Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

Niliagiza chakula, ilivyokuja bili nusura nikimbie niwaache watoto. Umewahi kukumbana na fedheha hii?

mungu mwema mudawote, alifanikisha usianze kudanganya housegirl wa watu uchape(upwiru usikiage tu ukiwa ugenini
 
Nilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.

Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.

Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.

Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.

Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.

Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare wote…yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.

Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.

…..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa

chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5

kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.

Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.

Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…

Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.

Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.

Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.

basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.

Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂

Katarama Bus Services baada ya kupigwa tukio la kikatili kabisa!

Umenivunja mbavu
 
Binti mmoja mkali enzi hizo dansa Fm marehemu sasa.
E bana katika kupiga sound,
Poa njoo mazoezini.
Nikazama huko sijui Chez ntemba Kino ndani mkwajuni studio.
Ile kufika demu kaja bia zao Heineken, sijakaa vizuri madansa wenzie nao hao km sita hivi.
Halafu hawaulizi ni salamu tu "aa shem pedeshee",
hapo supu , bia zinaenda Tu
Then hao waimbaji hawa wacongo wote hao km 12.
Walifakamia nyama bia, supu km hawana akili nzuri. alafu hao
Wakayeyuka😆.
Nilienda na kilo nikijua bajeti yetu wawili demu hamalizi.
Kuletewa bili "mama nene"🙆‍♂️
K
ilo 3+,
Nikamuita mshkaji aje arekebishe nae ana kilo tu si zaidi.
Duh ikabidi tuache simu, tukazirudia baada ya siku 2
Ndio ikatimia hela ya bill yote.
kwahali hiyo hata mbususu ulipewa?
 
Mimi juzi hapa tarehe 25 siku ya Christmas mida ya usiku jamaa yangu akaniambia tutoke out viwanja Usiku. Mda huo nilikuwa nishashiba vya kutosha nikasema hata nikienda viwanja sitaki nitumie zaidi ya elfu kumi. Basi tumeenda club moja kiingilio ilikuwa ni 5000,kila mtu akilipia Kiingilio chake,baada ya hapo nikaagiza KVANT ndogo nikaanza kupiga polepole huku nikiangalia watoto waziri wanavyo zungusha viuno.
Ilifika mda vibe likapanda nikasema nalala huko huko nakesha mpka asubuhi ndo niondoke,, ghafla dada zake na jamaa yangu wakaja pale club,wakaanza kucheza pale mezani kwetu,mda huo Niko tungi Sina hili Wala lile jamaa yangu akaniambia dada zake wanataka waondoke warudi nyumbani kwamba wechoka,,mm nikamwambia wao waende jamaa akaanza ku force kuwa hawezi kuenda akaniacha ikabidi nikubali tusepe,kufikia nje pale jamaa kuongea na dereva taksi akaambiwa wote kutubeba watano ni 15,000 huku ni sehemu ya Karibu sana,,basi nikapanda,tumefika mwisho madem wameshuka jamaa ananiambia Hana hela ya kulipa nimkope atanirudishia,duhhh iliniuma Sana Ila nikampatia,,Cha kishangaza mpka Leo hajanipa hio hela dahh iliniuma Sana aisee ile hela maana nilitaka kesho yake niende kwa dem wangu nimpe anunue kuku tu enjoy.
wala usiumie, siyo wewe, ni ukosefu wa pesa.
 
kuna siku moja niliingia saluni mwanza hakika sikumbuki mtaa….tulikua huku kwenye harusi ya jamaa yangu,huwa sipendi kufanya mambo kwa mkumbo…huwa natamani kufanya mwenyewe tena kwa kujaribu vitu vipya….

ila nakumbuka niliingia kwanza saluni eti ina sehemu ya reception…mimi hapo hata akili hainichezi machale…saluni gani ina reception bhana😀

mara yule muhudumu kaniandikisha jina na vitu nimeingia navyo…kavaa khanga tu,mi hapo mawazo hata hayapo hapo…anachekacheka kama vile kanipenda na mii nikawa naongeza confidence.

akanipeleka huko kwa kunyoa kwanza….tulitembea kama vyumba vitano mbele,yaani wale jamaa niligundua ile berbershop wamekodi floor nzima ya ghorofa….kila kitu kinafanyiwa chumba chake…

mimi kwenye kunyoa huko kwanza nashangaa wananihudumia watu watatu tofauti

alianza dada akanivalisha ile kitambaa na kunichana nywele….akaja jamaa alaninyoa halafu akamaliza jamaa mwingine wa kuchonga pamoja na ndevu…..akaja dada yule wa reception mwingine akanihamisha chumba….huko nilikuta wadada tu wamekaa kwenye makochi na kila mtu kavaa nusu utupu….akamkabidhi mmoja aanze sasa niosha…alisema unafanya scrub au steamer…nikasema steamer…yaani hapo anauliza anakupapasa shingoni,basi akaanza puliza ule mvuke…nilikaa pale karibia dakika 45 ananihudumia mimi tu…sasa hapa ndio machale yakaanza kunicheza,hawa mbona wakarimu hivi hawaa

sasa baada ya hapo wakasema kucha nazo zifanyiwe marekebisho pamoja na massage ya kichwa na shingo….mimi haya yote najua ni bonus…

tukamaliza zoezi ndio wakampigia yule dada wa reception…akaja.

