Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

Pale Kahawa cafe pembeni kushoto CHIPS KUKU ROBO 25,000, maji 3000 na juice 5000
Almanusura tuache mawigi na simu pona pona yetu ni huu mkopo wa Tigo Niwezeshe.

Hatutasahau
Hahhaa watu hawakawii kujua ni uongo, sijhi kama bado ile cafe ipo. Nimeingia tu jambo la kwanza weusi hakuna watasha tu, nikasema no sweat tupo wawili mm na AmKatarna mwenzio, haya lete chai wanatuletea ka birika kadogo tujisevie, vijani, sukari, kisu, uma na kijiko. Kisha silesi, kiazi cha asili, gimbi na vipisi sijui vya nn. Nikanywa ila njaa ipo pale pale, sijasikia chochote tumboni haya lete bill 25,000 per person watu wawili 50k.
Hela ilikuwepo bahat nzuri ila ni hiyo bei na vilivyoletwa haviendani.
Nikaprintiwa risti nikajuta nikaondoka
 
Nilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.

Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.

Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.

Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.

Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.

Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare wote…yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.

Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.

…..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa

chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5

kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.

Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.

Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…

Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.

Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.

Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.

basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.

Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂
Hizi kadhia huwakumba Wakurupukaji kama wewe.
 
Yawezekana kweli pesa nyingi..Lakini kwakuspend zaidi ya watu 5 mbona figue ya kawaida.Ukija nextime utenge budget nzuri Mjomba.
 
Sisi tulikuwa na hela ya kuvunja kikundi laki 450, tukaenda hotel kubwa kuona menu tukaagiza vinjwaji tukasepa. Tukaenda sehemu nyingine tukaaagiza tunachotaka na salio likabaki. Tulikua 6.
Safi sana. Hakuna kuona aibu kuomba menu. Kama hutaki kuuliza basi mfuko wako uwe hauyumbi
 
Pole sana jamani.. juzi nilikua nimekaa kwenye kijiwe flan
ikaingia familia ya baba mama na watoto kama watatu.. watoto wapo very excited.. menu ilivyoletwa nikaona baba na mama wametizamana, watoto wakaanza kuchagua chakula,
Maskin baba akawanyanyua haooo wakaondoka🙌
Ile scene imeniongezea morali ya kusaka hela aisee.. kuna experience inafaa tuwape watoto wetu before waje wapewe na walimwengu.

2025 Mungu awasaidie wote Muingie sehemu mlidhani ni za hadhi ya juu zaidi yenu na ziwe kawaida tu kwenu.
 
Do not bite off more than you can chew.Maisha ya kuiga na kujifaragua matokeo yake ndio haya.Ungekufa na tai shingoni baada ya kuamua ulichoamua.Kulalama na kutafuta walioingia cha kike kama wewe haitakusaidia lolote.
Anajua km haitamsaidia chochote ila ameamua tu kushare na sisi ili wengine tuchukue tahadhari ni funzo pia na ni sehemu ya vichekesho kimtindo
 
Nilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.

Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.

Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.

Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.

Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.

Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare wote…yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.

Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.

…..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa

chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5

kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.

Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.

Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…

Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.

Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.

Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.

basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.

Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂
Safi sana mkuu.
You will be back strong. Pesa inatafutwa ili itumike
 
Ulitumia card gani hiyo ya Bank inayo access malipo kwa njia ya Card (machine) ? Ambayo inatumika kuongoza mshahara wako?
 
Hahaha pole sana ila nimejifunza kitu kimoja Wafanyabiashara tuna rule moja "lipia ulichokitumia/unachokiona" probably tupo close saba na hii Scenerio kinachotuokoa Tunauliza Bei ili Tu Negotiate
 
Ulizia menu usione aibu........ Nauliza hata kama tandale uzuri mimi aibu na macho kubadilika rangi plus kuforce tabasamu sitaki kabisa hizo mbanga
Kwako blood Ibn Unuq
Kijana wangu secretarybird zerominus10

Mshaurini mjomba kama mjomba
Anaagizaje chakula kabla hajajui gharama zake cha ajabu anakimbia asa anakimbia nini?

Chanzo cha tatizo ni nani?
 
Back
Top Bottom