ya kua rais wa taifa la marekani kipindi hicho lakini akakataa...ni mtu ambaye theory zake mpaka leo wanasayansi bado zinawatatiza

haijalishi nani alikua mentor wa nani
albert ni zionist moja ya mafounder wa israel na marekani aliishi kama asylum kwa kuwa alikuwa ni most wanted person na wagerman(nazism) baada ya vita kuu ya pili ya dunia so sidhani kama mtu wa sifa hiyo angepewa nafasi ya kuwa raisi wa marekani
 
Naomba niongezee kidogo huyu jamaa Nikola Tesla hakumaliza degree yake ya kwanza ya electrical engineering ila mwaka wa kwanza na wa pili alipiga GPA za hatari , alikuwa mtu wa misuli mirefu anasoma kuanzia saa tisa usiku hadi saa tano usiku mfululizo bila kupumzika lakn alipofika mwaka wa tatu akaanza kubet yaan Gambling matokeo yake akafeli mitihani ya mwaka wa tatu akatimkia kisiwani flan ivi nimekisahau jina hakurud nyumban aliogopa kuchekwa .Baba yake alimtafuta sana mpaka ikafikia hatua akaamini kuwa mwanae alikufa kwa sababu ya kupiga misuli mirefu akamtafuta akampata lakn Tesla aligoma kurud nyumbani dingi alitumia nguvu nyingi sana kumshawish mpaka akakubali aliporud nyumban akaanza kufundisha tuition kitaa cha kwao alikuwa maarufu kichz baadae akapata zali la kupata kazi kwenye branch ya edison yule mgunduz wa umeme wa DC hapo ndo Tesla akapata mwanya wa kutokea alikuwa akifanya kazi kupitiliza hadi akahamishiwa makao makuu ya kampun ya edison then alipofika makao makuu alipiga kazi nying sana edison alimkubali ila alikuwa anadhulum mishahara yake ndo maana Tesla akasepa akagundua umeme wake akauita AC ndo lile battle la AC vs DC likawa kubwa sana ila Edison sio mtu mzuri coz alikuwa akiwaaminisha watu kuwa AC sio umeme mzuri , Tesla alipogundua umeme wa nguvu za maji ndo akaua kabisa ,,, jamaa alikuwa vizuri kichz alipanga kugundua umeme wa wireless sema tu Mungu akamchukua
 
Kwanza asante kwa makala safi kabisa ya kumuenzi huyu jamaa Nikola Tesla, amekuwa Icon kubwa sana ktk ulimwengu wa sayansi bila kusahau huyu ndo mtu wa kwanza kutengeneza transmitter ambayo ilianza kwa kurusha mawimbi kwa umbali wa km 8 ..Tunampa credit British spy marconi kwa invert radio but sio kweli Tesla ndio anastahili Lakini pia tesla alikufa as lonely man yani hakuoa wala kuwa na watoto pia alifukuzwa chuo kikuu graz university


..Jamaa ni genius kweli kweli ila nashindwa kuelewa kwann alikuwa down kiuchumi pia kuandikwa ktk historia anafichwa sana Wakati kazi zake ndo zinaendesha ulimwengu huu mfano yeye ndo wa kwanza kujenga hydro electric power station niagra aka produce ac current aka design transformer na motor za Ac pia

R.I.P Nikola Tesla
Hicho chuo sijui kilijisikiaje baada ya kumfukuza jamaa akaenda fanya maajabu na wao kukosa credits
 
Tunaposema JF ni kitovu cha greatthinkers/intelligent guys kimenifanya kutaka kujifunza Thinkers hawa maisha ya kila siku na jinsi walivyovumbua vitu, kufanya mambo makubwa, kutawala kwa njia za kipekee,

Leo Tumjadili huyu japo kwa kupapasa.