aisee bili ananisomea inakuja 72,000/=🥹🥹🥹🥹….aibu ndio sipendi,kwa confidence ile ile nikazama mfukoni nikatoa 75,000/=….sema walinigundua chuplichupli nadhani nilivyoshindwa kujizuia kudai 3000/= ndio mmoja akauliza kwani kaka wewe wa wapi…..

ile natoka ndio nakumbuka kusoma bango….ni hasfi sijui ile mule wanaenda waliopata zao mawe ya madini…

lakini ni kujikaza tu *****….kupendeza nilipendeza sana harusini.
Walikuona umetoka pori sana
 
😄😄Ndo maan hata nikitolewa kabla sijaagiza nauliza bei hat km sinunui mm nijue ninaubavu nikikimbiwa kulipa nitaweza 😄
Kuosha vyombo sio poa
😄😄Ndo maan hata nikitolewa kabla sijaagiza nauliza bei hat km sinunui mm nijue ninaubavu nikikimbiwa kulipa nitaweza 😄
Kuosha vyombo sio poa
Kabisa kuuliza mapema kunakuepusha na aibu ndogo ndogo
 
Hahahaaa nimecheka, hivi shoppers plazza pale Dodoma ndo pakuniuzia breakfast 25,000 × 2 = 50,000 ~ wakati mm nilitegemea brekafast iwe 10,000]
Hahahaha asee wamekuonea, kidogo ninachojua huwa Kuna resident rates hata kwa hotel kubwa kubwa..
 
Kitu cha kwanza ukifika mahali , omba menu au kama hamna uliza bei kwa wahudumu !
Yaan mimi bora mnione bahiri ila ni muhimu sana !!
Unaweza umbuka vibaya sana !
ukishaonba nn kinafata::=walaji ni watoto na ndo waagizani ebo!! unataka uwashikishe menu afu iweje au kshike ww iweje uwakataze kula vya bei(nn maana ya matembezi hapo?)

FATA KILICHOKUPELEKA [emoji23][emoji23]

Huyo cha mtoto Dar free market kuna mtu alikutana na za uso
 
Matembezi ni kitu kizuri kwa watoto hata mimi hupendelea kumpeleka Dogo na mama mahali wakapate chochote kitu inaongeza upendo !

Ila kwenye kutembea kuna mahali unaweza kwenda huenda ni kiwanja kipya au unapachukulia poa ukaingia ukala vitu vile vile ambavyo ungekula au huwa mnakula sehemu nyingine Bill ikaja ukapiga ukunga sehemu ambayo ungetumia 100k unakuja kusomewa Bill inasoma 300k kuna mahala soda ni 4k-7k ila hiyo hiyo kuna sehemu inauzwa 2000 tu, chips kuku 25k wakati maeneo mengine hata kwa 10k utakula

Bora nusu shari kuliko shari kamili uliza bei ukiona hamuwezi mnahama na mama watoto na mtoto ! Yaan kuna haja gani kujimwambafai kwa mke na mtoto wangu wakati niwaoneshe ushujaa wa kulipia vitu 🤣🤣 wakati tukirudi nyumbani wote tunasuffer hayo madhara !
 
Kuna baa moja niliifakamia mida asubuhi holiday flani way back, sasa kilochotokea kumbe pale kila baada lisaa limoja ikifika saa 1 usiku bia hupandwa kwa 2.5k haijalishi ni brand gani na uliingia saa ngapi pale.
Kwa kua nilikua fresh sikudhalilika ila nikaishia kumfadhil staff mwenzangu ili asiabike kwan alikua anapiga Mji mkuu wa Namibia , ilipoanza kupanda bei yeye alikua hajui na akawa anazidi kuziagiza tu .
 
Mi 'watoto' walitaka nikawanunulie soda nikajua ni soda za kawaida! Walikuwa wawili tu, tukaenda sehemu tulivu wakaagiza vinywaji na kitimoto kilo moja. Ghafla wakawa wanne wawili wakasema hawali kitimoto wanataka nyamachoma ikabidi waagize kilo moja kama wenzao wawili. Zile 'soda' walizoagiza ni bia za yale machupa ya shingo ndefu. Mzee nikabaki na soda yangu nakunywa taratibu huku wale mabinti wanafakamia bia zao kwa fujo, wakaaigiza tena chupa za pili, changanya na madikodiko mengine bili ikaja ni laki moja ikateketea ndani ya muda mfupi na bajeti yangu ya kwenda kununua simu kali mpya ikavurugika palepale. Nilidhani wanakunywa soda kumbe ni bia, bahati yao nilikuwa na hela nikalipa huduma hiyo. Cha ajabu wale mabinti hawakulewa walikwenda baa kunyweshwa na masela wengine
 
Nilienda kutembea Dar es Salaam kwa dada yangu wakati wa sherehe hizi za christimass.

