Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

Mkuu siku zngne uliwa na mob ya watu kama hivo usithubutu kwenda sehem kila mmoja akaaagiza vyakwake utafilisika kweupe ujanja agiza kisinia hata cha 80-100k na vinjwaji tena soda au ungechukua pizza 2 chips 2 na kuku mzima umalize kazi na soda zenu bc
 
We umeenda sehemu iko ufukweni na laki 1 huku ukiwa na nyomi la vijana😁!? Bahati yako tu tajiri alifanya miujiza.

Siku nyingine usirudie kushobokea viwanja vya ufukweni kama huna walau million 1 kwenye account.
 
Kitu cha kwanza ukifika mahali , omba menu au kama hamna uliza bei kwa wahudumu !
Yaan mimi bora mnione bahiri ila ni muhimu sana !!
Unaweza umbuka vibaya sana !
Yaani hilo muhimu sana. Hapo ukiona bei km huiwezi ama unasepa zako au unanunua Chakula kdg. Hapo hio sahani ya elfi 6 wangekula mtu mbili dadeki 😅😅😅
 
Mkuu Nimecheka kwamba kuna mmoja kiherehere aliagiza pizza. Mimi kipindi nipo chuo weekend na mama watoto tumeingia supermarket tunafanya shopping sasa kuna shelf la wine tukafika sasa ile nachukua chupa ya wine lahaula upande wa shelf wote upo chini wine kadhaa zimepasuka walinifwata spidi kama mama anavyosikia kishindo alafu mtoto wake Akalia huko nje. Wakawa wanafoka kweli kwa hasira nikasema nipeni bill nitalipia. Nakumbuka mmoja akaniambia utaweza wife akamjibu Unatuchukulia kama wewe mfanyakazi supermaket. Wakatupa bill inasoma 645000/-. Uzuri pembeni kulikuwa na ATM ya NBC wife akaenda kutoa maana mfukon nilikuwa na 180000/- Tukawalipa Tukawafyonza Tukaondoka Zetu Ila ile pesa inaniuma mpaka Leo nadhan lile shelf walikuwa wamelitegesha sikuapply nguvu kubwa kuchukua chupa ya wine kiasi cha kuuangusha ule upande wa shelf
 
Niliwahi kunywa chai ya 25,000/= nashela hotel Morogoro.

Chai yenyewe Sasa:-
1. Kipande Cha kiazi Cha kienyeji kimoja.
2. Kikombe kidogo Cha Maziwa mixer kahawa.
3. Yai moja lililokaangwa
4. Slices mbili za mkate
Bia moja 5000/=

Jumla fasta tu 50,000/=
 
Daah hii inauma yaani kumlipia mkaburu ha Mi mwenyewe juzi shangazi na Dada wamekuja kutembelea na watoto kibao wakawa wanasema eti mjomba wao awatoe out awapeleke campsite wakanywe hata soda na chips nikachenga chenga nikamwambia sister chukua 30k inawatosha Hawa alafu mi nikasepa masuala ya kuanza kusumbua watu hapana asee
 
Tulawalipa tukawafyonza tukaondoka zetu 😀😀
 
Mama mtu hapendi aibu ndogo ndogo mkuu 🤣🤣 ila salute sana huyo ndo mke sasa anapangua mashambulizi mtaenda mkajadili wenyewe ndani !!

Mwingine angejificha nyuma yako tu anaangalia.
 
Mimi mtu akileta mada tatamishi kwanza ukimbilia kuangalia "avatar" yake maana inabeba taswira ya muhusika! Hiyo avatar inaonyesha hukukosea kujiingiza katika maamuzi yatakayokugharimu! Pole!
 
Hiyo akili kubwa
 
Mafundi gareji wanafikiri kumiliki gari ni utajiri. Nilienda gereji nikamueleza tatizo akasema andaa kama 60,000. Nikasema fanya kazi. Wakafungua kwenye miguu baadaye anasema wamekuta matatizo mengine. Jumla ikaja 380,000. Ilikuwa balaa. Kuacha gari gereji siwezi maana wizi mwingi. Mpangaji akaniokoa. kodi ilikuwa inaisha siku hiyo, kumpigia akatuma muamala chap😃. Nikalipa na kusepa. Sijarudi gereji hiyo tena.
 
Kuna sehemu wana menu za hovyo. Msosi wenyewe sio mzuri, hio bei yake sasa
 
Ungempigia mkaza dadako (shem) akupunguzie maumivu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…