NIKOLA TESLA(10 July 1856 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 7 January 1943)

tesla-productive-virgin-wide.jpg

Nikola-Tesla.jpg

nikola_tesla_vs_thomas_a_edison_2014-08-17.jpg


Alizaliwa ulaya mashariki kwenye nchi ambayo leo ni Croatia/Serbia. Kipindi ambacho kulikuwa na option mbili tu Kujiunga na Jeshi au dini. Baba yake alikuwa ni Mchungaji wa kanisa na mama yake alikuwa mama wa nyumbani. Alilazimishwa kujiunga na kanisa lakini alikataa hakuwa tayari. Mama yake kakuwahi kwenda shule lakini alikuwa na talent ya kushona na uwezo mkubwa wa kukariri mashahiri vitu vilivyomfanya mtoto Tesla kuvutiwa sana.Vitu hivi vilimfanya kuwa na uwezo wa kufanya hesabu ngumu za CALCULUS (watu wahisabati mnanielewa) kwa kichwa kitu kilichowafanya waalimu wahisi anadanganya au kunasehemu anaangalizia.


MAISHA YA AWALI


Akiwa mtoto mdogo aliposoma kuhusu mapolomoko ya niagara marekani kichwani mwake aliona Gurudumu likizunguka katikati ya maji. Kwa immagination na meditation akajakuwa founder wa umeme wa maji miaka mingi baadae alipofika hilo eneo.
Kuna kipindi akiwa chuo alikuwa akisoma kuanzia saa tisa usiku hadi saa tano usiku mfululizo. Hadi siku moja akiwa nyumbani akakuta barua ya siri ya proffesor akimuandikia baba yake wamrudishe nyumbani maana akiendelea atafariki.


KISA CHA KWENDA MAREKANI

akiwa na upenzi wa sayansi alipata kazi katika viwanda. Baadae alienda ujerumani alipopata kazi kisha akaajiriwa na kampuni ya kimarekani ya umeme DC General Electric ya thomas edison founder wa DC current
Waliokuwa na tawi ufaransa. Kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha akapata transfer kwenda makao makuu ya kampuni hiyo Marekani afanyekazi ya kudesidn na pia atakuwa karibu zaidi na edison.
Akaingia Newyork akiwa bado kijana sana.

KUTOKA KUWA MTAALAMU HADI KUCHIMBA MITARO KAMA KIBARUA



Akifanya kazi bila kuchoka, akifanya design, Siku moja bosi wake Edison alimuambia akidesign system ambayo itasaidia kuboresha ufanisi wa mashine zake atapewa dora 50 ambayo ilikuwa pesa nyingi kwa wakati huo. Alipofanikiwa jamaa akamgeuka akamwambia alikuwa anamtania. Jamaa akaamua kuacha kazi hata baada ya kulazimishwa saana. Alichokutana nacho ni maisha magumu kupita kiasi. Ilifika kipindi akawa anachimba mitaro, ili angalau apate pesa ya chakula. Hadi siku moja alipojiuliza kwa nini anafanya kazi za ajabu huku kichwani anaazina ya kutosha.


MVUMBUZI WA AJABU


alikutana na jamaa ambao aliingia nao makubaliano ya wao watamsupport ktk vitu anavyokuwa akivumbua. Uvumbuzi wa DC motor alioufanya na baadae kuwa mshauri kwa kampuni pinzani ya edison. Alijipatia pesa nyingi maana kwa uvumbuzi wake ulilingizia kampuni hilo mamilion ya pesa. Kitu ambacho kilihatarisha uhai wa kampuni yake aliyoacha kazi ya Mr Edson. Alikuwa halali zaidi ya masaa manne.fedha hizo aliziingiza katika utafiti wake huku akiishi hotelini maisha yake yote hadi mauti inamkuta.


VITA VYA UMEME


Wivu wa uvumbuzi wa umeme mbadala wa edison ulimfanya jamaa kutumia fitna kuwatisha watu kua umeme huo ni hatari saana kwa uhai.
Edison alikusanya watu newyork akafanya maonyesho ya hatari. Kuua tembo, nyani kwa umeme wa AC. Watu walijaa hofu. Tesla yeye aliwaita watu waje washuhudie jinsi alivyoweza kuzungusha yai bila kupasuka juu ya sahani kwa kutumia AC motor. Siku Edison aliponyamazishwa rasmi ni pale alipowanyima akina tesla haki ya kutumia Taa zake Za DC siku maalumu ambapo watu walitoka dunia nzima kuja kushuhudia uvumbuzi mwingine wa tesla. Tesla aliishangaza Newyork nzima, usiku ulipofika akiwasha taa zake mwenyewe kwa umeme wake ambao ulifunika jiji zima. Dc bulbs zikaonekana kama koroboi. Mji ukawa kama mchana.


