Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

Hotel zenye bei utazijua kwa muonekano tu

Watu wanazigharamia kwa hiyo bei lazima ziwe juu

Zipo hotel nzuri na za bei kubwa Dar hiyo hela tulikula watu wawili tu Cape Town fish market kama sijakosea jina

Ila kama huna cash ya maana na kadi juu wala usihangaike
 
Shemeji yako akija kwenu anaweza kuwatoa out nyie? Au atajifanya kila kitu hatumii kuanzia bia nk nakujifanya busy na watu wengi wa kutembelea, usirudie tena kujipendekeza.
 
Nilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.

Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.

Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.

Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.

Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.

Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare wote…yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.

Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.

…..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa

chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5

kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.

Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.

Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…

Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.

Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.

Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.

basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.

Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂
Mikipo ya mtandaoni inaokoa jahazi mara nyingi
 
Hapo ulitakiwa uondoke kama upo wale watoto ndo dhamana yako wahudumu wakiwaona wanajua upo around, bahati nzuri mabasi siku hizi yapo hadi usiku, zile nguo ulizoacha kwa shemeji yako unaachana nazo.

Unapanda katarama lux ukifika manyoni ndo unampigia simu dada yako unamwambia akafate watoto wake huko ulipowaacha.
Ingekuwa bonge la aibu, hao watoto mpaka utu uzima wao wangekuwa wanakumbuka icho kituko cha mjomba wao
 
Aisee ukiwa na tupesa kidogo unaweza pata jeuri kumbe we ni pimbi tu mbele ya wenye nazo. Tatizo hapo lilianzia kwa wewe kuamini una laki moja mfukoni na ukaamini ni kubwa ukadharau hata kufata procedure za siku zote. Pole mkuu.
 
kuna siku moja niliingia saluni mwanza hakika sikumbuki mtaa….tulikua huku kwenye harusi ya jamaa yangu,huwa sipendi kufanya mambo kwa mkumbo…huwa natamani kufanya mwenyewe tena kwa kujaribu vitu vipya….

ila nakumbuka niliingia kwanza saluni eti ina sehemu ya reception…mimi hapo hata akili hainichezi machale…saluni gani ina reception bhana😀

mara yule muhudumu kaniandikisha jina na vitu nimeingia navyo…kavaa khanga tu,mi hapo mawazo hata hayapo hapo…anachekacheka kama vile kanipenda na mii nikawa naongeza confidence.

akanipeleka huko kwa kunyoa kwanza….tulitembea kama vyumba vitano mbele,yaani wale jamaa niligundua ile berbershop wamekodi floor nzima ya ghorofa….kila kitu kinafanyiwa chumba chake…

mimi kwenye kunyoa huko kwanza nashangaa wananihudumia watu watatu tofauti

alianza dada akanivalisha ile kitambaa na kunichana nywele….akaja jamaa alaninyoa halafu akamaliza jamaa mwingine wa kuchonga pamoja na ndevu…..akaja dada yule wa reception mwingine akanihamisha chumba….huko nilikuta wadada tu wamekaa kwenye makochi na kila mtu kavaa nusu utupu….akamkabidhi mmoja aanze sasa niosha…alisema unafanya scrub au steamer…nikasema steamer…yaani hapo anauliza anakupapasa shingoni,basi akaanza puliza ule mvuke…nilikaa pale karibia dakika 45 ananihudumia mimi tu…sasa hapa ndio machale yakaanza kunicheza,hawa mbona wakarimu hivi hawaa

sasa baada ya hapo wakasema kucha nazo zifanyiwe marekebisho pamoja na massage ya kichwa na shingo….mimi haya yote najua ni bonus…

tukamaliza zoezi ndio wakampigia yule dada wa reception…akaja.

aisee bili ananisomea inakuja 72,000/=🥹🥹🥹🥹….aibu ndio sipendi,kwa confidence ile ile nikazama mfukoni nikatoa 75,000/=….sema walinigundua chuplichupli nadhani nilivyoshindwa kujizuia kudai 3000/= ndio mmoja akauliza kwani kaka wewe wa wapi…..

ile natoka ndio nakumbuka kusoma bango….ni hasfi sijui ile mule wanaenda waliopata zao mawe ya madini…

lakini ni kujikaza tu *****….kupendeza nilipendeza sana harusini.
Ulishangaa mbona wakarimu mno kuliko sehem zingine 😂
 
Pole sana jamani.. juzi nilikua nimekaa kwenye kijiwe flan
ikaingia familia ya baba mama na watoto kama watatu.. watoto wapo very excited.. menu ilivyoletwa nikaona baba na mama wametizamana, watoto wakaanza kuchagua chakula,
Maskin baba akawanyanyua haooo wakaondoka🙌
Ile scene imeniongezea morali ya kusaka hela aisee.. kuna experience inafaa tuwape watoto wetu before waje wapewe na walimwengu.

