Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

Aaha juzi kati kimenikutaa kitu nimebeba kalaki kangu nikafanye service aisee Si fundi akasema afanye ni Gear box nikakubali kamaliza kila kitu bill inasoma 230k mafundi usiwazikilize hata siku moja fanya marekebisho ya kitu ulichoenda kufanya sepa.
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
wife umepata wa kufanana naye
 
Bujumbura city center Havana lounge....nimekuja booke hazishiki bia flan Kama gines light...nkaagiza short za godons 3 wewe naona watu wannishangaaa nikasema labda wanamuona nakula ngumu sana...nkaletewa bili short moja faranga 7000...khaaa nikasema godons hii hii au henes sikuwa mnyonge nkalipa..Ila toka hapo kila nikitaka kuagiza foreign beer au gin lazima niulize Bei.... Wakati huo haba bongo short za godons NI 2000 au 1500
 
Qappp
Nadhani wahudumu saazingine hutengeneza bei za maghumashi kwa kutumia udhaifu wa mteja kufakamia bidhaa bila kuuliza bei.
 
Nshawah zungumza na mtu as per your comment anasema lack of exposure nikamwambia sawa.....

Lakini soda hii ya 600 ni elfu nne sijui, it's ok hata kama ni advanced basi waone namna nzuri ya kueka bei

Au msosi.... Nikamwambia siwezi toa 30k kununua kuku ambaye siku Kuna kuku point Hawa wanachomwa vizuri kwa bei simple unaridhika!
 
kuna siku moja niliingia saluni mwanza hakika sikumbuki mtaa….tulikua huku kwenye harusi ya jamaa yangu,huwa sipendi kufanya mambo kwa mkumbo…huwa natamani kufanya mwenyewe tena kwa kujaribu vitu vipya….

ila nakumbuka niliingia kwanza saluni eti ina sehemu ya reception…mimi hapo hata akili hainichezi machale…saluni gani ina reception bhana😀

mara yule muhudumu kaniandikisha jina na vitu nimeingia navyo…kavaa khanga tu,mi hapo mawazo hata hayapo hapo…anachekacheka kama vile kanipenda na mii nikawa naongeza confidence.

akanipeleka huko kwa kunyoa kwanza….tulitembea kama vyumba vitano mbele,yaani wale jamaa niligundua ile berbershop wamekodi floor nzima ya ghorofa….kila kitu kinafanyiwa chumba chake…

mimi kwenye kunyoa huko kwanza nashangaa wananihudumia watu watatu tofauti

alianza dada akanivalisha ile kitambaa na kunichana nywele….akaja jamaa alaninyoa halafu akamaliza jamaa mwingine wa kuchonga pamoja na ndevu…..akaja dada yule wa reception mwingine akanihamisha chumba….huko nilikuta wadada tu wamekaa kwenye makochi na kila mtu kavaa nusu utupu….akamkabidhi mmoja aanze sasa niosha…alisema unafanya scrub au steamer…nikasema steamer…yaani hapo anauliza anakupapasa shingoni,basi akaanza puliza ule mvuke…nilikaa pale karibia dakika 45 ananihudumia mimi tu…sasa hapa ndio machale yakaanza kunicheza,hawa mbona wakarimu hivi hawaa

sasa baada ya hapo wakasema kucha nazo zifanyiwe marekebisho pamoja na massage ya kichwa na shingo….mimi haya yote najua ni bonus…

tukamaliza zoezi ndio wakampigia yule dada wa reception…akaja.

aisee bili ananisomea inakuja 72,000/=🥹🥹🥹🥹….aibu ndio sipendi,kwa confidence ile ile nikazama mfukoni nikatoa 75,000/=….sema walinigundua chuplichupli nadhani nilivyoshindwa kujizuia kudai 3000/= ndio mmoja akauliza kwani kaka wewe wa wapi…..

ile natoka ndio nakumbuka kusoma bango….ni hasfi sijui ile mule wanaenda waliopata zao mawe ya madini…

lakini ni kujikaza tu *****….kupendeza nilipendeza sana harusini.
 
Kama kipato chako ni cha kuunga unga au cha mawazo ni vyema unapoingia hotel kubwa kuuliza bei za vitu kwanza kabla ya kuagiza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…