MAAJABU YA KISAYANSI


Aliweza kutengeneza radi hata ndani ya chumba alichokuwa anafanyia utaafiti.
Alijenga mnara kwa mara ya kwanza alitaka umeme uwe wireless. Dunia nzima iwe na umeme bila hata waya.
Alipotengeneza wireless controlled boat waalikwa wa siku ya maonyesho waliona ni uchawi. Wakasema kuna nyani mdogo kamtrain ndio anaendesha baadae wakafungua hawakukuta kitu.
Akasema awauzie jeshi la marekani hiyo technology wakamdharau lkn leo mabomu,drones navitu krbu vyote wireless huwezi kumsahau Tesla. Mnara wa kwanza wa mawasiliano ulijengwa na huyu jamaa japo kwa lengo la kutransmit power alifanikiwa kupokea signal kwa mara ya kwanza zikitokea ulaya. Huku yey na wenzake walidhani zimetoka mbinguni au sayari tofauti.

ANATUFUNDISHA NINI UNAPOTEGEMEA KITU KIKUBWA GHAFLA MKASA WAAJABU UNAKUPATA (usikate tamaa)

Akiwa katikati ya Uvumbuzi na utafiti wa X-RAY(ambayo baadae wakati akiwa na hili tatizo jamaa mwingine akavumbua) katika maabara yake, Hakuamini macho yake kesho yake asubuhi alipokuta maabara yake imeungua na kila kitu kimekuwa ni majivu tu. tesla alipoteza Mamia ya ,
1. Documents za mipango yake,
2. Design zake zote alizokuwa ameziandaa,
3. Notes , invention models
4. Picha zake alizokuwa amejitunzia pamoja na vitu ambayo alikuwa ameviandaa tayari kwa maonyesho.
alipoteza kiila kitu, vitu vyote vilikuwa na thamani zaidi ya $50,000 miaka hiyo. alipoulizwa na gazeti ya New York times kuhusu janga lililompata, kwa huzuni na uchungu alisema, "I am in too much grief to talk, What can I say?". lakini alijikongoja akaanza upya kwa kuwa supported na sponsors waliomuamini na akafanya mambo makubwa zaidi ikiwepo wireless radio wave driven boat.

KUFA MASIKINI HUKU AKIACHA MAMBO YALIYOWAACHA WENGI MABILIONEA

Pamoja na mambo makubwa aliyofanya nikola tesla alikufa akiwa hana kitu. Alifia hotelini alipokuwa akiishi. Kazi kubwa aliyoifanya iliishia kuwafanya kuwa mabilionnaire. Mfano mwanasayansi wa italia Marconi ilipata tenda na patent kutoa huduma ya fax marekani baada ya kumshinda kesi Tesla. Lakini kiukweli karibu kila alichotumia ni ideas za tesla na mfadhili wake morgan akaamua kumuacha na kumsupport Marconi. Vitu karibu vyote alivyovumbua viliishia mikononi mwa wanasayansi makanjanja na kujitajirisha. Tatizo lake hakujielekeza kwenye haki miliki na pia yawezekana wamarekani hawakutaka kumpa umaarufu japo alichukua uraia. Kama angekuwa umiliki wa uvumbuzi wake leo. Angekuwa tajiri namba moja duniani maana krb kila kitu cha sasa anamkono wake.