2025 Mungu awasaidie wote Muingie sehemu mlidhani ni za hadhi ya juu zaidi yenu na ziwe kawaida tu kwenu.
Dah mimejisikia vibaya sana kusoma hii comment....
 
Nilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.

Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.

Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.

Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.

Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.

Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare wote…yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.

Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.

…..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa

chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5

kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.

Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.

Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…

Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.

Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.

Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.

basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.

Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂
😂😂😂😂 Sema WAJOMBA watakukumbuka ndugu yetu wala usiwazee
 
Dah mimejisikia vibaya sana kusoma hii comment....
Unajua kuna watu wanahisi hizi ni habari za kutunga….lakini wanasahau kwamba haya ni matukio ya kawaida sana kutokea.

tunatofautiana tu uwezo kwa kushare katika lugha ambayo mwingine ataelewa,lakini wengine wanaona vichekesho…wala siyo vibaya,kikubwa ni kujifunza

mimi sijashare hii habari ili nilalamike,hata kidogo…nishapigwa na matukio mengi makubwa kuliko hata haya na maisha yanaenda vizuri kabisa.

somo ni kwamba tutafute pesa…kumbe bado hazitoshi.
 
Mimi juzi hapa tarehe 25 siku ya Christmas mida ya usiku jamaa yangu akaniambia tutoke out viwanja Usiku. Mda huo nilikuwa nishashiba vya kutosha nikasema hata nikienda viwanja sitaki nitumie zaidi ya elfu kumi. Basi tumeenda club moja kiingilio ilikuwa ni 5000,kila mtu akilipia Kiingilio chake,baada ya hapo nikaagiza KVANT ndogo nikaanza kupiga polepole huku nikiangalia watoto waziri wanavyo zungusha viuno.
Ilifika mda vibe likapanda nikasema nalala huko huko nakesha mpka asubuhi ndo niondoke,, ghafla dada zake na jamaa yangu wakaja pale club,wakaanza kucheza pale mezani kwetu,mda huo Niko tungi Sina hili Wala lile jamaa yangu akaniambia dada zake wanataka waondoke warudi nyumbani kwamba wechoka,,mm nikamwambia wao waende jamaa akaanza ku force kuwa hawezi kuenda akaniacha ikabidi nikubali tusepe,kufikia nje pale jamaa kuongea na dereva taksi akaambiwa wote kutubeba watano ni 15,000 huku ni sehemu ya Karibu sana,,basi nikapanda,tumefika mwisho madem wameshuka jamaa ananiambia Hana hela ya kulipa nimkope atanirudishia,duhhh iliniuma Sana Ila nikampatia,,Cha kishangaza mpka Leo hajanipa hio hela dahh iliniuma Sana aisee ile hela maana nilitaka kesho yake niende kwa dem wangu nimpe anunue kuku tu enjoy.
 
Yule dem alikuwa anameza savannah kama maji, aligaiza six pack ikaisha, akaagiza ya pili akanywa tano, moja akabeba,,,, plus kuku akala,,, weka na bia zangu na msosi bili ilisoma around 140k, mm mfukoni nilikuwa na 87k tu ,,,, ! ! Unaumbuka mchana kweupe, sim banking ilinisaidia !! Na sikumla, nilikuja kumla a year later, nilihama ule mkoa kikazi !
 
Mimi juzi hapa tarehe 25 siku ya Christmas mida ya usiku jamaa yangu akaniambia tutoke out viwanja Usiku. Mda huo nilikuwa nishashiba vya kutosha nikasema hata nikienda viwanja sitaki nitumie zaidi ya elfu kumi. Basi tumeenda club moja kiingilio ilikuwa ni 5000,kila mtu akalipa Kiingilio chake,baada ya hapo nikaagiza KVANT ndogo nikaanza kupiga polepole huku nikiangalia watoto wazuri wanavyo zungusha viuno.
Ilifika mda vibe likapanda nikasema nalala huko huko nakesha mpka asubuhi ndo niondoke,, ghafla dada zake na jamaa yangu wakaja pale club,wakaanza kucheza pale mezani kwetu,mda huo Niko tungi Sina hili Wala lile jamaa yangu akaniambia dada zake wanataka waondoke warudi nyumbani kwamba wamechoka,,mm nikamwambia wao waende jamaa akaanza ku force kuwa hawezi kuenda akaniacha ikabidi nikubali tusepe,kufika nje pale jamaa akaongea na dereva taksi akaambiwa wote kutubeba watano ni 15,000 huku ni sehemu ya Karibu sana,,basi nikapanda,tumefika mwisho madem wameshuka jamaa ananiambia Hana hela ya kulipa nimkope atanirudishia,duhhh iliniuma Sana Ila nikampatia,,Cha kishangaza mpka Leo hajanipa hio hela dahh iliniuma Sana aisee ile hela maana nilitaka kesho yake niende kwa dem wangu nimpe anunue kuku tu enjoy.
 
Back
Top Bottom