Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
Kutaka kuonekana pesa sio shida zake !!Anaagizaje chakula kabla hajajui gharama zake cha ajabu anakimbia asa anakimbia nini?
Chanzo cha tatizo ni nani?
Mikipo ya mtandaoni inaokoa jahazi mara nyingiNilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.
Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.
Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.
Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.
Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.
Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare wote…yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.
Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.
…..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa
chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5
kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.
Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.
Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…
Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.
Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.
Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.
basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.
Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂
Matajiri msiombe , ila wenye vipato vya kawaida lazima tujue tunatumia kiasi gani!Asa unaombaje menu akati ummewatoa watu out ..
Ingekuwa bonge la aibu, hao watoto mpaka utu uzima wao wangekuwa wanakumbuka icho kituko cha mjomba waoHapo ulitakiwa uondoke kama upo wale watoto ndo dhamana yako wahudumu wakiwaona wanajua upo around, bahati nzuri mabasi siku hizi yapo hadi usiku, zile nguo ulizoacha kwa shemeji yako unaachana nazo.
Unapanda katarama lux ukifika manyoni ndo unampigia simu dada yako unamwambia akafate watoto wake huko ulipowaacha.
Ni bora aibu ya kuwakimbia kuliko aibu ya kuosha vyomo na kufanya usafi compound nzima mbele yao kwa kushindwa kulipa laki mbiliIngekuwa bonge la aibu, hao watoto mpaka utu uzima wao wangekuwa wanakumbuka icho kituko cha mjomba wao
Ulishangaa mbona wakarimu mno kuliko sehem zingine 😂kuna siku moja niliingia saluni mwanza hakika sikumbuki mtaa….tulikua huku kwenye harusi ya jamaa yangu,huwa sipendi kufanya mambo kwa mkumbo…huwa natamani kufanya mwenyewe tena kwa kujaribu vitu vipya….
ila nakumbuka niliingia kwanza saluni eti ina sehemu ya reception…mimi hapo hata akili hainichezi machale…saluni gani ina reception bhana😀
mara yule muhudumu kaniandikisha jina na vitu nimeingia navyo…kavaa khanga tu,mi hapo mawazo hata hayapo hapo…anachekacheka kama vile kanipenda na mii nikawa naongeza confidence.
akanipeleka huko kwa kunyoa kwanza….tulitembea kama vyumba vitano mbele,yaani wale jamaa niligundua ile berbershop wamekodi floor nzima ya ghorofa….kila kitu kinafanyiwa chumba chake…
mimi kwenye kunyoa huko kwanza nashangaa wananihudumia watu watatu tofauti
alianza dada akanivalisha ile kitambaa na kunichana nywele….akaja jamaa alaninyoa halafu akamaliza jamaa mwingine wa kuchonga pamoja na ndevu…..akaja dada yule wa reception mwingine akanihamisha chumba….huko nilikuta wadada tu wamekaa kwenye makochi na kila mtu kavaa nusu utupu….akamkabidhi mmoja aanze sasa niosha…alisema unafanya scrub au steamer…nikasema steamer…yaani hapo anauliza anakupapasa shingoni,basi akaanza puliza ule mvuke…nilikaa pale karibia dakika 45 ananihudumia mimi tu…sasa hapa ndio machale yakaanza kunicheza,hawa mbona wakarimu hivi hawaa
sasa baada ya hapo wakasema kucha nazo zifanyiwe marekebisho pamoja na massage ya kichwa na shingo….mimi haya yote najua ni bonus…
tukamaliza zoezi ndio wakampigia yule dada wa reception…akaja.
aisee bili ananisomea inakuja 72,000/=🥹🥹🥹🥹….aibu ndio sipendi,kwa confidence ile ile nikazama mfukoni nikatoa 75,000/=….sema walinigundua chuplichupli nadhani nilivyoshindwa kujizuia kudai 3000/= ndio mmoja akauliza kwani kaka wewe wa wapi…..
ile natoka ndio nakumbuka kusoma bango….ni hasfi sijui ile mule wanaenda waliopata zao mawe ya madini…
lakini ni kujikaza tu *****….kupendeza nilipendeza sana harusini.
Hii ya kuosha vyombo ndio funga kazi 😂Ni bora aibu ya kuwakimbia kuliko aibu ya kuosha vyomo na kufanya usafi compound nzima mbele yao kwa kushindwa kulipa laki mbili
Dah mimejisikia vibaya sana kusoma hii comment....Pole sana jamani.. juzi nilikua nimekaa kwenye kijiwe flan
ikaingia familia ya baba mama na watoto kama watatu.. watoto wapo very excited.. menu ilivyoletwa nikaona baba na mama wametizamana, watoto wakaanza kuchagua chakula,
Maskin baba akawanyanyua haooo wakaondoka🙌
Ile scene imeniongezea morali ya kusaka hela aisee.. kuna experience inafaa tuwape watoto wetu before waje wapewe na walimwengu.
2025 Mungu awasaidie wote Muingie sehemu mlidhani ni za hadhi ya juu zaidi yenu na ziwe kawaida tu kwenu.
😂😂😂😂 Sema WAJOMBA watakukumbuka ndugu yetu wala usiwazeeNilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.
Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.
Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.
Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.
Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.
Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare wote…yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.
Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.
…..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa
chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5
kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.
Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.
Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…
Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.
Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.
Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.
basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.
Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂
Unajua kuna watu wanahisi hizi ni habari za kutunga….lakini wanasahau kwamba haya ni matukio ya kawaida sana kutokea.Dah mimejisikia vibaya sana kusoma hii comment....
Nina mpango wa kufungua uzi kama series ya story zangu za maisha,fupi fupi ila zinaweza funza sana watu na kuchekesha.
unganisha hapa hapa