Niliacha kumuunga mkono magufuli na kujitenga na CCM baada ya jaribio na kumuua Tundu Lissu

Niliacha kumuunga mkono magufuli na kujitenga na CCM baada ya jaribio na kumuua Tundu Lissu

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Amani iwe nanyi wanabodi.

Mwaka huu naenda kutimiza miaka 10 ya membership kwenye jukwaa hili kwa Id hii. Hata hivyo, kwa ujumla nina miaka mingine 4 nyuma ya 2015 ya membership nikiwa na id nyingine ambayo kwa sasa siitumii.

Mimi ni mwanachama wa CHAMA CHA MAPINDUZI ninayependa Demokrasia, Utawala Bora, Haki na maendeleo ya kweli.

Mwaka 2017 nilifanya u turn kubwa sana humu jamvini ya kuanza kupinga utawala wa Magufuli na watu wake kutokana na ukiukwaji mkubwa wa Katiba, Haki na misingi ya Utawala Bora. Hii ilitokana na jaribio na Magufuli na Utawala wake kutaka kumuua Mwanasiasa ninayemkubali zaidi nchini Tundu Antipass Lissu.

Siasa za hovyo za chama changu cha Mapinduzi zilizidi kunifanya nijiweke kando na chama hicho hasa baada ya kuzidi kuendekeza ujinga na uchawa katika kipindi ambacho nchi inatakiwa ifanye mambo makubwa kwa mustakabali wa maendeleo yetu watanzania.

Alipokuja Rais Samia nae nilianza kumuunga mkono ila alivyoanza kubadilika hasa kusigina misingi ya utawala bora na Katiba nae akaanza kunikera.

Ingawa hadi sasa sina shida kubwa na Samia kama Samia ila nina shida kubwa na CCM.

Nakiona Chama cha Mapinduzi kama chama ambacho kilishafika ukomo katika kuwa na fikra sahihi za maendeleo ya nchi yetu na wananchi wake. Nakiona Chama hiki kama kikwazo cha nchi kupata Katiba nzuri na Bora ambayo itahakikisha ustawi wa wananchi na jamii yetu kwa miaka mingi ijayo.

Niseme ukweli. Kwangu hakuna mwanasiasa wa kipekee nchi hii kama Tundu Antipass Lissu. Ni maombi yangu siku moja aje kuwa Rais wa JMT.

Sijutii kumuunga mkono mtu huyu. Na kamwe sitojutia. Ni mwanasiasa anayehitahika sana kwa nchi zetu za Afrika.

Mungu mbariki Tundu Antipass Lissu.
 
Unajua mtu kulengwa risasi 32, halafu utoke salama kwenye hiyo attempt sio jambo la kawaida. Mungu ana mpango mwema na TUNDU LISSU na Tanzania yetu. Mungu atujalie kufika huko salama.
 
Unajua mtu kulengwa risasi 32, halafu utoke salama kwenye hiyo attempt sio jambo la kawaida. Mungu ana mpango mwema na TUNDU LISSU na Tanzania yetu. Mungu atujalie kufika huko salama.
Hadi sasa naamini Lissu ni mpango wa Mungu kwa Tanzania.

Kila siku nikimsikiliza nasema sentence moja tu! Mungu wafanye watanzania wamchague huyu mtu.

Tanzania tuna nafasi ya kuwa nchi ya kipekee sana kwa Afrika na Duniani kimaendeleo na kiuchumi ila CCM ni kikwazo kikubwa sana kufikia hiyo ndoto.
 
Ila UKATETEA UHUNI WA DP WORLD?
Hadi sasa niko tayari kuwajibika kutetea uwekezaji kwenye Bandari zetu ukiwemo wa DP World.

Kwa exposure yangu, lile ni jambo sahihi ambalo nitaliunga mkono hadi siku ya mwisho.
 
Back
Top Bottom