Basi tarehe 25/12 kama kawaida tulikwenda ibadani na kurudi nyumbani,kilichofuata ni maongezi tu ya kifamilia huku tukichoma nyama jioni na kunywa pombe pamoja na shemeji na marafiki zake.

Tarehe 26/12 nikataka na mimi onyesha msuli wangu kwa shemeji ili asinichukulie poa…Basi bwana nikawaambia leo niachieni hawa vijana nitoke nao out nao waone raha ya kuwa na mjomba,wako watoto wanne na dada wa kazi. jumla watano.

Basi wao wenyewe wakataja mahala wanataka kwenda…ni beach fulani hivi wamejenga vizuri sana na kuna michezo mingi sana ya watoto,vyakula na vinywaji.

Basi tukaondoka tukafika…kiukweli mimi nilidhani ni mahala naweza afford kulipia kila kitu na nilitenga 100,000/= nzima kwa ajili ya kutumbua.

Sasa kufika nikaambia kwanza vijana wapate chakula.Wakaagiza kila mmoja chipsi kavu pamoja na kuku nusu.Pia waliagiza juice freshi na kuna kamoja kiherehere kakaagiza pizza moja ya kushare wote…yule dada wa kazi kwa aibu za kikubwa aliagiza chipsi na mshkaki mmoja tu na juice.

Mahesabu yangu yalikua pale itakata kama 50,000/= hivi pamoja na michezo yao ile…wakamaliza kula,mimi mwenyewe nikaagiza bia zangu 5 pamoja na nyama choma ya mbuzi.

…..sasa game ikaanza karibia wanamaliza kula yule dada ndio akaniletea ile “menu”,lahaulaaaa

chipsi kavu-inasoma 6000/= mara 5
kuku nusu-inasoma 21,000/= mara 4
fresh juice-inasoma glass moja 6000/= mara 5
pizza moja-inasoma 35,000/=
mshkaki mmoja(niligundua wameandika fillet)-3500/=
nyama choma mbuzi—inasoma 25,000/= per portion
bia moja local ni 4000/= mara 5

kwa haraka haraka ilisoma kama 227,500/= kinyume kabisa na matarajio yangu.

Kwanza nilihisi baridi sana imenichapa sababu vitu vyote vishaagizwa na vingine vishaanza kutumika,watoto wanaenjoy sana na huwezi waambia kitu wakakuelewa.

Hapo wanasubiri washibe nikawalipe kila mmoja 5000/= ya kwenda kwenye michezo yao ya watoto…

Mimi bhana nikajitetea nataka kulipa kwa kadi…walete mashine,lengo langu hapa kubahatisha sababu ndio zilikua tarehe bosi anaingiza chochote kwenye account.

Ile kugusa tu pyaaaaa….nakuta sms inaingia umefanikiwa kulipia 227,500/= kwenda Utulivu beach resort,ikaja na sms ya muamala wa makato ya muamala kama 4000/= hivi.

Kwa kweli mood yote ilikata…kwa mshahara wangu hiko kiwango kilikua ni zaidi ya nusu yake mimi nimetumia kulipia watoto kula sehemu ambayo siyo level zangu….ila nikakaza kiume,ile kulipia kwa kadi nikaonekana doni sana pale.

basi na ile laki mkononi nayo nikaibunya mjini…..sahivi niko zangu kwenye katarama narudi zangu mkoani na somo.

Umewahi kutana na dhahama kama hii?!😂
nmecheka sana sas ww ndugu utaagizaje chakula bila kusoma kwanz menu!!?

shukur Mungu jomba ulikuw unaosheshwa vyombo😂😂😂
 
Nimecheka sana, eti kamoja kiherehere, mie nakumbuka nikiwa kikazi Dom mida ya saa 4 usiku nikaingia saloon nikwangue nywele, ile kumaliza bei kaniambia buku 5 na kunyoa kwenyewe ovyo, iliniuma hiyo buku 5
Kuna sehemu nilienda nyoa na rafiki yangu na kupaki mikweche miwili jamaa yangu kapigwa 20000 na scrubing ila mimi sikunyoa, siku nyengine nimeenda wameona mkweche mmoja umekuja, ile nanyoa namaliza dada mmoja na mshepu wake kaka hamia kiti kile pale, nikwambia wife atamind nikiosha, nikakwepa mshale wa 20000 😂😂
 
Back
Top Bottom