Tesla alikuwa kikwazo kwa wafanya biashara wakubwa na wanasayansi wenzake,hivyo walifanya kila mbinu kumtuliza.Hayo mabaya karibu yote yaliyomtokea yalipangwa na wafanyabiashara akiwemo JP.Morgan.
-Tesla alipingana na mwalimu wake kuhusu sayansi ya AC motor,Tesla alikuwa sahihi.
-Tesla alipingana na Edison kuhusu sayansi na faida za AC current,Tesla alishinda.
-Mantiki za Tesla zilipingana na hoja za Albert Eistein kuhusu relativity theory,Tesla alikuwa sahihi.
Tesla alijenga mnara mkubwa sana kwa lengo la kulisha umeme dunia nzima bure,watu wangepata umeme huo kwa njia ya kuukinga na antenna kwenye nyumba zao.JP.Morgan alipomuuliza "unajenga mnara huo kwa lengo gani?",Tesla akasema "nataka kulisha umeme dunia nzima bure bila kutumia wire".JP.Morgan aliposikia hivyo akasimamisha ufadhili wake kwa Tesla na kuachana naye,Tesla akashindwa kuendelea na project hiyo kwa kukosa mfadhili.
Tesla alikuwa mwanasayansi mwenye ethics halisi za sayansi halisi,alikuwa na lengo hasa la kuona watu wanafaidika na kichwa chake.Lakini lengo lake lilitofautiana na mabeberu wa kipindi kile ambao ndio offsprings zao zinashikilia serikali ya Marekani kwa sasa.Na ndio maana project yoyote yenye lengo la kusaidia watu walio wengi bure au kwa gharama nafuu kwa sasa haiwezi kufadhiliwa au kuachwa iendelee.Ukitaka kuamini hili anza kufuatilia taratibu masuala makubwa kwenye AFYA,KILIMO na ELIMU,utaona kuna watu kazi yao ni kuzuia maendeleo katika nyanja hizo.
Kwangu mimi Tesla ndio mwanasayansi bora wa karne yake.Sasa hivi kuna mwanasayansi mmoja muhimu sana na amefanya mambo mazito sana kwenye dunia hii lakini wengi hawamfahamu,huyu jamaa project yake ikikamilika dunia itaandika historia nyingine kabisa na kuweka mambo ya sasa kwenye makabrasha yatakayowekwa kwenye makumbusho kwa ajili ya kufundishia watoto wetu.Huyu anaitwa Jacque Fresco,project yake inaitwa The Venus.
Fuatilia 'The Venus Project' kwenye mitandao/youtube ili ujionee huyu ni mtu wa aina gani.Hapa ndio utaona kwamba sisi tumewekewa vifungo vya akili na mambo fulani katika dunia hii,espe
jamaa amesha fariki mwaka huu R.I.P Jacque Fresco