AMEKUFA LAKINI KAACHA ALAMA ZA KUDUMU DUNIANI IKIWA NI MATUNDA YA MATUMIZI SAHIHI YA UBONGO WAKE.



miaka ya sitini Tesla ilipitishwa kuwa SI unit ya magnetic flux density kumuenzi. Amekuwa kivutio kwa wanasayansi vijana enzi hizo akiwapo Albert Einstain ambaye anamuona kama role model. Baada ya kufa inasemekana makachelo wa marekani waliofika hotelini hapo waliondoka na mavumbuzi mengi yake ya kijeshi ndio maana wako vizuri kivita baada ya kudevelop.
Mfano wanasayansi leo wanafanya utafiti wa kusambaza umeme dunia nzima kupitia anga linaloitwa Ionosphere. Marekani wanafanya research ya kutumia reflecting satelite kupeleka umeme Japan. Zote hizo ni kazi za tesla zilizomfanya akaitwa Mwanasayansi KICHAA.
Baadhi ya vitu vilichukuliwa na ndugu zake zikapelekwa serbia na yawezekana wanasayansi wa urusi walitumia pia kudevelop vitu na silaa. Mitaa, vyuo, mabarabara, vikundi vya wasomi, taasisi za kisayansi vimeitwa kwa jina lake kumuenzi Great thinker huyu katika mambo ya science na technolojia.


Wapenzi wa historia ya great thinkers, wavumbuzi na watu waliopita karibuni.
NIna ''A'' za Engineering Science na Mathematics. Lakini mpaka leo sijui nizielekeze wapi. Elimu yetu ni shida tupu.
 
Naomba niongezee kidogo huyu jamaa Nikola Tesla hakumaliza degree yake ya kwanza ya electrical engineering ila mwaka wa kwanza na wa pili alipiga GPA za hatari , alikuwa mtu wa misuli mirefu anasoma kuanzia saa tisa usiku hadi saa tano usiku mfululizo bila kupumzika lakn alipofika mwaka wa tatu akaanza kubet yaan Gambling matokeo yake akafeli mitihani ya mwaka wa tatu akatimkia kisiwani flan ivi nimekisahau jina hakurud nyumban aliogopa kuchekwa .Baba yake alimtafuta sana mpaka ikafikia hatua akaamini kuwa mwanae alikufa kwa sababu ya kupiga misuli mirefu akamtafuta akampata lakn Tesla aligoma kurud nyumbani dingi alitumia nguvu nyingi sana kumshawish mpaka akakubali aliporud nyumban akaanza kufundisha tuition kitaa cha kwao alikuwa maarufu kichz baadae akapata zali la kupata kazi kwenye branch ya edison yule mgunduz wa umeme wa DC hapo ndo Tesla akapata mwanya wa kutokea alikuwa akifanya kazi kupitiliza hadi akahamishiwa makao makuu ya kampun ya edison then alipofika makao makuu alipiga kazi nying sana edison alimkubali ila alikuwa anadhulum mishahara yake ndo maana Tesla akasepa akagundua umeme wake akauita AC ndo lile battle la AC vs DC likawa kubwa sana ila Edison sio mtu mzuri coz alikuwa akiwaaminisha watu kuwa AC sio umeme mzuri , Tesla alipogundua umeme wa nguvu za maji ndo akaua kabisa ,,, jamaa alikuwa vizuri kichz alipanga kugundua umeme wa wireless sema tu Mungu akamchukua
Hiyi inaitwa ...struggle for ''A'' ili uwe mtumishi wa ''C''.
 
kwa point ya hapo chini, Tesla hakuhitaji mathematical formulas kuvumbua vitu kama akina Einstain ambaye formula yake ilitengeneza bomu la atomic liliouwa wajapani, jamaa alifikiri na kufanya majaribio na kuwaacha watu midomo wazi.

mfano alipotengeneza vibrating electric shock ambayo ilitetemesha ghorofa zima ilasababisha police na zima moto wajaea lakini kumbe ni tesla alikuwa kazini.

Baada ya hapo alisema anaweza tengeneza low friquency electric vibrator ambayo ikifungwa madarasani na watu wanapokuwa wanasoma hiyo vibration inaweza kustimulate ubongo na hata kama ni kilaza kiasi gani lazima akili zichaji.
Jamaa hawakumtilia maani lkn angeweza,
Hiyo ingekuwa moja ya project muhim sana. Ku stimulate bongo za wanafunzi. Ingekuwa inasaidia sana
 
Back
Top Bottom