Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

Nashera bana paache tu, palitutembeza kwa miguu kutoka pale mpaka mjini Ili tusitumie nauli ya kurudi Mzumbe aisee.
 
Unaweza jikuta unaumbuka mjini pole kwa dhahama io
 
Mbona jumla inakuja tofauti? Inakuja tsh 30,000.
 
Ile iliyopo karibu na Viwanja vya furahisha??
 
Siagizi kichwakichwa. Lazima niletewe menu. Nikiona ghalama za hovyo nawapanga tuishie penye uwezo wangu au naamua kipi wasitumie.
 
Pole sana. Ndio uache sifa. Mimi hata nikiwa na 2m kwenye account siwezi peleka watu out kutumbua hela zangu. At least ziwe 5 na zaidi. Mambo ya kuanza kuwa na mawazo sitaki kabisa.
Yaani wewe una laki 1 unaenda beach za bei. Ungewapeleka kwenye mihogo huko ingetosha.
 
Siagizi kichwakichwa. Lazima niletewe menu. Nikiona ghalama za hovyo nawapanga tuishie penye uwezo wangu au naamua kipi wasitumie.
Sisi tulikuwa na hela ya kuvunja kikundi laki 450, tukaenda hotel kubwa kuona menu tukaagiza vinjwaji tukasepa. Tukaenda sehemu nyingine tukaaagiza tunachotaka na salio likabaki. Tulikua 6.
 
Sio mbaya umejifunza na muache kudharau wanaume wa dar..
 
Sionagi aibu kuuliza bei aisee.

Na kabla ya kumpeleka mtu eneo ambalo bills ni juu yangu lazima nikasurvey kwanza hilo eneo au hata mtandaoni au kwa watu wanaolijua.

Ukienda kichwakichwa pesa yako itakuuma sana.
 
Hahahaaa nimecheka, hivi shoppers plazza pale Dodoma ndo pakuniuzia breakfast 25,000 × 2 = 50,000 ~ wakati mm nilitegemea brekafast iwe 10,000]
Pale Kahawa cafe pembeni kushoto CHIPS KUKU ROBO 25,000, maji 3000 na juice 5000
Almanusura tuache mawigi na simu pona pona yetu ni huu mkopo wa Tigo Niwezeshe.

Hatutasahau
 
safi sana baba.. hio ndio akili kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…