Nile chakula gani tofauti na wali na ugali kwa muda wa wiki mbili mfulizo?

Mr Q

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
18,046
Reaction score
38,598
Wana jukwa salaam kwenu.

Imekuwa kawaida kwangu Mimi kula ugali na wali kama Chakula kikuu siku hadi siku. Sasa nimepata wazo la kuviweka kando kwa siku 14 bila kuvigusa

Hivyo naomba mniambie kwa hapa kwetu Tanzania ni Chakula gani mbadala naweza kutumia kwa hizo siku 14 na mwili ukabaki na nguvu zake zile zile
1.Jumapili
2.Jumatatu
3.Jumanne
4.Jumatano
5.Alhamisi
6.Ijumaa
7.Jumamosi
8.Jumapili

Natanguliza shukrani za dhati
 
hivyo naomba mniambie kwa hapa kwetu Tanzania ni Chakula gani mbadala naweza kutumia kwa hizo siku 14 na mwili ukabaki na nguvu zake zile zile!
1.Jumapili
2.Jumatatu
3.Jumanne
4.Jumatano
5.Alhamisi
6.Ijumaa
7.Jumamosi
8.Jumapili
.
.
.
Natanguliza shukrani za dhati
Mkuu swali gani hilo, vyakula vyote vimejaa masokoni wewe una waza wali na ugali tu, acha mazoea ya hovyo. Mimi mwenyewe huwa sili hivyo vitu kila siku.
Haya jichagulie.
Magimbi
Tambi
Mihogo.
Ndizi Bokoboko.
Sheli sheli.
Ndizi mshale, malindi nk.
Mahindi mabichi unatengeneza makande.
Matunda ya kila aina.
Ngano mbegu.
Ngano unga, ie, chapati, mandazi, mikate nk
Mahindi ya kuchemsha.
Hapo unajumlisha na mboga za aina mbali mbali na samaki
 
Ufafanuzi hapo shelisheli na ngano mbegu

Vinginevyo ahsante kwa orodha hii
 
Mkuu ngano mbegu, kama ilivyo hapo, unaipika kama kande, ni nzuri sana, unaweza kuipika na maharage au chochote, na ni nzuri kwa afya. Ngano mbegu inapatikana masokoni, masoko ya nafaka. Sheli sheli ni tunda, linapatikana juu ya mti, linapikwa na kuwa kama kiazi, ni nzuri kwa afya pia hupatikana kwa msimu masokoni.
 
Wana jukwa salaam kwenu.

Imekuwa kawaida kwangu Mimi kula ugali na wali kama Chakula kikuu siku hadi siku. Sasa nimepata wazo la kuviweka kando kwa siku 14 bila kuvigusa

Hivyo naomba mniambie kwa hapa kwetu Tanzania ni Chakula gani mbadala naweza kutumia kwa hizo siku 14 na mwili ukabaki na nguvu zake zile zile
1.Jumapili
2.Jumatatu
3.Jumanne
4.Jumatano
5.Alhamisi
6.Ijumaa
7.Jumamosi
8.Jumapili
.
.
.
Natanguliza shukrani za dhati
Jumapili maboga na samaki, mboga za majani
Jumatatu tambi, nyama, mayai,
Jumanne magimbi, mishikaki,
Jumatano mihogo, dagaa, njegere au maharage
Alhamisi ndizi nyama, utumbo,
Ijumaa kitimoto choma, roast na chips,
Jumamosi samaki , kuku na chapati , sambusa,

Vyakula ni vingi tu unaweza hata kukaa mwaka bila kula vitu hivyo

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Asante kwa ushauri wako mkuu. Na kwakweli ukifanikiwa hapo hadi mwisho wa wiki utafeel mabadiliko kwenye tumbo lako
 
Sana mi nimekuwa nikifanya hivi sana tu na kiukweli mafanikio yamekuwa makubwa hata mwili umepungua sana
Ila mi nimeachana kabisa na wanga kwa kipindi kirefu tu, nakula mara chache mno

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
wali na ugali ni vyakula vigumu sana ukila unaweza kupiga ndefuu bila njaa tofauti na vyakula vingine km hayo ndiz na mabokoboko..vyakula hvyo simpo ukiacha ugali na wali utakula sawa ila haipiti mda mrefu unaskia njaa tena!utajikuta unakula ula ovyo badala ubane matumiz ndio unazidisha
 
😁😁😁 sawa mkuu nakuelewa naona hoja yako imejikita zaidi kwenye bajeti. Sawa hilo nalo ni lakuzingatia
 
Sana mi nimekuwa nikifanya hivi sana tu na kiukweli mafanikio yamekuwa makubwa hata mwili umepungua sana
Ila mi nimeachana kabisa na wanga kwa kipindi kirefu tu, nakula mara chache mno

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Mbona naona Menu yako hapo juu imejaa wanga tupu kuanzia jtatu to Jpili..!??

Mihogo,Ndizi,Magimbi,Tambi si bado wanga tu!??au umepunguza ulaji tu rafiki
 
Ni ngumu sana kuota kitambi uzembe ukifuruliza unakula ndizi kuliko ukifuruliza ulapo ugali. Japo vyote vinazalisha nutrients ambazo zawezakuwa zinafanana.
 
Hivyo nimemtajia yeye ambae hataki wali na ugali

Mi nilipokuwa najipunguza milikuwa nakula mayai, nyama (hadi kitimoto)
Maziwa ya aina zote (full cream milk)
Mboga za majani
Matunda nilikuwa nakula matango na maparachichi
Na nilikuwa nakula mboga zote za majani pamoja na kabichi
Ila nilikuwa nakula pia maharage na wali hii japo mara moja kwa miezi kama mitatu, hii nilishindwa kuacha kabisa sababu napenda mno na nilipunguza sana alcohol nilikuwa nakunywa red wine tu tena weekends na sio zote
Na nilipungua toka 89kg mpaka 64kg
Sasa hivi nimeongezeka kidogo nna 68 ila nataka nirudi 64kg mpaka kufika october mwaka huu

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Ni ngumu sana kuota kitambi uzembe ukifuruliza unakula ndizi kuliko ukifuruliza ulapo ugali. Japo vyote vinazalisha nutrients ambazo zawezakuwa zinafanana.
Ni kweli,Ila pia hata ulaji uliopitiliza wa kitimoto na nyama halafu ukiwa unapiga na kilevi kitambi nacho kitakuja tu
 
Back
Top Bottom